Muislamu Anayedaiwa Kuwa ‘Gaidi’ Hastahili Kuachiliwa na Mahakama chini ya Tawala za Kisekula!

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Mnamo Jumatano, 7 Oktoba 2020 Hakimu Mkuu mjini Nairobi Francis Andayi alihukumu kuwa Liban

Abdillahi Omar hana makosa katika tukio la kigaidi la Westgate. Mnamo Alhamisi, 8 Oktoba 2020 dakika chache baada ya kutoka makao makuu ya Kitengo cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) kilichoko Upper Hill, Abdillahi Omar ‘alitekwa nyara’ na wanaume waliokuwa wamebeba bunduki. Tukio hilo lilitokea ilhali Omar alikuwa pamoja na dada zake ndani ya gari la teksi.

Maoni:

Tukio hili jipya la ‘utekaji nyara’ linatokea baada ya lile la mwisho lililotokea mnamo 16 Agosti 2020 ambapo Sheikh Khalid Swaleh, Ustadh Juma Shamte na Hassan wote kutoka Markaz Noor iliyoko Mtondia, Kaunti ya Kilifi. Watekaji nyara walidaiwa kuwa ni maafisa kutoka Kitengo cha Kupambana na Ugaidi (ATPU) ambao walivamia majengo hayo mwendo wa saa 7 usiku (Daily Nation, 16/08/2020). Kabla ya tukio la 16 Agosti kulitokea shambulizi za kidhalimu mnamo Jumamosi, 30/05/2020 eneo la Kibundani Kaunti ya Kwale, ambapo Waislamu waliamkia taarifa za kuuliwa kwa Muislamu mwanamume, Mohamed Rahma Mapenzi (miaka 41), watoto wake wawili, Swalia Rahma (miaka 6) na Idd Rahma (miaka 3).  Kwa kuongezea wanachama wa familia ya marehemu walijeruhiwa vibaya mno huku mkewe aliyekuwa na mimba ya miezi minane, Mwanahalima Mwachili alipoteza mimba yake wakati alipokuwa amepelekwa Hospitali ya Msambweni akiwa hali mbaya. (The Standard, 31/05/2020).

Tukio hili jipya ni thibitisho kuwa Kenya ni dola ya kimafia ya kisekula ya kidemokrasia ambayo inadai kuwa inaheshimu hukumu za kisheria ilhali kiuhalisia inakwenda mbio kukandamiza uhuru wa mahakama. Kile kinachoitwa utekaji nyara ni njama tu ya asasi za kiusalama za serikali kuzitia hofu akili na mioyo ya Waislamu. Zaidi ya hayo ni kutuma ishara kwa maafisa wa mahakama kwamba kinachotakiwa kutoka kwao kwa mujibu wa kesi zinazohusiana na ‘magaidi na wenye misimamo mikali’ ni kufungwa na kwamba kuachiliwa hakutakikani katika mchakato mzima!

Kenya imezama ndani mno katika kuwatoa kafara raia wake kwa jina la kupigania vita vinavyosukumwa na Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali. Sheria na sera za Kenya zinaathiriwa na mabwana zake Wamagharibi wakiongozwa na Uingereza na washirika wake. Na ndio sababu walivamia Somalia ili kwenda kulinda maslahi ya bwana wake kwa jina la kupiga vita Alshabab, kundi ambalo vibaraka wa Wamagharibi wamepenya ndani yake na kuliongoza.

Na ndio maana lilikuwa sio jambo la kushangaza kwa rais wa Kenya kuzuru Ufaransa kwa ziara ya siku tatu kuanzia 30 Septemba 2020 na kisha wakati anarudi nchini akaizuru Misri.  Nchi mbili hizo zinajulikana kwa sera zao ovu dhidi ya Uislamu na Waislamu ambapo rais wa Misri anajulikana kwa kuwa dhalimu kiasi kwamba ameivunja misikiti na kupiga marufuku maandishi ya Kiislamu kwa kisingizio cha kupigia debe misimamo mikali! Kwa upande mwingine rais wa Ufaransa ana andaa uzinduzi wa sera mnamo Disemba 2020 zinazolenga kupambana na ule unaoitwa ‘Uislamu wa siasa kali’ ambao hauendani na sheria za kisekula za Jamhuri ya Ufaransa.

Ni wajibu kwa Waislamu nchini Kenya na duniani kote kufahamu uhalisia unaouzunguka Uislamu na Waislamu leo. Uhalisia ni kuwa yeyote anayebeba itikadi ya hakuna kinachostahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Nabii Wake; na kisha akajikaza kuishi kwa mujibu wa itikadi hiyo; anazingatiwa kuwa ni adui na tawala za kisekula kwa maana ni ‘gaidi au mwenye misimamo mikali’ anayestahili kupigwa vita ili kubeba itikadi ya kisekula ili kuwa ‘Muislamu wa kati na kati’ anayepima vitendo kwa msingi wa maslahi na manufaa (sheria za kisekula)!

Uislamu na Waislamu wataendelea kutaabika chini ya tawala hizi za kisekula za kirasilimali kwa zinahofia kurudi kwa Uislamu kama mfumo mbadala katika ulingo wa kiulimwengu. Ni muhimu kutambua kwamba njia pekee ya kujinasua na ukandamizaji na mateso haya ni kuunga juhudi na kufanyakazi na Hizb ut Tahrir, chama cha Kiislamu cha kisiasa. Chama ambacho kinaongoza katika kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ndio mlinzi na ngao ambayo italinda Uislamu, Waislamu na wanadamu kwa ujumla dhidi ya njama za maadui wa Uislamu na Waislamu. Ni chini ya Khilafah ambapo Waislamu watatawaliwa kwa mujibu wa Shari’ah ya Kiislamu na kuwapelekea kupata heshima na hadhi na kuhifadhi damu, mali na matukufu yao. Kwa kuongezea, wanadamu watafurahia ustawi, amani na utulivu wa kweli chini ya kiongozi muadilifu Khalifah. Mwenyezi Mungu (swt) asema: وَعۡدَ ٱللَّهِ‌ۖ لَا يُخۡلِفُ ٱللَّهُ وَعۡدَهُ ۥ وَلَـٰكِنَّ أَڪۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ* بِنَصۡرِ ٱللَّهِ‌ۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُ‌ۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ*وَيَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ “Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui. [Ar-Rum 30: 4 – 6].

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.