Kujikinga na Kutotosheka
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ * وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ * فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ * وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّى
“Na ama mwenye kufanya ubakhili na akajiona anajitosheleza, na akadhibisha lililo jema. Tutamsahilishia yawe mazito. Na mali yake yatamfaa nini wakati atakapokuwa anadidimia (katika maangamivu)?”
[Al-Lail: 8-11]
Ni kiwango gani cha mali kinachomtosheleza mwanadamu kuishi maisha ya furaha? Swali hili laweza kujibiwa kwa njia zaidi ya mia moja.
Ama Uislamu umemfanyia mwanadamu wepesi kwa kumuunganishia baina ya matarajio yake na matakwa ya Allah (swt). Allah (swt) amempa mwanadamu haki kamili kufanya jitihada za kujipatia kile anachoweza kukipata miongoni mwa vilivyo halalishwa, na katika historia yetu tuna mifano kadha wa kadha ya watu waliokuwa na utajiri mkubwa na kufurahia manufaa yake na kila fursa ya kutoa kwa ajili ya Allah ilipo wadia kamwe hawakufikiria mara mbili. Hili lawezekana tu ikiwa Muislamu atatambua kwamba saada (furaha) ya kikweli iko katika kupata radhi za Allah (swt) na jambo la pekee ambalo mwanadamu anastahili kutokinai nalo ni akhera.
Ukweli ni kuwa, kuporomoka kwa Waislamu kumetokana na kutotosheka na khiyana na nidhamu ya ulafi ya
kirasilimali iliyo wageuza watu kuwa mashini za uchumaji pesa. Ni ulafi huu ndio uliomfanya Abdul Aziz ibn Saud kuuza Ummah wa Kiislamu na Akhera yake kwa makafiri. Na pia ni ulafi huu ndio unaowafanya watawala vibaraka kutekeleza uhalifu mbaya dhidi ya watu wao wasiokuwa na hatia. Huu ndio ulafi uliopelekea serikali ya Uturuki kuwatelekeza watu wa Syria kufa; ulafi uliolizuia jeshi la Pakistan kutoikomboa Kashmir; ulafi wa Wasaudi ndio uliotia fora zaidi. Ulafi wa utawala na pesa; huu ndio uliolemaza uongozi wa Waislamu.
Khalifah Umar Bin Abdul Aziz (rh) aliwahi kusema;
“Moyo wangu kamwe haukinai mazuri yoyote ya ulimwengu unayopewa bali hutaka mazuri zaidi, na nilipopewa lile ambalo ni kubwa zaidi kuliko ulimwengu, moyo wangu ulilitamani hilo nalo ni, akhera.”
Ni vipi basi itakuwa miondoko ya watu wa kawaida ikiwa hao walio ngazi za juu
watakuwa na tabia kama hii?
Sio tu ulafi wa mali na utawala ndio unaogandamiza Ummah wetu; bali pia kutotosheka na maisha. Kutotosheka huku kumeenea kwa sura ya ubinafsi na utaifa na kumetupa chaguo. Ikiwa naweza kuokoa siku yangu ya leo kupitia kuwauza ndugu zangu na dada zangu, basi hilo litakuwa ni chaguo sahihi.
Mtume wa Allah (saw) amesema:
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم يوشك الأمم أن تداعى عليكم كما تداعى الأكلة إلى قصعتها فقال قائل ومن قلة نحن يومئذ قال بل أنتم يومئذ كثير ولكنكم غثاء» كغثاء السيل ولينزعن الله من صدور عدوكم المهابة منكم وليقذفن الله في قلوبكم الوهن» قال حب الدنيا وكراهية الموت
“…na Allah ataondoa vifuani mwa maadui zenu hofu kwenu na Allah atazigonga nyoyo zenu kwa al-Wahn” Mmoja akauliza, ‘Ewe Mtume wa Allah, al-Wahn ni nini?’ Akajibu, “Kupenda dunia na kuchukia kifo.”
Mapenzi haya ya vitu vya kimada yaliyo penyezwa polepole yameuteka mujtamaa wetu. Tumegeuka kuwa watu tunaojali vitu na matabaka. Ulafi wa kufikia “kiwango cha juu” unawasukuwa watu kwenye haramu. Fesheni mpya ya gari kuwa nalo ni kitu cha lazima; najali nani ikiwa nitachukua mkopo wa riba benki almuradi niwe nalo. Matangazo ya kibiashara katika runinga yanaonesha kuwa mume atapewa kikombe cha chai ikiwa tu atakubali kuchukua mkopo kutoka benki ili mkewe aweze kurembesha nyumba yake. Hivi majuzi, mtindo mpya ulianzishwa nchini Pakistan kwa jina la sherehe ya harusi ya muda mrefu. Sherehe hii ya harusi iliendelea kwa muda wa mwaka mmoja na kusababisha shoo kufanywa kutokana nayo. Ukweli ni kuwa, hili, lilikuwa ni kuanzisha mtindo mpya wa kuonesha utajiri ambao hautachochea tu wivu bali pia ulafi kwa wengine kutaka zaidi, kwa njia yoyote iwayo.
Ni lazima tukumbuke kuwa kutotosheka ndiko kuliko wafanya Mayahudi kuchukiwa sana machoni mwa Allah kwani kuliwapelekea kumuasi Yeye (swt):
وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَى حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُواْ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ وَاللُّ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ
“Na kwa hakika utawaona ni wenye pupa ya kuishi (Mayahudi), na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Allah anayaona wanayo yatenda. ”
[Al-Baqara: 96]
Sisi, Waislamu wa leo, ni lazima tuzingatie na kufahamu kuwa kadhia hii ya kinafsiyyah ya ulafi yaweza
kutupelekea kumuasi Allah (swt) na yaweza kutupelekea kikamilifu katika upotevu kutokana na matamanio yetu. Hatuna budi kujifunza njia za kujitolea na ni lazima tuzungumzie juu ya haki zetu na za ndugu zetu ambazo zinapunjwa na watawala walafi walioko leo ili tufaulu hapa duniani na kesho akhera.
Masoud Salim Mazrui
Inatoka Jarida la Uqab: 17 https://hizb.or.tz/2018/06/01/uqab-17/
Maoni hayajaruhusiwa.