Kukamilika Kampeni ya “Ufunguzi wa Constantinople”

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut Tahrir / Tanzania imekamilisha kampeni ya “Ufunguzi wa Constantinople” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwezi (Jumada al-Awwal ) na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Kampeni hiyo ya aina yake na ya kilimwengu ni kwa ajili ya kuadhimisha tukio la Ufunguzi wa Constantinople (makao makuu ya mtawala Heraclius), mji uliovamiwa kijeshi kuanzia tarehe 26 Rabii’ al-Awwal na kutiwa mikononi tarehe 20 Jumada al-Awwal 857 Hijri, sawa na tarehe 5 Aprili mpaka tarehe 29 Mei 1453 Miladi.

Kampeni hii iliyotekelezwa kwa maelekezo ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mashuhuri (Allah SW Amlinde) ilibeba kauli mbiu isemayo: “Bishara iliyotimia……….na bishara nyengine zinafuatia”, huku ikijikita zaidi kufafanua yafuatayo:

1. Fathi (Ufunguzi) ya Constantinople inadhihirisha utukufu na izza ya Uislamu, wakati Uislamu unapotabikishwa (kutekelezwa kimfumo) kiasi cha ukafiri kukosa nafasi kabisa.

2. Kuwaliwaza Umma wa Kiislamu juu ya kutimia bishara nyengine tatu za Mtume SAAW kama vile ilivyotimia ya kwanza. Bishara hizo tatu ni : Waislamu kuifungua Rome, kurejea Khilafah kwa Manhaj ya Utume na Waislamu kuwapiga na kuwashinda vibaya Mayahudi

3. Kuwakumbusha Waislamu juu ya uwajibu wa kufanya kazi ya kuirejesha tena dola ya Khilafah Rashidah, huku wakitambua kwamba nchi za kikafiri za kimagharibi, pamoja na vibaraka waliweza kuiangusha Khilafah mnamo mwaka 1342 Hijria / 1924 Miladi, na bado wanaendelea na juhudi kubwa kwa kutumia mbinu na ala mbali mbali ili kuizuiya Khilafah isirudi tena.

Kampeni hii ilifanyika sehemu mbali mbali ndani ya Tanzania ikiwemo ndani ya majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Mtwara, (Mkoa wa Kusini), Tanga (Kaskazini Mashariki) nk. Huku kampeni ikitumia ala na mbinu mbalimbali kuifanikisha, kama vile: kutawanya nakala ya khotuba ya Amiri (inayozungumzia ufunguzi huo), mihadhara ya misikitini, kalima nje ya misikiti, kutoa bayana, khutba za Ijumaa, video fupi fupi, matumizi ya mitandao ya kijamii, pia baadhi ya wanaharakati wa Hizb waliweza kuipaza kampeni hiyo kupitia vyombo vya habari ikiwemo Tv na redio, kama vile kituo cha Island Tv na Redio – Chuchu fm. ( vya Zanzibar)

Sambamba na kuwashukuru kwa dhati wale wote walioshiriki na kuchangia kwa namna moja au nyengine kufanikisha kampeni hii, tunamuomba Allah Taala Atupe mafanikio matukufu yanayotokana nae pamoja kutulipa malipo makubwa.

KUMB: 1441 / 01

Alkhamis, 21 Jumada I 1441 AH

16/01/2020 CE

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

#ﻓﺘﺢ_ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻨﻴﺔ
#ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻴﻨﻴﺔ
#ConquestofIstanbul
#İstanbulunFethi
#istanbul

Maoni hayajaruhusiwa.