Ubepari Ndio Unaohamasisha Ushoga

بسم الله الرحمن الرحيم

Ummah wa Kiislamu ulimwenguni kote na wapenda maadili katika wanadamu wana wasiwasi na wanapaza sauti zao juu ya kushamiri na kupigiwa kampeni vitendo viovu vya ushoga, amma kwa upana wake kinachoitwa mahusiano ya jinsia moja.
Nchi za magharibi ambazo zimeshatopea katika uovu huu zinapiga kampeni ya nguvu kwa nchi changa ili jambo hili liruhusiwe au walau raia wasipaze sauti zao dhidi yake. Wanafanya hayo wakijua kwamba uovu huo sio tu uko kinyume na dini bali hata na mila na desturi za watu ikiwemo mila za kiafrika.
Kwa upana wake tatizo la uovu wa ushoga limeenea takriban duniani kote likianzia katika nchi kubwa duniani, kwa mujibu wa mtandao wa stastica.com. mwezi Novemba mwaka uliopita, nchini Marekani kuliripotiwa asilimia 5.6 ya watu wazima waliojitambulisha wao wenyewe kuwa ni mashoga, wasagaji, na waliobadilisha jinsia pamoja na wanaojiita wapenzi wa jinsia moja yaani (LGBTQ).
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea kukithiri na kuchochea kwa tatizo hili kila kukicha, na miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:-
A. Uhuru wa Kibinafsi: Miongoni mwa fikra hatari zinazoenezwa na mfumo wa kibepari ni kuwa mwanadamu yuko huru, anaweza kufanya atakalo kwa njia anayoitaka, hivyo suala la ushoga , usagaji na mengine ni katika haki msingi za mtu yoyote kwa mujibu wa wamagharibi.
B. Lengo la Maisha: Kwa mujibu wa mfumo wa kimagharibi wa kibepari lengo kuu la mtu maishani ni kufikia katika kiwango cha juu cha starehe, hata kama starehe hiyo itaharibu jamii nk. ambapo kupitia mtazamo huu mwanadamu anahamasishwa kufanya kila aina ya starehe bila ya kuzingatia dini, maadili au utu.
C. Kupunguza idadi ya watu: Kuendelea kushamiri kwa kampeni za ushoga kunachangiwa pakubwa na kampeni ya kupunguza idadi ya watu duniani, ambapo mashoga wakiwa wengi watakuwa hawana uwezo wa kuoa na kuongeza kizazi kilichopo. Na hii imetokana na falsafa ya kiuchumi ya kimagharibi inayoamini kuwa rasilimali ni kidogo na watu ni wengi, hivyo lazima watu wapunguzwe ili wachache watakaobakia wafaidi rasilimali. Jambo ambalo ni kinyume na uhalisia.
D. Mitala ya elimu na vyombo vya habari : miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa janga hili ni ushawishi mkubwa unaotolewa kupitia mitaala ya elimu na vyombo vya habari ambavyo huhamasisha vitendo hivyo viovu kupitia majukwaa mbali mbali ikiwemo michezo, sanaa nk huku wakionesha jamii kuwa matendo hayo ya kibaradhuli ni katika haki msingi ya binaadamu na si tatizo kwa jamii.
Pamoja na hayo, Uislamu kama mfumo mbadala wa mfumo wa kidemokrasia/ kibepari kutoka kwa Muumba wa binaadamu na vilivyomo, daima hukinga, hutibu na hutatua matatizo ya jamii likiwemo suala la ushoga. Hivyo , katika kukabiliana na janga hili umeweka misingi ifuatayo:-
1. Ufafanuzi wa Lengo la Maisha: Uislamu umemtatulia mwanadamu ttizo lake kubwa nalo ni kumfafanulia kwa kina kuwa yeye ni kiumbe na malengo yake maishani ni kupata radhi za Allah SWT, jambo hilo pekee ndilo litakalomjaza moyo wake utulivu. Aidha, Uislamu ukamtaka mwanadamu huyo vitendo vyake avipeleke kwa mujibu wa maamrisho na makatazo ya Mola Muumba.
2. Nidhamu fafanuzi ya Kijamii: Uislamu unatambua kuwa kila mwanadamu ana hisia ya kuendeleza kizazi, hivyo, ukampangia njia maalum ya kuliendea hilo, nayo ni kupitia msingi wa ndoa ambayo hujenga jamii imara na yenye ustaarabu.
3. Hakuna Uhaba wa Rasilimali: Kwa mujibu wa Uislamu, rasilimali zilizopo zinawatosha wanadamu, hivyo hakuna haja kuwazuia watu kuongezeka iwe kupitia kampeni ya ushoga au kampeni nyingine. Bali Uislamu unaamini tatizo msingi ni kukosekana namna bora ya kusimamia rasilimali hizo na kuzigawanya kwa Umma. Chini ya utawala wa Kiislamu, Khalifah Umar bin Abdul-aziz alikuwa mfano tosha wa makhalifa wa Kiislamu waliotokomeza umasikini kwa kipindi chake na hakuna raia aliyebaki na njaa.
4. Kuzibwa Mianya ya Ushoga: Chini ya usimamizi wa serikali ya Kiislamu (Khilafah) vishawishi vyote vinavyopelekea watu kuwa mashoga vitazuiwa, vikiwemo kudhibiti vyombo vya habari, mitaala ya elimu, majarida nk. na kuithakafisha/ kuifinyanga jamii kwa mtazamo safi wa Kiislamu ambao unalenga kuilinda jamii kuepukana na kila aina ya balaa ikiwemo ushoga. Aidha, Uislamu ukaweka adhabu kali kukabiliana na matendo ya ushoga. Kwa mfano, Uislamu ukaweka hukmu ya Kiislamu ya ‘taazir’ ((kuanzia kuchapwa hadi kuuliwa) kwa vitendo vya kishogashoga kama mavazi, sauti au muonekano wa kimakusudi. Amma, ikidhihiri kwa ushahidi juu ya kutenda moja kwa moja matendo ya ‘liwaati’ hukmu yake ni kuuliwa kwa mfanyaji na mfanywaji.
Janga la ushoga, usagaji, kubadilisha jinsia na mfano wake kamwe hayawezi kuondoka chini ya mfumo wa kibepari, kwa kuwa ndio unaoyahamasisha. Bali yataondoka chini ya utawala wa Kiislamu wa Khilafah ambao hauna budi kuanzia katika ulimwengu wa Kiislamu na kusambaa kila mahali ili kuunusuru ubinadamu na majanga kama hayo na mengineyo mengi yaliyoletwa na mfumo wa kibepari/ kidemokrasia.
Mwisho, tunatoa mwito kwanza kwa Umma wa Kiislamu kusimama kidete katika kuukosoa na kuukataa mfumo wa kibepari/ kidemokrasia na fikra zake chafu za kimagharibi na kushika nguzo muhimu ya Uislamu kwa kuulingania na kufanya kazi ya kurejesha tena dola ya kilimwengu ya Khilafah. Aidha, kwa wasiokuwa Waislamu, uwepo wa matendo ya ushoga yanayopigiwa debe na mfumo wa kibepari ni dalili ya kutofaa mfumo huo kumsimamia mwanadamu. Basi hali hiyo iwe changamoto kwao kutafiti mfumo mbadala wa Kiislamu unaowafikiana na maumbile, kisha kusilimu. Na lau hawako tayari kusilimu walau wautizame Uislamu kwa uadilifu kuwa mfumo rafiki ulioletwa kuwa Rehma kwa wanadamu wote.
Risala ya Wiki No. 153
14 Shaaban 1444 Hijri / 06 Machi 2023 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.