19 Ramadhan

بسم الله الرحمن الرحيم

Siku kama hii tarehe 19 Ramadhan 40 Hijria /Januari 26, 661, Khalifah wanne Imamu Ali bin Abi Talib (ra) wakati akiswali swala ya Alfajiri alipigwa dhoruba ya upanga na mshenzi Abd al-Rahman bin Muljam al-Muradi. Dhoruba hiyo ilisababisha kifo chake baada ya siku chache.

Imamu Ali (ra) alizaliwa miaka 23 kabla ya Hijra, alilelewa na Mtume SAAW na alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuukubali Uislamu.
Alifanya kazi kubwa ya kuutumikia Uislamu, alibeba majukumu mbali mbali ya kidola ikiwemo pia kushiriki katika vita mbalimbali. Aidha, alikuwa mshauri mkubwa kwa makhalifa wengine na alikuwa mwanachuoni wa daraja ya juu.
Hatimae Waislamu walimchagua kuwa Khalifah wa nne baada ya kuuwawa Uthman bin Affan.

Khilafah ya Ali bin Abi Talib ilikabiliwa na changamoto nzito za uasi mkubwa katika utawala wake kiasi cha kumlazimu kupigana vita kadhaa ili kurejesha utiifu na kuweka mambo sawa.

Imamu Ali aliuwawa mjini Kufa na kuzikwa mjini Najaf, Iraq.

19 Ramadhan 1441 Hijri – 12 Mei 2020 M

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.