Tatizo la Mchanga Zanzibar
Katika ziara ya mwishoni mwa mwezi wa Februari mwaka huu katika Wilaya ya Kaskazini B’ Unguja katika vijiji vya Kiombamvua, Pangatupu na Donge chechele, Rais wa Zanzibar Dr. Ali Muhamed Shein aliwakumbusha wananchi juu ya suala la uwepo kwa uhaba mkubwa wa rasilimali ya mchanga itumiwayo katika harakati za ujenzi wa makaazi ya raia, maofisi, hoteli na madaraja, upigaji tofali nk.
Suala la uhaba wa mchanga liliibuliwa rasmi na serikali kupitia aliyekuwa Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na uvuvi Hamad Rashid amesema Zanzibar ndani ya mwaka 2017, ambapo alitangaza kuwa Zanzibar haina mchanga utakaokidhi mahitaji ya ujenzi, kutokana na kiwango kikubwa cha rasilimali hiyo kuchimbwa kwa kasi Unguja na Pemba.
Waziri huyo alisema utafiti uliofanywa kwa Unguja na Pemba umeonesha kuwa Unguja inachimba hekta 3 kila mwezi, na Pemba inachimba nusu hekta kila mwezi ambapo kwa mwaka 2016 uchimbaji huo umefikia tani millioni moja laki nane na arobaini na sita elfu.
Serikali inadai kuwa kutokana na uchimbaji mbaya wa mchanga usiozingatia utaalamu, imelazimika kuzuia harakati zote za uchimbaji, jambo lililosababisha ukosefu wa ajira kwa maelfu ya watu kuanzia madereva wa malori ya kubebea mchanga, wapakizi, wapiga matofali, fundi uwashi, vibarua, mwenye gari za punda na ng’ombe wanaobeba matofali, watengeneza makalbi ya visima nk.
Uchimbaji huu kwa kiasi kikubwa ulikuwa unasimamiwa na watendaji wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar lakini Cha kusikitisha na kushangaza tunaambiwa kwamba uchimbaji huo haukufanywa kwa misingi ya taaluma isiyoathiri mazingira
Kama kweli tatizo ni kubwa kiasi hicho hapana shaka athari zake ni kubwa na limegusa roho ya maisha ya wananchi, nalo ni suala la makaazi.
Kuna hatua mbalimbali za kivitendo zinazoweza kuchukuliwa kusaidia kuwaondolea dhiki kubwa wananchi kama vile serikali kujenga nyumba kwa bei nafuu ili wenye uwezo wauziwe, na wengine wakopeshwe kwa bei nafuu, Ila isiwe kwa kuangalia faida kwani zipo nyumba zinazokopeshwa kama za ZSSF ambazo bei yake iko juu sana.
Aidha, kutumika rasilimali mbadala za ujenzi ambazo nchi nyengine wanatumia. Hili litaondosha kutegemea aina moja tu ya rasilimali kama ilivyotokea kwa mchanga. Rasilimali hizo mbadala ni kama jasi ambayo Zanzibar ipo kwa wingi maeneo ya maweni ambako hakulimiki. Rasilimali hii ina uwezo wa kutumika kuwa mbadala wa mchanga kwani ina uwezo wa kutengezea matofali ikichanganywa na saruji, na vilevile kutumika kugandishia matufali na kupigia plasta.
Vilevile rasilimali ya mawe inaweza kuwa mbadala wa mchanga kwa kuyasaga kwa machine maalumu na kuzalisha unga ambao unasarifika kama mchanga kwa matumizi ya ujenzi. Namna hii ya matumizi ya mawe ni maarufu Uarabuni kama Omani, vilevile China kiasi cha wao kusahau kutumia mchanga katika ujenzi.
Pia kuna rasilimali ya kutumia udongo kwa matofali ya kuchoma ambayo pia ni maarufu sana duniani. Hii itawezekana kwa kuingiza mashine za kupigia matofali hayo na matanuri ya kuyachomea. Teknolojia hii inatumika sehemu nyingi hapa Tanzania, Malawi, Afrika ya Kusini, Zimbabwe nk.
