Khilafah ndio mkombozi wa Wanawake- No.1

0

Kwa Munasaba wa tarehe 8/Machi ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake tunaweka mtiririko wa mada kuhusu wanawake na mtazamo wa Uislamu na Suluhisho lake.

Utangulizi

Kwa kipindi kirefu dini ya Uislamu imekuwa inaandamwa na vyombo vya habari vya kiulimwengu kuwa ni dini ambayo inakandamiza wanawake. Pia semina na makongamano mbalimbali yameitishwa kuchangia juu ya namna ambavyo Uislamu unavyomkandamiza mwanamke. Wao hudai Uislamu humnyima uhuru mwanamke kuendelea katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, uchumi na kadhalika. Huleta dai la kuwa mwanamke  wa Kiislamu ndiye mwanamke aliyenyuma kuliko wanawake ndani ya ulimwengu huu na huonekana kama kiumbe ambaye hajachangia katika maendeleo ya ulimwengu huu.

Wanafikra wa kadhia hii hudai kuwa idadi kubwa ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika hutoka kwenye jamii ama familia za Kiislamu. Biladi za Kiislamu nazo hushutumiwa kuwa ndio zinazoongoza kwa uvunjifu wa haki za binadamu.Uvunjifu huu hautokani na maelezo ya kutosha kama ndani ya hizo biladi kwanza zinatawaliwa Kiislamu. Tuhuma zote hizi hutolewa kuupaka matope Uislamu na ili watu waogope Uislamu na ili wajitolee kuunga mkono harakati za kupiga vita Uislamu.

Waislamu nao baada ya kupandikiziwa ufahamu na fikra za kigeni hususan baada ya ukoloni wengi walivurugwa kifikra na hatimaye kujikuta wamebeba fikra na mila za kigeni ambazo zinakinzana na Uislamu wao.

Mwanamke wa kimagharibi kifikra na kimila ni tofauti na mwanamke wa Kiislamu na hili linatokana na tofauti ya fikra/hadhara  baina ya Umagharibi na Uislamu.

Vugu vugu la  Kupigania Haki za Wanawake

Chimbuko la harakati za kupigania haki za wanawake lilianza mara  baada ya Zama za “mwamko” huko Ulaya. Alikuwa mwanamama Mary Wollstonecroft ambaye aliathiriwa na kuzunguukwa na mufakiruuna/wanafikra wa kiliberali ambao walitoa masuluhisho ya ‘mwamko’ kwenye masuala ya wanawake katika chapisho la vindication of the rights of women ndani ya mwaka 1792. Alifuata pia chapisho la “the rights of man” kutoka kwa rafiki yake wa karibu Thomas Paine ambaye alipinga haki “takatifu ya wafalme’. Baada ya kupitia mapinduzi ya kifaransa, muswada mwingine uligusa haki za wanawake ulitokea kwenye kitabu cha The subjugation of women cha John Stuart Mill. Kiligusia fikra za kisiasa juu ya haki za wanawake na wanaume kuwa sawa. Na wanawake walidai pia kuwa haki ya mwanaume kuwa juu halikuletwa na maumbile ya kibaiolojia bali ililetwa na mazoea

Simone de Beauvoir mmoja miongoni mwa sauti kubwa baada ya Wollstone Croft ambaye amegusia suala la ukombozi  wa wanawake kwenye kitabu chake cha The second sex”. Usawa kwa haraka humaanisha usawa kisiasa, kichumi, haki za kijamii  na fursa kama vile kwenye elimu, ajira na uwakilishi wa kisiasa. Mgawanyo kati ya mwanamke kama mama wa nyumbani na mwanaume msaka tonge ni mbinu ya ukandamizaji na ni matokeo ya ukandamizajwaji baada ya Mapinduzi ya Viwanda.

