Matokeo ya Kisiasa Katika Mkoa wa Catalonia!

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali

Shirika la habari la BBC liliripoti afisi ya Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, leo (19/10/2017), ikisema: “Baraza la Mawaziri huenda likakutana kukifanyiakazi kifungu cha 155 cha katiba, kuliruhusu kuchukua mamlaka ya kuendesha eneo hili… Kiongozi wa serikali ya eneo la Catalonia, Carles Puigdemont, alikuwa ametuma barua kwa serikali ya Uhispania, akitishia kuwa bunge la eneo hilo litapitisha kura ya maamuzi juu ya uhuru wa kujitenga na Uhispania ikiwa Madrid itaweka kizuizi kwa mazungumzo na kuendelea na unyanyapaa wake.” Baada ya kura ya maamuzi ya mnamo 1/10/2017, Raisi wa eneo hilo alitangaza mnamo 10/10/2017 mbele ya bunge la eneo hilo kujitenga kutoka kwa Uhispania, lakini akafanya utekelezaji wa hili kuwa wazi kwa mazungumzo. Sasa, ni kwa nini eneo hili lilifanya kura hii ya maamuzi licha ya upinzani kutoka kwa dola ya Uhispania; mfalme wake, serikali yake na mahakama yake ya katiba?

Msimamo wa kimataifa ni upi juu ya hili? Na ni upi uwezekano wa kutekelezwa kwa uhuru wa Catalonia? Jazakum Allah Khairan.

Jibu

Ili taswira hii iwe wazi na kupata jibu sahihi zaidi la swali hili, tutaitathmini upya hali halisi ya Catalonia, harakati zake kabla ya kujitenga, na kisha yanayojiri baada ya kura ya maamuzi, tutataja msimamo wa kimataifa juu ya hili, na baadaye, tutadadisi uwezekano wa kutekelezwa kura hii ya maamuzi:

Kwanza: Historia na hali ya kijiografia ya Catalonia:

Eneo hili linapatikana Kaskazini Mashariki mwa Uhispania lenye ukubwa wa kilomita 32.1 mraba, ambayo ni asilimia 8 ya Uhispania, Barcelona ikiwa ndio mji mkuu wake. Eneo hili linajumuisha mikoa minne, kwa majina: Barcelona, Girona, Lleida na Tarragona, jumla ya idadi ya wakaazi ni milioni 7.5, inayo wasilisha asilimia 16 ya wenyeji wa Uhispania ambalo ni miongoni mwa maeneo kumi na saba yenye uhuru wa kujitawala wenyewe nchini humo.

Uislamu umeangaza Catalonia tangu mwaka wa 95 Hijria wakati wa kufunguliwa kwa Andalusia. Utawala wa Kiislamu ulipo malizika, eneo hili liliendelea kuwa eneo huru, baadaye Uhispania ukaliunganisha nayo kwa nguvu mnamo 1714 Miladi. Watu wa mkoa huu hawakukubali hili na walidumu kung’ang’ana kujikomboa kutokana na uvamizi huu wa Uhispania. Mnamo miaka ya 1930, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka baina ya serikali kuu ikishirikiana na serikali mshirika wake inayo jitawala wenyewe ya Catalonia upande mmoja, na jeshi la Franco upande wa pili. Baada ya ushindi wa jeshi la Franco, Franco aliwahangaisha wana Catalan, kuzuia lugha yao kuwa lugha rasmi ya eneo hilo, kupiga marufuku kusomeshwa lugha ya Catalan mashuleni, na kuwanyima wa-Catalan kitambulisho. Baada ya kuanguka kwa utawala dhalimu wa Franco, kura maarufu ya maamuzi ilifanywa huku asilimia 30 ya kura hizo zikipendelea katiba ya Uhispania inayo pendekeza umoja wa nchi na haki ya kujitawala wenyewe kwa makabila, jamii za walio wachache na mikoa ya Uhispania. Mnamo 1979, wenyeji wa Catalonia kwa mara nyengine tena walijipatia haki ya kujitawala wenyewe, na hii ndio iliyopelekea kutambuliwa kwa lugha ya Kihispania na Catalan kama lugha rasmi za eneo hili.

