Hizb ut Tahrir / Tanzania Yatuma Ujumbe Ubalozi wa Pakistani jijini Dar es Salaam
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutokana na kitendo cha fedheha cha serikali ya Pakistani kuwanyakuwa na kuwatia nguvuni wakina mama wa Kiislamu : ukhty Romana na ukthy Roshana na mume wake, kwa sababu tu, wamejifunga na ulinganizi wa Uislamu kupitia Hizb ut Tahrir, Hizb ut Tahrir Tanzania mnamo 20 Agosti 2018 ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistani nchini Tanzania kuukabidhi nakala mbili za taarifa kuhusiana na qadhia hiyo.
Ujumbe huo wa Hizb ut Tahrir / Tanzania ulimuhusisha Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania na Kaema Juma, Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Tanzania.
Afisa mkuu wa ubalozi alizipokea nakala za taarifa hizo, na kuzisoma kwa kiasi fulani mara baada ya kuzipokea, na kuahidi kuzifikisha kwa serikali yake ya Pakistan.
Tunamuomba Allah (swt) katika masiku haya matukufu kuwafariji na madhila na kuwalipizia kisasi ukhty Romana , ukhty Roshan, mume wake na Waislamu wote wanaodhulumiwa Mashariki na Magharibi
Wakati umewadia kwa madhalimu ukiwemo utawala wa Pakistan kutafakari kwa kina na kuwa wasikivu kutokana na indhari nzito kutoka katika Quran Tukufu:
وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ * مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ
“ Wala usidhani Allah (sw) ameghafilika na wanayotenda madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka yatakapokodoka macho* Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na noyo zao tupu.” [Ibrahim: 42-43]
Masoud Msellem
Media Representative of Hizb
Maoni hayajaruhusiwa.