Mapinduzi ya viwanda hayakuwaokoa wanawake kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa kihistoria ila iliendeleza kifungo chao. Utajiri mkubwa uliotengenezwa katika kipindi cha mapinduzi ya  viwanda ulitengeneza idadi kubwa ya wanaume wa daraja la kati ambao hawakuthamini wanawake. Wanawake walianza kulalamikia juu ya huduma wanazopewa wanaume ambao walijitetea tabia ya ulevi na tabia chafu zinginezo zilitokana na shinikizo la kuongezeka kwa mashindano katika biashara na viwanda na hawakuonyesha mkazo wowote kwenye mambo ya nyumbani zaidi ya kudai mahitaji yao yafikiwe. Hakika ilikuwa hali hii katika Ulaya ya viwanda ambayo ilizalisha jamii ambayo ilitawaliwa na wanaume ambapo huu usawa ulikuwa jambo zito. Haraka mjadala wa usawa ulizalisha taswira ambapo Ulaya ungeshughulika na ukandamizwaji wa wanawake Na kusahisha makosa ya kihistoria. Kwa hiyo kusahihisha makosa ya kihistoria ukawa ndio msingi wa kutolea maana ya mahusiano kati ya watu.

Kwa hiyo tunaona chimbuko la harakati hizi hazikuanzia kwenye ulimwengu wa Kiislamu kwani kipindi hicho cha mwanzo wa harakati hizi Waislamu walikuwa wana serikali yao na kiongozi wao Khalifa. Na kwa hiyo ukandamizwaji wa wanawake hauna mahusiano na Uislamu.

Ulaya ndio ina historia ndefu ya ukandamizwaji wa haki za wanawake na utumikishwaji wa wanawake bila ya kujali thamani yao kama wanadamu. Hilo linapatikana kwa kuwa watu wa Ulaya kwa kipindi kirefu wamekuwa chini ya imani ya kikristo ambayo ni batili na inashindwa kutatua matatizo ya wanadamu kwa ujumla. Thiolojia ya kikristo ambayo ndio nguzo ya falme za kale za Ulaya ilifanya kazi kubwa katika kujenga mtazamo finyu juu ya wanawake kwa magharibi. Kanuni ya “Decretum gratiani iliweka msingi wa sheria ya kanisa kwa takribani miaka 800 kati ya mwaka 1140 mpaka 1917, uligawanya majukumu kwenye msingi wa dhana ya “dhambi ilikuja duniani kupitia wanawake” na “kwa sababu ya dhambi ya asili ya wanawake basi ni wajibu wajisalimishe kwa wanaume”. Ukiachana na hayo “Hawa” aliumbwa kutokana na mbavu za “adamu” Mitazamo hiyo iliathiri mwenendo wao hata baada ya mageuzi, kazi za wanathiolojia zililenga kwamba wanawake wana nafasi ya kutenda maovu.

Papa Innocent  wa 8 katika kitabu cha “ The hammer of the witch” cha mwaka 1484 amesisitiza:  “kipi kingine kwa mwanamke kama sio adui katika urafiki, adhabu isiyoepukika, dhambi muhimu, matamanio ya asili, janga la kupendeza, hatari ya nyumbani, muovu wa asili, aliyepakwa  rangi nzuri”(malleus maleficarun 1971) . Fikra hizi zilisababisha matokeo ya kuchoma moto  maelfu ya wanawake. Hata wanafikrana wa kipindi cha “mwangaza” walizungumzia mada hii kwa mtindo wa kufuata mila za asili. Rousseau ndani ya chapisho la “Emile” kilichohusu masuala ya elimu aliandika:

  “Wake kwa wanaume wameumbwa kwa kutegemeana, lakini kutegemeana kwao hakuko sawa. Tunaweza kustahimili bila yao, kuliko wao kustahimili kuishi bila ya sisi. Wao hutegemea hisia zetu, juu ya bei tunavyoweka kwenye umuhimu wao, juu ya thamani ya uzuri wao na matendo yao. Kwa hiyo elimu ya wanawake inatakiwa ipangwe kwa mahusiano na wanaume ili kuwaridhisha wanaume, kwa umuhimu kwao na kulipata penzi na heshima yao…………..”

Itaendelea……….

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.