Baada ya hapo, harakati za kujitenga za Catalan zilipoa moto mpaka mwanzoni mwa karne hii ambapo zilianza kuibuka tena kidogo kidogo.

Pili: Hatua za Harakati za Sasa za Catalan:

  1. Harakati hizi zilianza mnamo 2006 kwa kupitishwa sheria mpya ya kujitawala wenyewe na ilipigiwa kura na watu kwa lengo la kupanua mamlaka ya kujitawala wenyewe ya eneo hilo. Sheria hii ililifafanua upya taifa la Catalonia. Mnamo 2010, Mahakama ya Katiba ya Uhispania iliifuta sheria hii jambo lililo pelekea maandamano chini ya mwito “Sisi ni taifa, tunajiamulia”. Mnamo Novemba 2012, kura ya maamuzi ya shangwe ilifanywa iliyopigia kura ya kujitenga na dola ya Uhispania. Mnamo Januari 2015, Waziri Mkuu wa Catalonia, Artur Mas, alitangaza kufanyika kwa uchaguzi wa ghafla wa aina ya kura ya maoni mnamo Septemba ya mwaka huo huo. Uchaguzi huu wa mapema ulifanywa na harakati ya kitaifa inayolingania kujitenga ikashinda viti vingi 72 kwa viti 63 ilivyoshinda vyama vinavyo pinga kujitenga. Walio wengi bungeni mnamo Novemba 2015 waliweza kuchapisha mswada unaotangaza mwanzo wa “Mchakato wa Catalonia kufikia hatua ya serikali huru”. Serikali ya Uhispania ilikata rufaa kwa mswada huo katika Mahakama ya Katiba ambayo iliikubali rufaa hiyo.
  2. Mnamo 9/6/2017, wakati ambapo hatua hizi zilipamba moto na kuchukua muelekeo imara, Raisi wa serikali ya Catalonia, Carles, alitangaza kwamba “kura ya maoni ya kujitenga kwa eneo hili kutoka kwa Uhispania itafanyika mnamo 1/10/2017 na kwamba serikali itauliza katika kura hii ya maoni swali lifuatalo: “Je, unataka Catalonia iwe dola huru kwa muundo wa jamhuri?” (Novosti, 9/6/2017). Siku iliyofuatia, serikali ya Uhispania ikatangaza kwamba itazuia jaribio lolote la kujitenga kwa Catalonia. Mnamo 6/9/2017, bunge la Catalonia likapitisha sheria inayoweka msingi wa kura ya maamuzi ya kujitenga kwa eneo hilo kutoka kwa dola ya Uhispania. Waziri Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy, akasema: “Serikali ya Uhispania huenda ikatumia nguvu za kikatiba kusitisha mamlaka ya kujitawala wenyewe ya Catalonia na hivyo basi kulizuia eneo hili kutokana na kujitenga kutoka kwa Uhispania”. Mahakama ya Katiba ya Uhispania ikajibu mnamo 8/9/2017 kusitisha kura hii ya maamuzi mpaka itakapo toa hukumu ya uhalali wake kikatiba.
  3. Licha ya hayo, kura hii ya maoni ikafanywa mnamo Oktoba 1, 2017 kama ilivyo pangwa. Matokeo yakawa kwamba asilimia 90 ya wapiga kura, ambayo ni asilimia 43 ya wakaazi wote, wakataka kujitenga kutoka kwa Uhispania na kuwa huru. Mfalme wa Uhispania, Philippe VI, akatoa hotuba mnamo Oktoba 3, 2017 baada ya kura hiyo ya maamuzi, huku akiita “isiyo halali na isiyo ya kidemokrasia”, lakini gavana wa eneo hilo akasema: ” Atatangaza rasmi uhuru huu mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo”. Akasema: “Mfalme amekataa jukumu la kuwa mpatanishi alilopewa na katiba ya Uhispania” (BBC 3/10/2017). Inaonyesha kuwa Uhispania imefedheheka. Haikuweza kuzuia mchakato wa kura ya maamuzi, kwa hivyo imechukua hatua za kuiwekea vikwazo iliyopelekea kujeruhiwa kwa watu 893 kutokana na ghasia kati ya majeshi ya usalama na wapiga kura. Hili limepelekea kuibuka kwa rai jumla dhidi yake, na ikawa basi inatafuta njia nyengine za kuzuia kutangazwa kwa uhuru. Kwa hivyo, ikaanza kutumia vita vya kiuchumi dhidi ya eneo hili; taasisi kuu za kifedha na makampuni yakatangaza kuondoka kwao Catalonia, na benki ya tatu kwa ukubwa nchini Uhispania, CaixaBank, mnamo 6/9/2017 ikatangaza uamuzi wake wa kuyaondoa makao yake makuu na kuyapeleka nje ya jiji la Barcelona, mji mkuu wa Catalonia. Mnamo 8/10/2017, maelfu ya wanaopinga kujitenga waliandamana barabarani nchini Uhispania kujenga msukumo wa upinzani ndani ya Catalonia.
  4. Raisi wa eneo la Catalonia, Carles, alitangaza mbele ya bunge mnamo 10 Oktoba 2017, uhuru wa mkoa wa Catalonia lakini akaakhirisha utabikishaji wake. Alisema: “Nachukua mamlaka ya watu kutangaza Catalonia kuwa dola huru katika muundo wa jamhuri, naliomba bunge kusitisha utabikishaji wa tangazo hili la uhuru kwa wiki chache kufungua mwanya wa mazungumzo”.

