Khotuba Ya Amır Wa Hızb Ut Tahrır Mwanachuonı Mashuhurı

بسم الله الرحمن الرحيم

Khotuba Ya Amır Wa Hızb Ut Tahrır Mwanachuonı Mashuhurı

Atta Ibn Khalıl Abu Rashtah Kuhusu Kumbukumbu ya  Fathı ya Mjı wa Constantınople  Mwaka 857 AH / 1453 AD

Sifa njema ni za Allah SW kwa neema Zake, na rehema na amani ziende kwa Mjumbe wa Allah SAAW na aali zake na masahaba wake na kila  anayemfuata yeye. Amma baada ya hayo:

Kwa Ummah wa Kiislamu, Ummah bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu… Na kwa wabeba da’awa wabora na wema… na kwa wanaozuru kurasa yangu ya mtandao wa kijamii,

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh,

Hakika katika historia ya nyumati kuna masiku yenye kung’ara ambayo ni sehemu ya fakhari kwa nyumati hizo, basi huwaje uzito wake ikiwa masiku hayo ni sehemu ya kuthibiti bishara ya Mjumbe wa Allah (SAW)? Hakika hapana shaka masiku hayo huwa nyota yenye mwanga angani, bali ni jua lenye kung’ariza dunia na kuunyanyua Ummah juu angani…

Na katika masiku hayo ni masiku yetu haya mashuhuri, masiku ya kumbukumbu ya ufunguzi wa Constantinople … Hakika alianza mfunguzi kuipiga vita Constantinople na kuizingira kuanzia tarehe 26 Rabiu Al-awwal hadi ulipotimia ufunguzi wake alfajiri ya Jumanne tarehe 20 katika mwezi huu wa Jamad Al-uula 857 AH, yaani mzingiro uliendelea kwa kiasi cha miezi miwili. Na alipouingia Muhammad Al-fatih mji hali ya kuwa ni mshindi alishuka juu ya farasi wake akatembea kwa miguu, na akasujudu kwa ajili ya Allah SW kumshukuru kwa ushindi huu na kufuzu , kisha akaelekea kwenye kanisa la “Hagia Sofia” ambako walikusanyika humo Waroma na Makasisi wao, akawapa amani na akaamrisha kubadilishwa kwa kanisa la “Hagia Sofia” kuwa msikiti, na akaamrisha kujengwa msikiti kwenye eneo la kaburi la sahaba mtukufu “Abu Ayoub Al- Ansari”ambae alikuwa katika safu za awali za kutaka kuifungua  Constantinople  na akafishwa hapo,  Allah Amrehemu na Amridhie…  Kisha ‘Al-Fatih’ ambaye alipewa lakabu hii baaada ya ufunguzi huu akatoa maamuzi ya kuufanya mji wa Constantinople, kuwa ndio mji mkuu wa dola yake, badala ya ule wa mwanzo wa Edirne, na baada ya ufunguzi huu wa mji wa Constantinople (Kostantiniyye) ukapewa jina la “Islamu Bul” yaani ‘mji wa Uislamu’ “Dar Al-Islam”, na ukajulikana mji huo kwa jina mashuhuri la “Istanbul”. Kisha Al-fatih akaingia katika mji akaelekea “Haga Sofia” na akaswali humo na likawa (kanisa hilo) msikiti kwa fadhila za Allah, Neema na Hamdu zake … Na ukabaki hivyo kuwa msikiti twahir wenye kung’aa unaoimarishwa na Waumini mpaka alipoweza muovu wa zama hizi Mustafa Kamal kuzuiya kuswaliwa humo na akaunajisi kwa kuufanya kuwa makumbusho kwa ajili ya wanaokuja na kuondoka!

