10 Ramadhan 1441 H

بسم الله الرحمن الرحيم

Siku kama hii ilikuwa ya huzuni na majonzi kwa kufariki dunia Ummul Muuminina Khadija bint Khuwaylid, mke wa Mtume SAAW.

Kifo hiki kilileta msiba na huzuni kubwa kwa Mtume SAAW na Waislamu kwa jumla. Mwanamke huyu mtukufu alikuwa ndio Muislamu wa mwanzo, alikuwa kila kitu kwa Mtume SAAW, alitoa mali zake, muhanga wake na kila chake kwa ajili ya Mtume SAAW na Uislamu. Alifariki akiwa na umri wa miaka 65, miaka miwili kabla ya Hijra.

Kuhusu darja ya Bi Khadija ra. Mtume SAAW amesema:

“Alinikubali ilhali wengine wakinikadhabisha, aliniamini ilhali wengine wakinita muongo, alikuwa karibu nami ilhali wengine wakiniacha mkono, alinifariji ilhali wengine wakinikebehi, na Allah Taala akanitunuku nae watoto, ambao sikupata watoto hao kwa wake wengine “

10 Ramadhan 1441 Hijri – 03 Mei 2020 Miladi

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.