Maneno Mazito Na Ya Kweli Kutoka Kwa Wakili Mahiri Kuhusu Uonevu Kwa Mgongo Wa Sheria Ya Ugaidi

بسم الله الرحمن الرحيم

“Akikamatwa mtu kwa tuhuma za wizi atahojiwa juu ya tuhuma maalum ya tukio maalum la wizi analotuhumiwa nalo.
Akikamatwa mwenye tuhuma ya mauaji atahojiwa kwa jambo maalumu la tukio maalum analotuhumiwa nalo.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa makosa mengine. Ndivyo sheria itakavyo. watuhumiwa wahojiwe kwa tukio maalum, labda tu endapo mtuhumiwa anahusishwa na makosa mengine zaidi ya kosa moja.
Lakini hata hivyo bado maswali hayawezi lenga dini yake au imani yake.
Kwanini inapokuja suala la ugaidi mtu huwa hahojiwi kwa tukio maalum bali huwa ni mzunguko wa maswali (mengi) yanayohusu dini yake na sio tukio mahsusi la ugaidi?
Kuhoji nini maarifa ya Uislamu, kina nani wanafundisha maarifa ya Uislamu, fiqhi katika Uislamu ni nini. Ina mantiki gani katika sheria ya makosa ya ugaidi na hata makosa mengine ya jinai kwa ujumla?
Ni vizuri kuwa wazi ili tujue inaposemwa tunamhoji mtu kwa tuhuma za ugaidi mnamaanisha nini au tuhuma yenyewe haswa ni nini katika huo ugaidi unaodaiwa? Vinginevyo ni kuumiza haki za watu na kujenga utengano “.
Wakili Juma Nassoro
kutoka post yake ya Facebook ya tarehe 28 Septemba 2019
Maoni:
Huo ndio uhalisia wa namna sheria ya ugaidi na mapambano yake kwa jumla yalivyokusudiwa kuonea, kuuwa, kudhulumu na kutesea Waislamu kwa msingi wa Uislamu wao, na hilo linapopata watendaji wenye chuki huzidisha chumvi kwenye kidonda.
Ni muda wa kujirekebisha sasa, tunavitaka vyombo vya kusimamia haki kuwaachia huru watuhumiwa wote wa ugaidi mara moja au kesi zao kuanza kusikilizwa kwa haraka. Kisingizio cha kutokamilika ushahidi kwa miaka ni guo la kujificha mgongo wazi la uonevu na dhulma.

Maoni hayajaruhusiwa.