Na hivi ndivyo ilivyofikiwa bishara ya Mtume (SAW) katika hadithi yake tukufu, kutoka kwa Abdillah bin Amr bin Al-As amesema: Tulikuwa tumemzungukaMtume (SAW) tunaandika, mara akaulizwa Mtume (SAW) mji gani katika miji miwili utakaofunguliwa mwanzo Constantinople au Roma? Mtume (SAW) akasema:

«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلاً، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ

“Mji wa Heraclius utafunguliwa mwanzo, yaani Constantinople”. Imepokewa na Ahmad katika Musnad wake na Hakim katika Al-Mustadrak na akasema “Hadithi hii ni sahihi kwa sharti ya mashekh wawili na wao hawakuitoa”. Na akaiwekea maelezo Al-Dhahabi katika Al-Talkhis akasema: “Kwa sharti ya Bukhar na Muslim”. Na vilevile imekuja katika hadithi tukufu kutoka kwa Abdillah bin Bishr Al-Khath’ami kutoka kwa baba yake, hakika yeye amemsikia Mtume (SAW) akisema:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Itafunguliwa Constantinople, na Amir bora ni Amir wake na jeshi bora ni jeshi hilo” akasema Abdillah bin Bishr Al-Khath’ami, aliniita Maslama bin Abdil-Malik akaniuliza, nikamuelezea kuhusu (Hadithi hiyo) akafanya uvamizi wa kutaka kuifungua Constantinople. Imepokewa na Ahmad.

Na kumekuja maelezo yake (Hadithi hiyo) katika kitabu cha Majmai Alzawaid “Ameipokea Ahmad, Al-bazar na A-Twabarani na wapokezi wake ni wa kutegemewa”… Basi ikafikiwa bishara hii katika mikono ya kijana huyu Muhammad ‘Al-Fatih’ ambaye alikuwa si zaidi ya miaka ishirini na moja, lakini aliyetayarishwa kwa matayarisho imara tangu utoto wake.  baba yake mzazi Sultan Murad II alimlea vyema akamfanya asome kwa walimu bora wa zama zake, na miongi mwao ni “Ahmad bin Ismail Al-kuuraani” ambaye Al-Suyyut alimtaja kuwa alikuwa katika walimu wa mwanzo wa Al-Fatih na akasema kuhusu yeye: “Hakika alikuwa ni mwanachuoni, mjuzi, wameshuhudia wanavyuoni wa zama zake daraja yake na ukomavu wake, na walikuwa wakimuita: Abu Hanifa wa zama zake”. Pia sheikh “Aaq Shamsudin Sunkar” ndie wa mwanzo aliyepandikiza katika akili ya (ya A-lFathi) tangu utoto wake juu ya Hadithi ya Mtume (SAW) kuhusu “Ufunguzi wa Constantinople”,na akakua kijana huyu hali ya kuwa ana shauku ya kuuhakikisha ufunguzi huo kwa mikono yake … Na sheikh “Aaaq Shamsudin” alimsomesha Muhammad Al-Fatih elimu za msingi za Quran, Hadithi za Mtume (SAW) na fiqhi, na pia lugha za Kiarabu, kifursi na kiturki, na pia alimsomesha baadhi ya sayansi za maisha kama hesabu, elimu ya anga na historia… Zaidi ya haya ushujaa wake katika mbio za farasi na fani za kivita …Na hakika Allah alimkirimu kwa neema zake na fadhila zake ikamstahikia sifa aliyoisifu Mtume (SAW), kwahiyo Al-Fatih alikuwa Amir bora na jeshi lake lilikuwa ni jeshi bora kwa kujaaa imani katika nyoyo zao na viungo vyao vikatayarisha ukweli wa jihadi, walimnusuru Allah SW, naye akawanusuru kwa ushindi huu mkubwa. Alhamdulillah kwa Mola wa ulimwengu.

Hakika Al-Fatih alikuwa mwenye mtazamo na uoni mzuri, kila anapoona kasoro anairekebisha inavyostahiki bi-idhinallah, na kila kinapojiri kizuizi hukiondosha bi-idhnillah. Hakika vilimkabili vizuizi vitatu akavitatua kwa umahiri mkubwa na kwa akili yake ambayo inavutia:

1-Jeshi lake lilimlalamikia hali ya hewa baridi ambapo wapo katika jangwa wazi na farasi wao, kwa hiyo akawajengea ngome ikawa wanaingia hapo kila inapolazimu, akawa hataki jeshi lake liachane na mzingiro baada ya kukaa kwa muda mrefu halafu warudi kama walivyofanya wanajeshi wa Kiislamu huko nyuma waliojaribu kuivamia Constantinople. Bali yeye alikuwa hataki kurudi mpaka ifunguliwe Constantinople bi-idhnillah…

