Athari Za Dola Ya Khilafah Kwa Ulimwengu

Tukiwa ukingoni mwa mwezi wa Rajabu, mwezi ulioangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah, ni muhimu pia kugusia athari zilizoachwa na dola hiyo kwa wanadamu , bara la Ulaya na ulimwenguni kwa jumla.

Uimara wa Dola ya Khilafah Uthmaniya kwa zaidi ya miaka 600 bila kuyumba wala kuingiliwa hauwezi kufananishwa na utawala wowote katika historia. Hata wanafikra, waandishi na wanahabari wengi duniani wamekiri mafanikio hayo.

Khalifah mashuhuri Muhamamd aI-Fatih alisukumwa kuifungua Istanbul kutokana na Hadith mashuhuri ya Mtume SAAW aliposema kuwa jiji la Istanbul (Constantinople) litafunguliwa, na jeshi bora na Amir bora ndio wataofanikisha hili.

Hii ina maana Makhalifah walikuwa na malengo makubwa endelevu ikiwemo kuifungua Istanbul na kisha kuiangusha Dola ya Roma, na hatimaye walifanikiwa. Hii inaonesha wazi kwamba makhalifah walikuwa wanafanyia kazi Aqida ya Kiislamu

Mwanahistoria mashuhuri Albert Hourani anathibitisha kwamba “jukumu kuu la mtawala wa Dola ya Kiislamu kwa kipindi chote ..liilikuwa ni kuhifadh sheria za Kiislamu. Kuliandaliwa maqadhi ambao waliajiriwa na kulipwa na serikali wakifanya kazi ya kusimamia hukmu za Kiislamu katika kuyachunga matendo ya raia na Dola.

Aidha, Khalifah wa pili wa Dola hii aliyeitwa Orhan Uthman aliyetabani madhhab ya Hanaf kuwa ndiyo maalum kufuatwa na dola, mnamo mwaka 1324 alipitisha sheria ya kugawa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa misikiti. Hili likafanywa katika kila ardhi mpya iliyofunguliwa. Ilikuwa jukumu la serikali kusimamia ibada, hivyo ndiyo ilijenga misikiti kama ilivyoshuhudiwa katika miji ya Ulaya Mashariki. Misikiti ilitumika kuwa nyumba za ibada za swala, bali pia ilikuwa vituo vya kueneza elimu na afisi.

Pia Khalifa Murad III alimsaidia Malkia Elizabeth I (Mkristo), alipovamiwa na Dola ya Roma akidhaniwa kulisaidia kwa siri jeshi la Hispania la Waislamu.
Khalifah aliandaa jeshi la askari 10,000 kutoa msaada lakini Malkia aliomba apewe askari 1000 wa kuongezea jeshi lake.

Hata hivyo, Khalifah aliongeza kupeleka kwa siri meli tatu zilizosheheni chakula na kuweka nanga pwani ya eneo la mapambano.

Ukarimu huu wa Khilafah uliendelea kwani mwaka 1845 lilipozuka baala la njaa kubwa lililosababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja ndani ya Ireland, Khalifah Abdul Majid I alitoa msaada paundi fedha na meli tatu za shehena ya chakula zilizotia nanga katika bandari ya Drogheda, nchini Ireland. http://archiveislam.com/how-muslims-helped-ireland-during-t

Khilafah ilitoa msaada huu katika wakati ambapo ilishaanza kudhoofika kisiasa na kiuchumi. Baada ya ukarimu huu Khalifah alipokea barua ya pongezi na shukrani kutoka kwa watu wa Ireland kwa msaada huu mkubwa ambao umebakia katika nyaraka za kihistoria.

Jambo hili limeacha athari kubwa iliyowashinda dola za magharibi, kwani ukarimu wa Dola ya Khilafah kwa watu wenye shida ulijengwa juu ya kujali msingi wa utu.

Mafanikio haya ya Khilafah bila ya shaka ni kutokamana na kushikamana na Uislamu. Haikutenda ila kwa mujibu wa maelekezo na mipaka iliyowekwa na sheria za Kiislamu. Ni ubora wa Aqidah (aidiolojia) ya Kiislamu ambayo ilitekelezwa na tawala za Khilafah iliyoleta athari zote hizi.

Leo Khilafah inahitajika kurejeshwa tena, ili kuifanya dunia mahali salama, pa uadilifu na utu kwa wanadamu wote. Ni wajibu kwa Waislamu kulifanyia kazi hili. Pia ni muhimu kwa wasiokuwa Waislamu kuutafiti Uislamu na nidhamu zake zote ikiwemo nidhamu ya utawala ili wajionee wenyewe uadilifu wake kwa macho yao.

Risala ya Wiki No. 35
28 Rajab 1440 Hijri / 04 Aprili 2019 Miladi

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania
https://hizb.or.tz/
https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania
#RajabuFarajaKwaWalimwengu

Maoni hayajaruhusiwa.