Lakini, hakufikia kiwango cha kuliunga mkono bunge kutangaza tangazo hilo la uhuru. (Euro News, Reuters 10/10/2017). Hii yamaanisha kwamba hakutaka kujifedhehesha kwa kutangaza kujitenga kwa sababu anajua kuwa kufikia hili sio rahisi. Kwa hivyo, aliuacha mlango wazi kwa ajili ya majadiliano na dola ya Uhispania kuepuka migongano. Eneo hili, bado limo ndani ya Uhispania, bali tatizo la eneo hili linasalia kuwa hai na lenye kulewa lewa shingoni mwa Uhispania na Muungano wa Ulaya mpaka dhurufu zitakapo ruhusu na uhuru kupatikana.

Tatu: Msimamo wa kimataifa juu ya matukio ya Catalonia.

Hapa, tutataja misimamo ya nchi zenye msemo, yaani, Muungano wa Ulaya na Amerika, pamoja na msimamo wa Umoja wa Mataifa ambao unaathiriwa pakubwa na msimamo wa Amerika:

  1. Msimamo wa Ulaya ulikuwa wazi dhidi ya kura hii ya maamuzi na uhuru wa Catalonia. Ujerumani, Ufaransa na Muungano wa Ulaya ziliunga mkono msimamo wa serikali ya Uhispania. Naibu wa Waziri wa Kigeni wa Ujerumani alisema kuwa: “mambo yanayo endelea eneo la Catalonia ni ya kutia wasiwasi na kujitenga sio suluhu. Kujitenga hakutatui matatizo yoyote. Wanachama wote wa Muungano wa Ulaya wanapaswa kuheshimu na kujifunga barabara na muongozo na kanuni za utiifu kwa sheria na demokrasia… mizozo ya kisiasa ndani ya Muungano wa Ulaya inapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo badala ya ghasia barabarani.” (Reuters, 2/10/2017). Ufaransa imetangaza msimamo wake kupitia Waziri wake wa masuala ya Ulaya, Nathalie Loiseau, kwamba “Ufaransa haitaitambua Catalonia ikiwa eneo hili la Uhispania litatangaza uhuru kipeke yake… Ili uhuru utambuliwe – na ambao sio jambo linalojadiliwa – natija itatayo jitokeza kwa haraka itakuwa ni (Catalonia) moja kwa moja itajiondoa katika Muungano wa Ulaya” (Reuters, 9/10/2017). Raisi wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, alitangaza msimamo wa muungano huo kuwa “unaotaka kuheshimu maamuzi ya serikali ya Uhispania na Mahakama yake ya Katiba”. Huku Raisi wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, akiandika katika mtandao wa Twitter mnamo 2/10/2017, akisema: “Kwa kushirikiana naye (Waziri Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy) kimaoni ya kikatiba, nimesihi kutafutwa kwa njia za kuepuka mzozo zaidi na utumiaji nguvu”.
  2. Ama kuhusu msimamo wa Amerika, unaonyesha kuwa serikali ya Catalonia na Raisi wake wameshajiishwa na kuungwa mkono na Amerika. Msemaji wa idara ya Amerika, Heather Nauert, alisema: “Amerika inachukulia kura hii ya maamuzi kama jambo la ndani la serikali ya Uhispania na hatunge taka kuingilia. Tutaiwacha serikali yenyewe na watu wake kutatua, na tutafanya kazi na serikali yoyote au utawala wowote utakao zaliwa kutokana nayo” (Gazeti la Misri la Al-Fajr, 16/9/2017). Sentensi hii ya mwisho inachukuliwa