2-Pia mji wa Constantinople ulikuwa na makuta matatu, na kati ya kila tabaka la kuta na tabaka jengine ni mitaa kadhaa. Kwa hali hiyo  Al-Fatih aliemewa katika jambo hili. Kwani hawakuwa na silaha zenye nguvu za kuteketeza katika zama zao, bali silaha zenye nguvu walizokuwa nazo ni manati ambayo yanarusha mawe yaliyokuwa si madogo, lakini yalikuwa hayatoshi kutoboa matundu katika kuta kwa ukubwa huu. Na kwa kuwa Muhammad Al-Fatih alikuwa anafuatilia uwezo wa kijeshi katika ulimwengu, basi alikuja kutambua kuwa mmoja wa wahandisi wa Kihangari (Hungarian) kwa jina (Urban) ametayarisha fikra ya kutengeneza mizinga yenye nguvu maalumu na uwezo wa kuzing’oa kuta. Na asili mhandisi huyu Urban alikuwa mtumishi wa Mtawala wa dola ya Constantinople lakini haukumjali na kumpa umuhimu ipasavyo.

Al-Fatih akamkaribisha (mhandisi huyo) kwa uzuri akammiminia mali na akamfanyia wepesi (kumpatia) kila vifaa vitavyomuezesha kutimiza uvumbuzi wake. Kwa hiyo, Urban akaanza kutengeneza mizinga kwa msaada wa wahandisi wa dola ya Uthmania, na Al-Fatih akawa anasimamia yeye mwenyewe, na haikupita miezi mitatu Urban akawa ameshatengeneza mizinga mitatu mikubwa ya kurushia. Uzito wa urushaji wa mzinga huo ni tani moja na nusu, na hakutaka kuijaribu zana hii ya kurusha kwenye kuta za(Constantinople)  kwa khofu kuwa matokeo yasiwe kama anavyotaka, na hayo kuyaona Warumi nyuma ya kuta,  halafu hilo likaathiri nguvu na morali ya Waislamu, kwa hiyo akafanya majaribio mjini (kwake) “Edirne” na jaribio likafaulu, akamshukuru Allah SW na akazihamisha mizinga ile mitatu ya kurushia kutoka Edirne hadi karibu na makuta ya Constantinople, ili yavunjwevunjwe na Warumi waweze kusalimu amri…

3-Kisha kukawa na jambo jengine linalomshughulisha (Al-Fathi),alikuwa anaelewa kwamba kuta ni dhaifu katika eneo la ghuba lililozunguka Constantinople, na pamoja ya kwamba Warumi wanaelewa udhaifu wa kuta katika upande wa ghuba, lakini wao walikuwa nyoyo zao zimetulia kwamba marikebu za Waislamu haziwezi kuwafikia wao kwa kufungwa sehemu ya kuingilia ya ghuba kwa minyonyoro ya madini. Lakini Al Fatih, Allah SW akamfungulia kufikia maamuzi ya kuzisukuma marikebu kutoka kwenye milima ya Galata (Galata hills) iliyoelekea kuta kwa upande wa ghuba ya (pembe ya dhahabu/ golden horn), akachomeka magogo kwenye milima akayamwagia mafuta mengi na shahamu, kisha akazisukuma marikebu juu yake na akaweza katika usiku mmoja kuzishusha marikebu 70 kwenye ghuba, na jambo hili liliwashangaza Warumi. Na kulipopambazuka asubuhi na kuona marikebu za Waislamu katika ghuba nyoyo zao zilijawa na khofu, ikawa nusra na ukombozi, Alhamdulillah, Mola wa viumbe wote.

Enyi ndugu zangu, nimependa niwakumbushe baadhi ya mambo kuhusu ukombozi wa Constantinople kwa sababu tatu:

Kwanza: Kurejesha kumbukumbukizi hizi ili kila mwenye macho mawili aone ulivyo utukufu wa Uislamu na Waislamu, unapowekwa Uislamu wao kwenye nafasi ya utabikishaji wakati huo ukafiri unakuwa hauwezi kusimama, bali haki huwa juu na kunyanyuka mnyanyuko wa adhana (Allahu Akbar), na hakika ilikua hivyo, Fursi na Bayzantine zikanyenyekea mbele yake na karibu itazifuata hizo ndugu wa Byzantine ambae ni Rome Inshallah, kusadikisha sehemu nyengine ya bishara ya Mtume (SAW) kwa ukombozi wa Rome…

