Tunaungana Na Afisi Kuu Ya Habari Ya Hizb ut Tahrir Katika Kampeni Dhidi Ya Ukatili Wa China Kwa Waislamu Wa Turkestan Mashariki

China ikiwa dola ya kibepari si tu inaendeleza unyonyaji kwa uroho wa rasilmali za nchi changa hususan za bara la Afrika na kuzitumbukiza nchi hizo katika mzigo usiohimilika wa madeni kwa ujanja wa mikopo. Bali pia China inaendeleza kampeni kali ya kiuadui na kikatili dhidi ya Uislamu na Waislamu wa Turkestan Mashariki. Eneo lililoporwa na China kwa mabavu na kulifanya kuwa sehemu yake.

Uadui wa China dhidi ya Waislamu ni athari ya chuki zake za asili katika tareekh tangu zama Utawala wa Manchu, na uadui waliotenda zama za Ukomunisti, ilhali uadui wa sasa unasukumwa zaidi na vita vya kimataifa dhidi ya Uislamu na Waislamu vinayoongozwa na madola ya Magharibi hususan Marekani. China katika zama za Ukomunisti ilishindwa kikamilifu kuifuta na kuingamiza dini ya Uislamu katika ardhi yao, licha ya kampeni yao kali na ya kikatili zama zile, hatimae Waislamu wa Uighur walipata nguvu wakaweza kuhifadhi na kulinda dini yao licha ya kuwa katika mzingiro wa hali ngumu.

Pamoja na hayo, China bado haijakata kiu yake kwa damu ya Waislamu kutoka mauwaji makubwa waliyoyatenda huko kabla, maangamizi ya taasisi za Kiislamu ikiwemo Misikiti kwa maelfu, kuuwa wanavyuoni wa Kiislamu nk. Hivi sasa inatumia mbinu tofauti tofauti kuendeleza yale yale. Inaendelea kuwaritadisha kwa nguvu Waislamu, kutenda mateso ya kimwili na kisaikologia, kuwauwa, kuwahilikisha kwa kisingizio cha ugaidi, na zaidi kuwafunga kikatili katika makambi maalumu ili kuwalazimisha waachane kabisa na kila athari ya Uislamu.

Mkakati wa China wa kuasisi makambi ya kuwafungia Waislamu ni katika mbinu ya kutaka kuondoa fungamano la Waislamu na jamii yao, na kuwatenga kando na athari za utamaduni wao (Uislamu). Hilo InshaAllah halitofanikiwa. Aidha, licha ya Ripoti ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mwezi Agosti 2018 kueleza kuwa katika Jimbo la Xinjiang, kuna kambi yenye Waislamu karibu milioni kwa ajili ya kuwabadilishwa dini (BBC). Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya Muungano wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu, idadi ya Waislamu katika makambi hayo ni kwa mamilioni. (Yenisafak)

Dhulma hii ya China kwa Waislamu wa Uighurs inatendeka ilhali hakuna hatua thabiti ya kuingilia kati kimataifa, ingawaje kuna matamshi ya kulaani hapa na pale, lakini kiuhalisia ni matamshi matupu, yakidhamiriwa kupoza tu na kuhadaa vilio vya kimataifa hususan za Waislamu, lakini kwa udhati hakuna hatua yoyote ya kivitendo.

Madola ya Magharibi yanayongozwa na Marekani, licha ya kujinadi kuwa ni vinara wa kulinda na kutetea ‘haki za binadamu’ lakini uzoefu unaonesha kuwa utetezi wao sio katika dhulma na majanga yanayowasibu Waislamu. Tumeshuhudia mengi katika dhulma na mateso ya Waislamu kama Afrika ya Kati, Myanmar, Kashmir, Ardhi Tukufu ya Palestine nk. Kote huko hakuna hatua zozote thabiti kukabiliana nayo.. Amma kwa upande wa nchi za Waislamu zilizotarajiwa zisimame kidete kivitendo kukinga na kukomesha uhalifu huu mkubwa, ziko kimya na nyengine zinashirikiana na wauwaji (China) kamwe ! zinajitia pambani kana kwamba haliwahusu.

Hizb ut Taahrir Tanzania inalaani uonevu na uadui wa China kwa Waislamu wa Uighur, pia inalaani udhaifu wa watawala wa nchi za Waislamu katika kukabiliana na dhulma hizi. Kwa upande mwengine, tunaungana bega kwa bega na kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kauli mbiu: “Vita vya China dhidi ya Uislamu ndani ya Turkestan Mashariki itakomeshwa na Khilafah Rashidah”. Tutashirikiana katika kufedhehi matendo maovu ya serikali ya China na pia kufedhehi ukimya wa Biladi za Waislamu.

Tunawaombea dua zetu ndugu zetu wa kike na kiume wa jamii ya Waislamu wa Uighur wamakinishwe zaidi kwa subra katika kipindi hiki cha ukatili mkubwa. Tunawakumbusha Waislamu wote, kuwa udhaifu wa watawala katika nchi za Waislamu ni dalili tosha ya kutofaa watawala hao kusimamia mambo na kuulinda Umma wa Kiislamu. Aidha, tunawakumbusha Waislamu wake kwa waume juu ya ufaradhi wa kufanya kazi na Hizb ut Tahrir Tanzania ili kurejesha tena dola ya Khilafah (katika nchi kubwa za Waislamu) ili kuwakomboa Waislamu wa Turkestan Mashariki na penginepo.

Tunawaomba Waislamu wote , na wote wenye hisia za ubinadamu ndani ya Tanzania na kila mahala kushiriki katika kampeni hii adhimu ili kufedhehi ukatili wa China kwa Waislamu wa Turkestan Mashariki.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

#Khilafah_Liberates_EastTurkestan

KUMB: 1440 / 04

Jumanne, 07th Jumada II 1440 AH 12/02/2019 CE

Maoni hayajaruhusiwa.