kuwa uidhinishaji wa Amerika wa kura hii ya maamuzi na uhuru. Kwa sababu inasema: “tutafanya kazi na serikali yoyote au utawala wowote utakao zaliwa nayo”; yaani, tutalitambua eneo la Catalonia endapo litapata uhuru. Gazeti la Uhispania la “El País” limesema kwamba “raisi wa eneo la Catalan, Carles Puigdemont, alizichukulia taarifa za msemaji wa Amerika kumaanisha kuwa Amerika ina heshimu matakwa ya watu wa Catalonia na matokeo ya kura ya maamuzi.” Kwani inajulikana kuwa Amerika inalenga kuvunja Muungano wa Ulaya kwa kutangaza kuunga mkono kwake Uingereza kujiondoa kutoka kwa muungano huo na kushajiisha hilo kwa nchi nyenginezo za Ulaya, au kwa uchache inataka kuukalia katika mambo yake ya ndani na katika harakati za kujitenga ili muungano huu na nchi zake kuu zisiweze kushindana na Amerika au kuiharibia katika kadhia za kimataifa. Kwa hivyo, kushajiisha harakati hizo za kujitenga ni kwa ajili ya maslahi yake. Na msimamo huu una kinzana na msimamo wake kuhusu kura ya maamuzi ya Kurdistan na uhuru wake ambayo inaipinga kwa nguvu na kuikataa na imezisukuma nchi zilizoko eneo hilo kuanzia Iraq mpaka Iran na Uturuki kupinga na kuikataa vile vile na kumshinikiza Barzani kwa sababu hili halina maslahi naye kwa sasa, hususan kwa kuwa (Amerika) ndiyo yenye athari kubwa nchini Iraq. Uingereza ndiyo iliyompa maagizo kibaraka wake Barzani kuchukua hatua hii ya kuivuruga Amerika ili kuleta takhfifu ya kuondolewa kwa vikwazo vya Amerika vinavyo tekelezwa na Saudi Arabia na Misri juu ya Qatar ambayo ni kibaraka wa Uingereza.
  3. Ama kuhusu msimamo wa Umoja wa Mataifa, unao tawaliwa na Amerika, msimamo wake kuhusiana na kadhia ya Catalonia ni kushajiisha kupatikana uhuru wake. Katibu Mkuu wake, Antonios Guterich, alizungumza “matarajio kwamba taasisi za kidemokrasia za Uhispania zitapata suluhu ya mgogoro kati ya wanaharakati wa Catalonia wanaotaka kujitenga na serikali ya kitaifa.” Msemaji wa raisi katika kikao cha 72 cha Kongamano Kuu la Umoja wa Mataifa alisisitiza kuwa “haki ya watu kutaka kujiamulia wenyewe ni haki msingi, huku akitaja haja ya kutekelezwa haki hii pasi na kukiuka msingi wa heshima wa eneo la nchi hii na kupitia itifaki baina ya pande husika” (Associated Press, 3/10/2017). Hili laashiria kwamba Umoja wa Mataifa unapigia debe uhuru wa Catalonia huku ukipinga kura ya maamuzi ya eneo la Kurdistan na uhuru wake kutokana na athari iliyo nayo Amerika katika maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Ni wazi kutokana na misimamo hii kuwa harakati za hivi karibuni za Catalonia katika kadhia ya kura ya maamuzi zimeshajiishwa na Amerika kwa sababu Amerika ana hamu ya kuyaharibu mazingira ya Ulaya, hususan katika enzi za Trump, na linalo ufanya mtazamo huu kuwa wenye nguvu zaidi ni misimamo na taarifa zilio tangulia kutajwa hapo juu.