Inaweza kusemwa pia kuagiza mchanga kama ifanyikavyo kwa saruji kama gharama zake zitakuwa rafiki kwa wananchi, lakini wasiwasi uliopo juu ya uagizaji huu ni kuwa wananchi wengi hawatomudu. Hili litawezekana pale tu serikali itakapoweka ruzuku maalumu ili kuwapunguzia wananchi mzigo huo.
Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah ina uwezo wa kuliondoa tatizo hili kwa ukamilifu kwa namna ifuatayo:
Dola ya Khilafah itatenga maeneo maalum (himma) ambayo ni milki ya Ummah kwa ajili ya kuchimba mchanga, baada ya kufanyika uchunguzi yakinifu na kuonesha kuwa hakutakuwa na madhara kwa jamii. Imepokewa Mtume SAAW “alitenga eneo Naqee kwa ajili ya malisho”. Pia Makhalifa Umar na Uthman walitenga maeneo maalum ya ardhi kwa ajili ya matumizi maalum na masahaba hawakuwakosoa. Jambo hilo ni ijmaa.
Dola ya Khilafah itasimamia ipasavyo maeneo makubwa yenye rasilmali ya mchanga na kamwe hayatoruhusiwa kumilikiwa na mtu binafsi, makampuni wala serikali, bali yanakuwa milki ya Umma, na serikali itasimamia kwa utaratibu mzuri watu kutasarafu na rasilmali hiyo kwa njia nzuri bila ya kuharibu mazingira au kumilikishwa iwe kampuni au watu binafsi
Amesema Mtume SAAW:
“Watu ni washirika katika mambo matatu, malisho, moto na maji” .
Hadithi hii inahusisha kila aina ya rasilmali ambayo kwa wingi wake na maumbile yake ikimilikiwa na mtu binafsi itawaingiza wengine katika dhiki na tabu kubwa.
Pia kwa kuwa dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashidah itaunganisha ardhi zote za Waislamu, rasilmali za upande mmoja zitatawanywa kuwafikia wengine, sio kwa dhamira ya kibiashara bali kwa kuwa rasilmali hizo ni milki ya Umma wote kwa pamoja. Kama ilivyotokea zama za Khalifah Umar (ra) mwaka wa 18 AH ilipotokea njaa Madina, na chakula kikasafirishwa kutoka Misri.
Kwa upana wake dola ya Khilafah utalikabili tatizo la makaazi litakaloibuka kwa ukosefu wa mchanga kwa kuwataka wenye uwezo wawasaidie wasiokuwa na uwezo. Hili liko katika pande mbili. Upande wa swadaka, kama Mtume SAAW alivyohimiza kivitendo kuwataka Answar wawasaidie Muhajirina. Kama yeye Mtume SAAW mwenyewe alivyopatiwa makaazi na Abu Ayoub al Answar (ra). Lakini pia jukumu hili lipo kwa upande wa ulazima, ikiwa asiyekuwa na uwezo, ana ndugu wenye uwezo. Na kubwa zaidi ni jukumu la dola ya Khilafah kama msimamizi wa raia kudhamini makaazi kwa raia wake wasio na uwezo.
Katika mwezi huu wa Rajab, wakati tukikumbuka tukio kubwa la msiba wa kuangushwa dola yetu tukufu ya Khilafah, ambayo ndio mlezi na msimamizi kwa raia kuwapatia makaazi na mengine. Ni wajibu tusimalizie kusononeka tu , bali tufanye kazi kwa mujibu wa njia ya Mtume SAAW isiyohusisha nguvu wala silaha kuirejesha tena dola hiyo.
Risala ya Wiki No. 32
11 Rajab 1440 Hijri | 18-03- 2019 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania
https://hizb.or.tz/
https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania
#RajabFarajaKwaWalimwengu
Maoni hayajaruhusiwa.