Pili: Ili nyoyo zenu zipate kutulia kwa kuzihakikisha bishara nyengine tatu za Mtume (SAW), kama ilivyofikiwa bishara ya kwanza, hakika ametubashiria rehema na amani ziwe juu yake ukombozi wa Constantinople , ukombozi wa Rome, kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume , kupigwa kwa Mayahudi na kushindwa kwao vibaya mno…  Na Mtume (SAW) hatamki kwa matamanio yake, hayakuwa anayoyatamka ila ni Wahyi. Na zitafikiwa bishara tatu za Mtume (SAW) zilizobakia kwa idhini ya Allah Aliyetakasika. Lakini hazitofikiwa kwa kuteremka Malaika kutoka mbinguni ili watupe sisi, bali hakika ya utaratibu wa Allah SW ni kuwa tumnusuru Yeye naye atupe ushindi sisi, kwa hiyo tusimamishe sharia yake na tunyanyue ukubwa wa Dola yake na tutayarishe nguvu tunazoweza kisha tupigane jihadi katika njia yake. Na wakati huo ardhi itang’aa kwa bishara tatu zilizobakia, na ardhi itang’aa upya kwa Khilafah…

Tatu: Hakika wamagharibi makafiri wameweza pamoja na makhaini waarabu na waturuki kuivunja Khilafah katika 1342H /1924 AD na kuchukulia kuangusha huku ni sawa na ukombozi wa Constantinople na hapo makafiri wamagharibi wakarejesha nguvu waliyoikosa. Na hima ya wamagharibi imekuwa ni kutumia juhudi katika kutorejea Khilafah upya, ili nguvu waliyoirejesha isijepotea, na hasa kwa kuwa wamekuwa ndio wakoloni wa miji ya Waislamu. Na wamekuwa wanafuatilia harakati katika biladi za  Waislamu. Na wakati kulipotangazwa kuasisiwa kwa Hizb ut Tahrir mwaka 1372H/ 1953AD na ikabainika kwa wamagharibi kuwa lengo la amali ya Hizb na kadhia yake nyeti (mtambuka) ni kurejesha upya Khilafah, na kwamba iko makini hasa (serious) katika amali yake hii, basi wamagharibi wakawaamrisha vibaraka wao ambao ni watawala kuizuiya Hizb na kuwatia ndani na kuwaadhibu wanachama wake hadi kufikia kuuawa katika baadhi ya maeneo, kisha (pia) kwa kuwahukumu vifungo virefu hadi vya maisha katika baadhi ya maeneo… Kisha wakazidisha kwa mbinu za uongo, kuwazulia uongo na kubadilisha mambo bila haya wala kimeme… Na ili uzushi huu uwe na athari kwa dhana yao, wakafanya miongoni mwa wale wanaoufanyia kazi kuwa watu wanaojiita kwa majina ya Waislamu na wanajipamba kwa muonekano wao. Kisha wakaendelea nao katika uzushi huu baadhi ya walioacha da’wa, waliovunja ahadi zao na walioadhibiwa katika wale waliokuwa katika Hizb awali…

Hivi ndivyo walivyoshirikiana watu wa aina hizi kwa pamoja katika uzushi, kusingizia uongo na kubadilisha mambo, na kila mmoja katika wao ana dori: Makafiri, wanafiki, na wenye kueneza habari za uongo. Kisha kikundi kidogo cha walioacha da’wa, walioadhibiwa, waliovunja ahadi zao na ambao katika nyoyo kuna maradhi wakashirikiana wote katika vitimbwi hivi dhidi ya Hizb na uzushi dhidi yake. Na wakaendelea na hayo kwa mpango wenye sumu wakitumikia uongo katika nyendo zao zote. Kila wanaposhindwa katika uongo fulani wanakuja na uongo mwengine na wanasahau wenye kutumikia uongo au wanajitia kusahau kwamba mashababu wa Hizb wana usafi wa akili na uwezo wa haraka wa kuelewa jambo na kutoa maamuzi na utambuzi wa kina wa mambo ambayo huwafanya watafautishe  ovu na zuri, kwahiyo hawauachi uongo uingie kwenye kundi lao…

