Khilafah ni Faradhi kabla na Baada ya Mapinduzi

0

ﺑﺴﻢ ﷲ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

Ingawa Allah (s.w.t) alitufaradhishia usimamishaji wa Khilafah, ambayo ni utawala jumla kwa waislamu wote duniani kwa ajili ya kusimamisha sheria za kiislamu na kubeba ulinganizi wa kiislamu katika ulimwengu, na ingawa sheria imetutaka kubakia bila ya khilafah kwa siku tatu tu, na sio zaid ya hapo, lakini bado tunakaribia miaka 100 ya kutawaliwa na mfumo wa kisekula ambao ni zao la mifumo ya binadamu kutoka katika sheria za ufaransa na uingereza na kutoka katika mabongo ya watu, wakati ambapo sheria ya Mungu haitumiki tena katika uhalisia.

O Waislamu: Usimamaishaji wa Khilafah ni faradhi kwa waislamu wote katika nchi zote katika dunia. Usimamishwaji wake ni jukumu na hakuna chaguo katika hilo na hakuna mjadala katika hilo. Kwa hakika ni moja katika madhambi makubwa yanayohitajia adhabu ya Mungu kama vile faradhi ya swala na zakat na jumla ya faradhi nyingine. Ni faradhi na haina uhusiano na mapinduzi ya Ash sham au mapinduzi mengine katika nchi za Kiislamu. Lakini zaidi ni faradhi kabla na baada ya mapinduzi. Ni mama wa faradhi zote na ndio kichwa cha faradhi.

Ushahidi wa ufaradhi wa kusimamisha khilafah unapatikana katika Qur-an, Sunnah na Ijmai swahaba.

Kutoka katika qur an Allah amemzungumzisha Mtume (saw):

ﻓَﺎﺣْﻜُﻢ ﺑَﻴْﻨَﻬُﻢ ﺑِﻤَﺎ ﺃَﻧﺰَﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻭَﻟَﺎ ﺗَﺘَّﺒِﻊْ ﺃَﻫْﻮَﺍﺀَﻫُﻢْ ﻋَﻤَّﺎ ﺟَﺎﺀَﻙَ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﺤَﻖِّ

“Hukumu baina yao kwa kile alichoteremsha allah na wala usifate matamanio yao baada ya kuwa haki imekufikia”

[Al-Ma’ida: 48].

Allah (swt) anasema:

ﻭَﺃَﻥِ ﺍﺣْﻜُﻢْ ﺑَﻴْﻨَﻬُﻢْ ﺑِﻤَﺎ ﺃَﻧْﺰَﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻭَﻻ ﺗَﺘَّﺒِﻊْ ﺃَﻫْﻮَﺍﺀَﻫُﻢْ ﻭَﺍﺣْﺬَﺭْﻫُﻢْ ﺃَﻥْ ﻳَﻔْﺘِﻨُﻮﻙَ ﻋَﻦْ ﺑَﻌْﺾِ ﻣَﺎ ﺃَﻧْﺰَﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﺇِﻟَﻴْﻚ

“Na hukum , baina yao kwa kile alichokutelemshia allah na usifate matamanio yao, na kuwa makini nao, wasikufitini ukaacha ambacho allah amekuteremshia.”

[Al-Ma’ida: 49]

Na kutoka katika Sunnah, imesimuliwa na Muslim kutoka kwa Nafi kwamba alisema: Umar aliniambia : nilimsikia Mtume wa Allah (saw) akisema:

مَنْ خَلَعَ يَدًا مِنْ طَاعَةٍ، لَقِيَ اللَّهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِ

“Mwenye kuondoa mkono wake katika utiifu wa kiongozi atakutana na allah bila hoja yoyote, na mwenye kufa na hakuna katika shingo yake kiapo cha utiifu kwa khalifah atakufa kifo cha jahiliyya

Mtume amefaradhisha kwa kila muislamu kutoa bay’ah (kiapo) katika shingo yake na amemuelezea yule anaekufa bila kutoa bay’ah atakua amekufa kifo cha kijinga. Uwepo wa Khilafah ndio hupelekea bay’ah au kiapo katika shingo ya kila Muislamu, na bay’ah hutolewa kwa khalifah pekee. Pia muslimu ameripoti kutoka kwa Al-a Araj kutoka kwa Abuu Hurayra kutoka kwa Mtume (saw) kwamba Mtume amesemaُ

إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ، يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ، وَيُتَّقَى بِهِ

“Kiongozi ni ngao, watu hupigana nyuma yake na huwalinda”