Nne: uwezekano wa kutekelezwa kujitenga huku:

Hili si rahisi kutokea angaa kwa mustakbali wa hivi karibuni, na hakuna shaka kuwa Amerika inatambua hili, na ushajiishaji wake kwa harakati za Catalonia ni kwa lengo la kuharibu mazingira barani Ulaya na kulishughulisha nayo kama hatua za mwanzo za mpango wa muda mrefu wa kuuvunja Muungano wa Ulaya. Zaidi ya hayo, kuna sababu nyenginezo zinazo ifanya Uhispania kushindwa kukubali kujitenga kwa Catalonia kwa njia yoyote ile sababu mbili kuu zikiwa:

  1. Eneo hili, licha ya udogo wake, huzalisha asilimia 20% ya utajiri wa kitaifa (GNP) wa Uhispania, linadhibiti asilimia 70% ya uchukuzi na mawasiliano yanayo husiana na biashara ya kigeni ya Uhispania na kuzalisha thuluthi moja ya viwanda vya Uhispania, na ndiyo sababu wakaazi wa Catalonia huitakidi kuwa wanazalisha zaidi kuliko wanacho pokea. Na serikali ya Uhispania inawatoza ushuru mkubwa unaofikia kiwango cha asilimia 10% ya uzalishaji wa eneo zima; yote haya yanatilia mkazo vilio na ari ya kujitenga. Kwa upande mwengine, Uhispania inakumbwa na matatizo ya kiuchumi, bajeti dhaifu ya umma, upungufu mkubwa wa matumizi ya bajeti na ongezeko la kiwango cha ukosefu wa ajira, ikiongezewa na uchache wa suluhu. Uchumi wa Catalonia ni jambo muhimu katika kusuluhisha matatizo ya kiuchumi.
  2. Zaidi ya hayo, kujitenga kwa Catalonia kutapelekea kugawanyika zaidi kwa Uhispania na sehemu nyenginezo kwa sababu uhuru wa Catalonia utakuwa ni kichocheo cha nchi ya Basque ya Uhispania ambayo imewahi kutafuta uhuru awali. Nchi ya Basque imeunga mkono hatua ya Catalonia, ishara kuwa nchi ya Basque huenda ikalingania kujitenga kwa mara nyengine tena kwa kuwa ari ya wanaharakati ya kujitenga haija fifia bado. “Nchi ya Basque tayari imetangaza hamu ya kujitenga kutoka kwa eneo la Uhispania kuanzia mwaka ujao” (Siyasa Post 24/9/2017). Ni eneo lililo kumbwa na ghasia na vifo vya mamia ya watu ambapo harakati ya ETA imekuwa ikiongoza mchakato wa kisilaha wa kujitenga kwa miaka mingi mpaka makubaliano ya kusitisha mapigano yalipo fanyika miaka mitatu iliyopita na harakati hii kutupilia mbali silaha zake baada ya kupata mamlaka ya eneo hili. Kwa hivyo, kujitenga kokote kutakako tokea katika mkoa mojawapo kwa kiasi kikubwa kutafuatwa na mikoa mengine. Waziri wa Haki wa Uhispania ameonya juu ya hili na alinukuliwa akisema: “Nina wasiwasi mkubwa kuwa uhuru wa Catalonia utafikisha hatima dola ya Uhispania, kwa sababu uhuru wa Catalonia huenda ukaleta “athari ya kichocheo” katika eneo zima” (Al Jazeera, 2/10/2017).

