Mtazamo Mpana Kuhusu Suala La Mohamed Ali Kibao

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:
Suala la Mohamed Ali Kibao (69), aliyetekwa nyara Septemba 6, 2024, na kukutwa amekufa asubuhi ya Septemba 7, 2024 eneo la Ununio, Dar es Salaam, Tanzania linahitaji kuangaziwa kwa uadilifu ili kutoa mtazamo sahihi wa kimfumo.
Maoni:
Kutekwa nyara na baadaye kuuawa kwa ndugu Kibao kumefichua zaidi ukweli wa mfumo wa kibepari katika suala la kutojali ustawi wa watu hasa katika muktadha huu suala la usalama.
Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) iliyotolewa tarehe 09 Agosti, 2024, zaidi ya watu 20 wameshatekwa nyara au kutoweka mwaka huu 2024 pekee, lakini Mkuu wa Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi mnamo tarehe 12 Septemba, 2024 alitoa taarifa kwa Umma kwamba hali ya usalama nchini ni imara na tulivu.
Huu ndio uhalisia wa ubepari ambapo maisha au kitu kingine chochote wana kijali pale tu penye maslahi, kwa kuwa kila kitu katika ubepari na demokrasia yake kinazunguka juu ya mtazamo huo.
Suala la uwepo wa sura mbili amma unafiki linajitokeza waziwazi katika suala hili. Wanaharakati wa Haki za binadamu, baadhi ya wapinzani pamoja na baadhi ya viongozi wa makanisa wamepaza sauti zao juu na kupinga mauaji hayo ya kikatili ya Kibao, kitu ambacho ni kizuri, lakini uwepo wa ubaguzi wao unaonekana waziwazi katika kukabiliana na masuala yenye sura kama hii.
Utekaji nyara na mauaji ya watu wasio na hatia si jambo geni nchini Tanzania. Hata hivyo, ikitokea wahanga wakubwa ni Waislamu kwa sababu ya Uislamu wao, wanaharakati, upinzani na viongozi wa makanisa huficha vichwa vyao katika ulimwengu wa kupuuzia au kutoa kauli za kijanjajanja nyepesi bila ya uzito wowote. Mathalan, kuna zaidi ya wahanga Waislamu 380 ambao hawajulikani walipo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani kufuatia oparesheni za serikali zilioambatana na mateso na mauaji ya kiholela mwaka 2017 (The East African, May 05, 2018) na oparesheni hizo kupelekea wengi wasio na hatia kuuawa,kuteswa na kutoweka. Hatujawahi kuona hatua zozote thabiti kutoka kwa wanaharakati wa Haki za binadamu, upinzani au makanisa.
Ikumbukwe pia wakati wa utawala uliopita wa Rais John Magufuli, ambapo watu wengi wakiuawa, kuteswa, kufungwa jela na kuwekwa kizuizini kwa kesi za kubambikiziwa, viongozi wa makanisa sio tu waliziba vinywa vyao kwa uimara mkubwa, bali walikuwa waungaji mkono wakubwa wa utawala wa Magufuli kiasi kwamba Kadinali Polycarp Pengo, alikuwa akishangaa kwanini watu walimuita Rais (Magufuli) kuwa ni dikteta (Mwananchi 18/11/2019).
Kuhusiana na mwito wa wapinzani na wengine wa kutaka uchunguzi huru na wa kina kufuatia kutekwa nyara kwa Kibao na mauaji yake ya kikatili, hapa kuna mambo mawili makubwa ya hatari yanayopaswa kuangaziwa:
a.Kukuzwa zaidi kwa ukoloni mamboleo kupitia uchunguzi wa kigeni kutoka kwa mataifa ya kikoloni na kibepari au taasisi zao. Ni ukweli usiopingika kwamba taasisi za ndani haziwezi kutegemewa katika kufanya uchunguzi huo kwa audilifi na uhuru, Inabidi iwe wazi kuwa mataifa ya kibepari na taasisi zao wamekosa mamlaka na uadilifu wa kimaadili kufanya uchunguzi huo. Suala la mauaji ya kimbari yanayoendelea ndani ya Gaza limewafedhehi zaidi kuwa hawako huru.
Mataifa ya kibepari yana ajenda zao za kinyonyaji katika mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania, na katika hali zozote yanaunga mkono tawala bila kujali hatua matendo ya tawala hizo ilmradi tu tawala hizo zitahakikisha maslahi yao (mabepari). Basi je unawezaje kutegemea nchi au taasisi kama hizo kufanya uchunguzi wa kina, wenye uadilifu na huru?
b.Kudai uchunguzi juu ya suala hili pekee na kupuuza mamia kama si maelfu ya wahanga ambao walikabiliwa na matukio kama haya kufuatia oparesheni za serikali huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani inamaanisha kuwa maisha yao hayana thamani, na hapa suala la ubaguzi linajidhihirika tena kwa mara ya pili.
Tunachokishuhudia katika vurugu na ukosefu wa utulivu ndani na nje ni matokeo ya mataifa ya kikoloni ya kibepari, na kutegemea kutoa masuluhisho kutokana na mtazamo huo huo wa kibepari au kutegemea mataifa hayo hayo na taasisi zao kuleta utatuzi ni hadaa ya wazi wazi kwa Umma na kuendeleza tatizo badala ya kulitatua.
Ni wakati muwafaka sasa kwa wanafikra miongoni mwa wapinzani na wengineo kutafakari kwa kina kwamba ulimwengu unahitaji mabadiliko ya kimsingi ya kimfumo, ili kung’oa kabisa mfumo wa kibepari na badala yake kuweka mfumo wa Kiislamu ili uhudumie jamii na kulinda ubinadamu kwa haki na uadilifu.
Imeandikwa na Said Bitomwa
Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.