Kumalizwa Kwa Waislamu wa Mashariki ya Turkestan

Uislamu uliingia China na Turkistan ya mashariki katika zama za umawiyah mwaka 96 Hijri, Na Uislamu ukaendelea kuwepo mpaka zama za Abasiyah, tokea zama hizo Waislamu wanaishi kwa amani Huko Turkestan na pia kuishi ndani ya China kwa amani bali walikua wakishiriki katika nyanja zote za maisha na wakafikia vyeo vya juu katika serikali na jeshi, mpaka ilipoingia familia ya Manchu katika utawala wa China mwaka 1054 Hijria Sawa na 1644 Miladia hapa ndipo ukaanza muhula wa Manchu na ikaanza kampeni ya kuwakandamiza Waislamu ndani ya China jambo lililopelekea Waislamu kubeba silaha mwaka 1058 hijria Sawa na 1648 miladia wakitaka Uhuru wa kidini, jambo lililopelekea kumwagika kwa damu nyingi na kupoteza roho nyingi, kwani maelfu ya waislamu waliuwawa na kuzimwa Mapinduzi yao kwa uovu mkubwa, ilifikia kiwango cha kufa kwa halaiki ya watu, kama wanavyoeleza wanahistoria.

Mauwaji dhidi ya waislamu yalipoisha ndani ya China Macho ya wachina yakaelekezwa Turkestan, China ikaingia katika vita vikali pamoja na waislamu wa Turkestan na wakaitawala mwaka 1174 Hijria sawa na 1760 miladia baada ya waislamu kudhoofika, na Serikali ya China ikauwa wakati huo waislamu milioni moja.

Baadhi ya maalumati kuhusu Turkestan :

Mji wa Kashgar ni katika miji muhimu sana ya Turkestan ya mashariki na mji huu ulikua ukiitwa (Bukhara ndogo) kwa uwingi wa wanazuoni katika mji huo na madrasa za elimu.

China iliwauwa waislamu wa Turkestan tangu ilipoinyakua ardhi hiyo mpaka Leo zaidi ya mashahidi wa Bosnia Iraq Afghanistan Chechnya na Palestine na hukadiriwa kwa mamilioni.

Mwaka 1952 China iliwanyonga Watu elfu 120 ndani ya mashariki ya Turkestan, wengi wao wakiwa maulmaa wa sheria, Akiyataja hayo burhan shahidiy aliyekua waali wa Turkestan ya mashariki zama hizo.

Katika muda wa 1949 miladia mpaka 1979 China ilivunja misikiti elfu 29 ndani ya Turkestan.

Kutokea mwaka 1997 miladia, mpaka sasa China imefunga msikiti 1200 ndani ya Turkestan, na baadhi ya misikiti ikaigeuza kua Makao ya chama cha kikomonisti au ofisi zao.

China imetia moto markaz za kuhifadhisha qur’an elfu 370 ndani ya Ürümqi mji mkuu wa Turkestan zama hizi.

Serikali ya China imewatuma wafanyakazi elfu 54 kutoka Turkestan katika kambi za kazi ngumu, wakawakusanya maimamu na kuwalazimisha wacheze densi.

China imewachoma wakiwa hai wanawake wenye hijabu kwa kukataa kuvua hijabu.

Kwa sasa China inazuilia karibia waislamu milioni moja katika mkoa wa Turkestan katika kambi zake za uzuizi.

اللهم أعد لنا خلافتنا ليعود بها عزنا ..ثم تكون خلافة على منهاج النبوة
Ewe mola turudishie khilafah yetu ili izza yetu irudi

Aameen.

Maoni hayajaruhusiwa.