Uhispania, hivyo basi, haiwezi kukubali kwa njia yoyote kugawanywa kwa eneo la Catalonia, bali, inatishia kukifanyiakazi kifungu cha 155 kuzuia haki ya kujitawala wenyewe kwa eneo hili ikiwa itashindwa kuzuia kujitenga kwa njia yoyote kama ilivyo fahamika kutoka kwa afisi ya Waziri Mkuu wa Uhispania, na kama ilivyo ripotiwa na shirika la habari la BBC mnamo 19 Oktoba 2017.

  1. Zaidi ya hayo, Muungano wa Ulaya unakaribia kuporomoka endapo fikra ya kujitenga itaenea maeneo yake, hususan ikiwa kujitenga huku (kwa Catalonia) kutapatikana. Hii ni kwa sababu zipo harakati za kujitenga nchini Ufaransa, ambapo eneo la Catalonia na nchi ya Basque zimegawanyika baina ya Ufaransa na Uhispania, na kunayo harakati ya kujitenga katika kisiwa cha Corsica kinacho taka kuwa huru na Ufaransa na kinasubiri tu mafanikio ya eneo la Catalonia kuchukua hatua.

Pia, kunazo harakati za kujitenga nchini Italia, Belgium na kwengineko, ambazo zinatishia mshikamano wa Muungano wa Ulaya unao kumbwa na migogoro mingi na tishio kutoka kwa harakati za kitaifa za kutaka kujiondoa kutoka kwa muungano huo kama ilivyo tokea kwa Uingereza almaarufu kama Brexit.

Yote haya yanafanya uwezekano wa kutabikishwa kujitenga huku kutokuwa na uhakika na kuwa vigumu sana, kwani ni tishio, sio tu kwa Uhispania pekee, bali kwa Muungano mzima wa Ulaya.

Inaonyesha kuwa raisi wa eneo hili ameanza kutambua hili kama alivyo jiona karibu ya kutengwa na mpaka eneo lenyewe, kwani alipingwa na halaiki ya watu. Kwa hivyo, uamuzi wa kutangaza uhuru hauku kamilika kwa kuwa raisi wa eneo hili aliakhirisha utabikishaji wake mpaka majadiliano ya kupata uhuru mkubwa zaidi wa eneo pamoja na kubuni fursa na kusubiri dhurufu muwafaka za kupata uhuru siku za usoni, ima hili liwe kwa ajili ya hadhi ya Uhispania au hadhi ya Muungano wa Ulaya. Hata Amerika iliyo ushajiisha imepunguza kasi ya kuunga mkono ilipo ona msimamo mkali wa Uhispania iliyo ungwa mkono na Muungano wa Ulaya. Hiyo ndio sababu ya Raisi Trump kusema wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uhispania, Rajoy, aliye kwenda Amerika kuvinjari rai yake juu ya uhuru wa Catalonia, “Tunaamiliana na nchi kubwa kweli kweli, na haina budi ibakie kuungana” (Gazeti la Misri la Ashorooq 27/9/2017).

Na Raisi wa eneo hili atatambua kuwa Trump ni kama shetani katika ahadi zake

(يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا)

Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet’ani hawaahidi ila udanganyifu.