Na katika Ijamaa Swahaba, radhi za Allah ziwe juu yao, walikubaliana umuhimu wa kupata mrithi wa mtume (s.a w) baada ya kifo chake. Walikubaliana kumpata mrithi wa Abu Bakar, kisha Umar, kisha Uthman kila baada ya kifo cha mmoja wao. Uthibitisho wa Ijmai ya maswahaba katika kumsimika Khalifah umekua wazi kwa kule kuchelewa kumzika Mtume (s.aw) baada ya kifo chake. Wakawa wanashughulishwa katika kumsimika mtawala baada yake ingawa kuzika maiti haraka baada ya kufariki ni faradhi iliyowekwa. Faradhi kubwa ya Khilafah ndio iliyopelekea Maswahaba kumuacha Mtume amelala mausiku mawili katika kitanda, wakiwa wanafanya juhudi ya kumpata kiongozi badala yake.

Maswahaba wote wamekubaliana wakati wote katika maisha yao kwamba Khalifah lazima apatikane, na ingawa kuna wakati hawajakubaliana kuhusu mtu chaguliwa kama khalifah Lakini hawajatofautiana katika kumsimika kiongozi, sio katika kifo cha mtume wala Khalifah yoyote

Hata wakati ilipokua wazi kwamba Umar (ra) yupo katika hatua za kifo kwa kushambuliwa kwa kisu, aliteua Maswahaba sita katika kinyanganyiro cha ukhalifah, miongon mwao ni Uthman, Aliy, Talha, Az zuber, Abdul Rahman bin Auf na saad bin Abi Waqas, na iliamuriwa kwamba kama hawatakubaliana kumpata Khalifah ndani ya siku tatu basi wakatwe vichwa. Na hivyo, aliagiza waislamu hamsini wanaume wakiongozwa na Abu talha al ansar kumuua yoyote atakaepinga.

O Waislamu katika Ash sham:  Tangu kuanguka kwa khilafah, tunaishi katika uvamizi  wa mkoloni wa kikafiri, na zaidi nikwa viongozi mawakala ambao ni wabaya zaidi kuliko mabwana zao dhidi ya waislamu, na ukweli ni kwamba kama tungelikua na Khilafah basi ubepari usingeingia kwa waislamu na kwa binadamu yoyote

O Waislamu katika  Ash sham. Ushindi wa mapinduzi na mafanikio yake unaharibiwa na viongozi makatiri wa Ash asham na vijitawala vyao vya kisekula kwa kurejea kwetu kwa allah, kutafuta msaada na ushindi kutoka kwake pekee, na kwa kubeba maamrisho yake na kuacha makatazo yake. Hata tukishambuliwa na dunia nzima , tunasema: yoyote ambae Allah yupo upande wake, ambae ananguvu na yule ambae Allah hayupo upande wake mwenye nguvu za kuwa nae ?? Sisi katika Hizb ut tahrir tutabakia kuwa ni washauri waaminifu kwa Ummah, tunasema ukweli, tunamuogopa Allah pekee. Hivyo basi, tumelengwa katika kampeni na wimbi katika kutengenezewa uongo na shutuma muda wote na watu wa sekula baada ya maandamano ya idlib na huo sio mwisho. Pamoja na hivyo, , hili linatuongezea nguvu na kuweka wazi ukweli tunaoufata, tukisukumwa na ahadi ya Allah ya ushindi na nguvu. O enyi watu wa Ash Sham ! Kuweni wamoja na shikamaneni na makubaliano kati yenu ya kusimamisha Khilafah kupitia njia ya Utume, na mfanye kiapo na viongozi wenu kwa ajili ya kumuabudu Allah pekee na msimuabudu yoyote zaidi yake na msimamishe  sheria zake  na msimuabudu yoyote ila yeye Allah pekee. Na Allah ndio mmiliki wa mamlaka na humpa mamlaka amtakae na humpokonya asie mtaka

ﻋَﺴَﻰ ﺭَﺑُّﻜُﻢْ ﺃَﻥْ ﻳُﻬْﻠِﻚَ ﻋَﺪُﻭَّﻛُﻢْ ﻭَﻳَﺴْﺘَﺨْﻠِﻔَﻜُﻢْ ﻓِﻲ ﺍﻟْﺄَﺭْﺽِ ﻓَﻴَﻨْﻈُﺮَ ﻛَﻴْﻒَ ﺗَﻌْﻤَﻠُﻮﻥَ

“Na Mola atamwangamiza  adui yenu na kukufanyeni watawala katika nchi , na aone jinsi mtakavyofanya.”

[Al-A’raf: 129]

 

H 24 Ramadhan 1439

M: jumamosi 09 June 2018

Hizb-ut-Tahrir

Wilayah Syria

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.