Miaka 60 Ya Uhuru Bado Umeme Na Maji Ya Mgao
بسم الله الرحمن الرحيم
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tarehe 9 Disemba, Tanganyika / Tanzania itaadhimisha miaka 60 ya uhuru iliyoupata kutoka kwa Uingereza 1961, baada ya awali kuwa chini ya ukoloni wa Ujerumani kabla ya nchi hiyo kushindwa katika Vita vya Kwanza.
Pamoja na kupata kinachoitwa uhuru, bado Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo inayoendelea sasa ya uwepo mgao wa umeme na maji, vyote viwili vimejiri kwa sababu kadhaa ikiwemo athari ya ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ni jambo lisiloingia akilini mpaka leo hii, tatizo la umeme ni kubwa baada ya viwango vya maji katika mabwawa mengi ya mitambo ya umeme kupungua. Hali hiyo imeathiri uzalishaji umeme katika baadhi ya vituo kama Kihansi, Kidatu na Pangani. Hali iliyopelekea nakisi / upungufu katika gridi ya taifa kwa karibu megawatts 345, sawa na asilimia 2. Zaidi ya yote hayo ni asilimia 15 tu ya raia ndani ya Tanzania ndio wanaotumia huduma ya umeme.
https://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/kenyaa/428.html
Kuhusiana na upungufu mkubwa wa maji hususan katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam ambalo zaidi hutegemea Mto Ruvu, mto huo umekuwa chini ya uzalishaji wa viwango vya kawaida vya lita 270 milioni kwa siku, kukiwa na upungufu wa lita milioni 70
Suala la mabadiliko ya tabia nchi kweli halikwepeki. Lakini kuna sababu nyengine nyingi zinazosababisha qadhia hii, ikiwemo usimamizi mbovu, kukosekana uoni mpana hususan katika suala la umeme, kwa kutowekeza zaidi katika vyanzo anuai vya uzalishaji nishati ya umeme, na badala yake kuwekeza nguvu zaidi katika miradi inayozalisha umeme usiotosheleza.
Ni zaidi ya aibu kwamba Tanzania inakabiliwa na tatizo la maji na umeme na mengine mengi kwa zaidi ya nusu karne tangu kupata uhuru wa bendera, ukijumlisha pamoja na uwepo kiwango kikubwa mno cha rasilmali mbalimbali ikiwemo kiwango kikubwa cha gesi asilia inayokadiriwa kuwa trilioni 57 cubic feet. Jumla ya uzalishaji wa bilioni 110 cubic feet kwa mwaka kutoka katika visima vitatu vilivyopo kusini ya Tanzania. https://www.tanzaniainvest.com/gas
Pia Tanzania ina maandini mbali mbali ikiwemo kiwango kikubwa cha dhahabu, kiasi cha kuwa nchi ya tatu katika uzalishaji dhahabu katika Afrika, nyuma ya Ghana na Afrika ya Kusini. Bila ya kusahau uwepo kwa kiwango kikubwa cha maadini ya urani (uranium). Kwa mujibu wa kampuni ya Uchimbaji Maadini ya Australia, Tanzania ina kiwango kikubwa cha maadini ya urani kuweza kuwa miongoni mwa nchi tano bora barani Afrika.
Na kwa upande wa rasilmali ya maji, Tanzania ina vyanzo vikubwa vya maji kama Bahari ya Hindi upande wa mashariki, Ziwa Victoria ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa ulimwenguni likiwa limetanda katika mita za mraba wa 65,583 (sq mi) ambapo Tanzania pekee ina sehemu ya 49% ya 33,700 ya kilomita mraba. Sehemu kubwa zaidi ukilinganisha na majirani zake (Uganda na Kenya).
Bila ya kutaja uwepo wa Ziwa Tanganyika, ziwa la pili kuchukuwa ujazo mkubwa duniani, na kuwa na kina kikubwa katika Afrika, likiwa na ujazo mkubwa zaidi wa maji mwanana na baridi.
Chanzo cha madhila, umasikini na kukosa maendeleo ndani ya Tanzania, Afrika na zote changa ni kutokana na unyonyaji na uroho wa mfumo wa kimagharibi wa ubepari, nchi hizo kukosa uhuru wa kweli wa kujiamulia
mambo yao pia nchi changa zinakosa uoni mpana kwa kule kukosa nguzo thabiti ya kimfumo kuwaongoza katika mambo yao.
Muda umeshawadia kwa watu wa chi changa ikiwemo Tanzania kuamka kwamba Ubepari kamwe hautosita ajenda yake ya kinyonyaji kwa nchi changa. Njia pekee ya kujivua na hali hiyo ni kung’oa mfumo muovu wa kibepari, na kuweka mfumo mbadala wa Uislamu unaotokamana na wahyi kiwahyi. Chini ya dola yake ya Khilafah itaukomboa ulimwengu na ubinadamu jumla kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo na kuondoa moja kwa moja minyororo yote ya unyonyaji.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
REF: 1443 / 01 | Monday, 24th Rabii’ II 1443 AH | 29/11/2021 CE |
Maoni hayajaruhusiwa.