[An-Nisaa: 120]

Hata hivyo, Amerika itaendelea kuuhujumu Muungano wa Ulaya, na itawatafuta wale watakaoitikia ahadi zake barani Ulaya!

Tano: Hivyo basi, utaifa humomonyoa wamiliki wa mfumo wa kirasilimali, hususan Ulaya, kuuzorotesha na kudhaifisha umoja wake, mshikamano na kazi yake ya kisiasa ng’ambo. Kwa sababu, mfumo wa kirasilimali haukuweza kushughulikia suala la utaifa, na wala hautaweza, ni mfumo ulio feli mbali na kuwa ni batili kutokana na msingi wake wa kutenganisha dini na maisha. Na ni fisidifu kwa sababu demokrasia yake inayo dhibitiwa na wamiliki wa rasilimali ambao hujinyakulia vyeo na fursa kupitia jina lake na kupitia matumizi mabaya ya sheria. Pia ni mfumo dhalimu kwa sababu hupiga vita dini na wale wanao shikamana nayo, na kuwepo ubaguzi baina ya watu kwa misingi ya dini au ukabila. Hili limejitokeza nchini Amerika na Ulaya na wala huu si ufahamu wa kimakosa wala kutia chumvi katika uoni.

Sheria zote zilizotungwa na mwanadamu haziku takata kutokana na dhulma hii, ugandamizaji na ufisadi wala kutokana na utumwa wa nchi na watu wake. Ni Uislamu pekee, ambao umeteremshwa na Allah, Mola wa walimwengu, unao simamisha haki na uadilifu miongoni mwa watu na kuweka sawa mambo yao,

 (أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ)

Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?

[Al-Mulk: 14]

Uislamu ndio ulio wayeyusha watu kuwa umma mmoja na kuondoa migawanyiko ya kitaifa na ya kikabila na uadui kama ulivyo haramisha hamasa za kitaifa na miundo yote ya Asabiyya na kuipiga vita vya kudumu.

Uislamu ndio unao simamisha uadilifu miongoni mwa watu katika uchungaji wa mambo yao bila ya ubaguzi wa kidini, kikabila, rangi, jinsia au jengine lolote, bali watu wote huchukuliwa kuwa sawa; huamiliwa kwa uadilifu mbele ya mahakama chini ya kivuli cha dola ya Khilafah Rashidah.

Imam Ahmad ameripoti katika Musnad yake: Ismail amepokea kutoka kwa Said al-Jurairi kutoka kwa Abi Nadra kutoka kwa wale waliomsikiza Mtume wa Allah (saw) katikati ya siku za at-Tashriq kwamba Mtume wa Allah (saw) amesema:

((يَا أَيُّهَا النَّاسُ، أَلَا إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ، وَإِنَّ أَبَاكُمْ وَاحِدٌ، أَلَا لَا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ عَلَى عَجَمِيٍّ، وَلَا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ، وَلَا أَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ، وَلَا أَسْوَدَ عَلَى أَحْمَرَ، إِلَّا بِالتَّقْوَى أَبَلَّغْتُ((، قَالُوا: بَلَّغَ رَسُولُ اللَّهِ))

“Enyi watu, Mola wenu ni mmoja, baba yenu ni mmoja. Hakuna fadhla kwa muarabu juu ya asiye kuwa muarabu wala asiye kuwa muarabu juu ya muarabu, wala kwa mwekundu juu ya mweusi wala kwa mweusi juu ya mwekundu isipokuwa kwa uchaji Mungu (Taqwa).  Je nimefikisha ujumbe?”

Wakasema, “Mtume wa Allah amefikisha ujumbe.”

Hii ndio haki:

 (فَماذا بَعْدَ الْحَقِّ إِلاَّ الضَّلالُ فَأَنَّى تُصْرَفُونَ)

“Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa?”

[Yunus: 32]

Inatoka Jarida la Uqab: 11 https://hizb.or.tz/2017/12/01/uqab-11/

Maoni hayajaruhusiwa.