Kwa hivyo, juu ya kwamba mbinu za kupamba uzushi walizozitumia, na ijapokuwa kutengeneza uzuri katika kubadili ukweli wa mambo, mambo ambayo yaliwachosha wenyewe katika kuyatengeneza, ila hakika mambo hayo hayakupata usikivu kwa mashababu wa Hizb wala kwa mwenye akili yeyote yule katika Waislamu. Bali yalikuwa:

﴿كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً﴾،

“Kama mangati njiani ambayo mwenye kiu huyadhania maji mpaka anapoyafikia hakuti kitu”

[Nur: 39].

Na pamoja na vitimbwi vyote walivyovifanya na uovu waliouunda na matendo yao mabaya kwa Hizb na uongozi wake wakidhania miongoni mwao kwamba wataiathiri Hizb, hakika dhana yao imekuwa yenye kuwarejea wenyewe, kisha kwa idhini ya Allah watakuwa wenye kushindwa hawatafikia kheri kwa hali yoyote ile hata ukirefuka uongo wao, mbinu zao na vitimbwi vyao.

﴿وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ﴾،

“Na havimstahikii vitimbwi viovu isipokuwa mwenye” [Fatir: 42].

Na watayakuta mwisho wake hayo mbele ya Allah SW hata uzushi wao na vitimbwi vyao vikiwa vikubwa kiasi gani:

﴿وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ﴾.

Na hakika walifanya vitimbwi vyao, na vitimbwi vyao hivyo mbele ya Allah (ndiko vitamalizia) hata vikiwa vitimbwi vyao vinaondosha milima” [Ibrahim; 46]

Mwisho, hakika misimamo yenu yenye nguvu enyi ndugu zangu, yenye kuthibiti juu ya haki, iliyo safi yenye nguvu mbele ya kampeni za mfululizo dhidi ya da’wa ya haki, hakika inatukumbusha misimamo ya masahaba (RA) kufuata misimamo ya Mtume (SAW) iliyo madhubuti, mikubwa katika kukabiliana na shida kadhaa…Hii ndio misimamo yenu, misimamo imara na thabiti haidhoofiki kwa mitihani na wala haitikisiki kwa fitna, bali azma zenu zinapata nguvu na hupasuka kwa haki mishipa yenu ya shingo, munaiangalia dunia mara moja na akhera mara kadhaa, basi hongera kwa Hizb kwenu na hongereni kwa Hizb.

﴿رِجَالٌ لَا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْماً تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ*لِيَجْزِيَهُمُ اللَّهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Wanaume ambao hawashughulishwi na biashara wala kuuza wakaepukana na utajo wa Allah, Na husimamisha swala na kutoa zaka, wanaiogopa siku ambayo nyoyo na macho vitakodoka. Ili Allah awalipe mazuri kwa yale waliyoyatenda na ili awazidishie katika fadhila zake. Na Allah anamruzuku amtakae bila ya hisabu” [Nur: 37-38]

Na mwisho wa yote, nanyenyekea kwa Allah (SWT) afuatishe kufikiwa kwa bishara za Mtume (SAW) irejee Khilafah ya ummah huu, kisha ikombolewe Quds yake, na kisha ikombolewe Rome kama ilivyotangulia ndugu yake na ikawa… Kusadikisha ukweli wa Hadithi za Mtume (SAW) … Kama ambavyo tunamuomba Allah (SWT) Atupe msaada kutoka kwake ili tufanye amali ya da’wa vizuri na kwa usafi wake ili tuwe tunastahiki nusra ya Allah Mwenye kushinda Mwenye kurehemu.

﴿وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴾.

“ Na siku hiyo watafurahi  Waumini. Kwa nusra ya Allah humnusuru amtakae naye ni Mwenye kushinda Mwenye kurehemu” [Rum: 4-5]

Wassalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Ndugu yenu

Atta Ibn Khalil Abu Rashtah

Amir wa Hizb ut tahrir

Alkhamis, 7 Jumada Al-uula 1441H

2/1/2020

#ﻓﺘﺢ_ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻨﻴﺔ
#ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻴﻨﻴﺔ
#ConquestofIstanbul
#İstanbulunFethi
#istanbul

 

Maoni hayajaruhusiwa.