Jihad Katika Kufanya Kazi ya Kurudisha Khilafah

Swali:
Hizb ut Tahrir wamechukua kipindi cha Makkah kama Manhaj ya kusimamisha Khilafah, na si kipindi cha Madinah, kwa kuandaa matendo ya kivita (Jihad) kwa ajili hiyo, ambayo wanadai inaenda kinyume na Sheria, kwa sababu Mtume (saw) hakupigana Jihad wakati wa kusimamisha Dola.
Kwa nini Hizb ut Tahrir isichukuwe dalili za kusimamisha Khilafah katika kipindi cha Madina ambapo Jihad ilikua ishasimama na inafanyiwa kazi?
Je kuna jibu lenye kukinaisha na lenye kutosheleza juu ya suala hili?
Allah akujaze kheri.

Jibu:
Hakika katika kujibu swali hili kuna mambo muhimu yanahitaji kubainishwa:
Kwanza, dalili zilizokuja sawa ama ziwe ni kutokamana na Kitabu ama Sunnah ni lazima kufuatwa kama zilivyo na hakuna tofauti kati ya dalili zilizopokewa Makkah al-Mukarramah na kati ya dalili zilizopokewa Madina.
Pili, dalili zinazotakiwa ni dalili juu ya suala fulani na si dalili nyenginezo zisizo juu ya suala hilo:
Kwa mfano: Ukitaka kujua vipi Kutawadha, basi utachambua dalili za udhu kama zilivyo, sawa sawa ziwe zimeteremka Makkah au Madinah na huvuliwa Hukmu ya Kisheria kwayo kulingana na kanuni zinazofuatwa. Lakini huwezi kuchambua dalili za Saum ili uchukue hukmu ya Udhu au namna ya kutawadha.
Au kwa mfano unapotaka kujua hukmu za Hijjah, kadhalika utachambua dalili za Hijjah kama zilivyo, sawa sawa ziwe zimeteremka Makkah au Madinah, na hufanyiwa Istinbaat Hukmu ya Kisheria kwayo lakini huwezi kufanya utafiti dalili za Swala ili uchukue hukmu ya Hijjah na namna yake.

Vivyo hivyo, unapotaka kujua Hukmu za Jihad, ufaradhi wake kwa kila mtu (فرض عين ) au faradhi ya kujitosheleza (فرض كفاية), jihad ya kujihami (دفاع) ama yakufuata (ﺍطلب) na yanayoambatana na jihad katika hukmu za kufungua miji na kusambaza Uislamu kwa nguvu ama kwa sulhu …. basi unapaswa kufanya uchambuzi (بحث) dalili kama zilivyo, sawa sawa ziwe zimeteremka Makkah au Madinah na huvuliwa kwayo hukmu ya Kisheria kulingana na kanuni zinazofuatwa lakini huwezi kufanyia uchambuzi (بحث) dalili za Zakka ili uweze kuchukua hukmu ya Jihad na ufafanuzi wake.
Basi katika kila jambo, hakika hufanyiwa uchunguzi (بحث) wa dalili popote ilipoteremka – Makkah au Madinah na huchukuliwa Hukmu ya Kisheria katika suala kutokamana na hizi dalili kulingana na kanuni zinazofuatwa.
Na sasa tunakwenda katika masuala ya kusimamisha Dola ya Kiislamu ili tuchambue (بحث) dalili zake sawa sawa ziwe zimeteremka Makkah au Madinah na kuifanyia uvuaji wa Kisheria kwayo kulingana na kanuni zinazofuatwa.
Kwa hakika sisi hatupati dalili yoyote ya kusimamisha Dola ya Kiislamu, isipokuwa zile alizozibainisha Mtume (saw) katika seera yake katika mji wa Makkah.
Mtume alilingania Uislamu kisiri akapata kundi lililo muamini na lenye subra … kisha akatangaza mbele ya watu katika mji wa Makkah na katika misimu ya Hijjah…. kisha akaomba nusra kwa wenye nguvu na himaya … ALLAH akamkirimu kwa Maanswaar, akahama kwenda kwao na kusimamisha dola Madina.
Hizi ndizo dalili za kusimamisha Dola na hatujaona dalili zengine, kwani Mtume ashatubainishia katika seera yake kwa uwazi unaojitosheleza na ni juu yetu kujilazimu nayo.
Maudhui sio kipindi cha Makkah kabla ya kufaradhishwa JIHAD wala kipindi cha Madina baada ya kufaradhishwa Jihad, bali ni uchambuzi (بحث) wa dalili za Kisheria juu ya kusimamisha Dola ya Kiislamu (Khilafah). Na dalili zenyewe hamna ila katika mji wa Makkah mpaka alipofanya Hijra Mtume (saw) kwenda Madina na kusimamisha Dola.
Kwa hiyo manhaji ya kusimamisha Dola ni jambo jengine na Jihad ni jambo jengine, na kama tulivyosema hakika dalili za kusimamishwa Dola huchukuliwa kutoka madhaanni yake na dalili za jihad huchukuliwa kutoka madhaanni yake hili si lile na lile si hili na haya mawili hayasimami mahala pamoja.
Na ndio maana Jihad haiwezi kuachwa kwa sababu kuna dola ya Khilafah.
Na Mtume (saw) amesema:

وَالْجِهَادُ مَاضٍ مُنْذُ بَعَثَنِي اللهُ إِلَى أَنْ يُقَاتِلَ آخِرُ أُمَّتِي الدَّجَّالَ، لَا يُبْطِلُهُ جَوْرُ جَائِرٍ، وَلَا عَدْلُ عَادِلٍ

“Na Jihad itaendelea kutoka aliponitumiliza Allah azza wajalla mpaka atakapompiga vita wa mwisho katika ummah wangu dajjali na wala haitobatilishwa na uovu wa muovu wala uadilifu wa muadilifu”

Kwa hiyo, Jihad inaendelea kulingana na Hukmu zake za Kisheria sawa iwe Khilafah imesimama ama haijasimama, na kadhalika haitoachwa kazi ya kusimamisha Khilafah kwa sababu watawala au Waislamu wameiwacha Jihad. Kwa hiyo, kufanya kazi kusimama Khilafah kutaendelea mpaka itakaposimama kwa sababu ni haramu kwa Waislamu wenye uwezo kuishi bila ya Khalifah… Mtume (saw) amesema:

من خلع يدًا من طاعة الله لقي الله يوم القيامة، لا حجة له، ومن مات وليس في عنقه بيعة، مات ميتة جاهلية

“Yeyote atakayeondoa mkono wake katika twaa atakutana na Allah siku ya qiyama hana hoja na atakaye kufa na katika shingo yake hakuna (amiri anaestahiki) baya’h amekufa kifo cha kijahilia”.

Kwa hiyo, Jihad inaendelea na kazi ya kusimamisha khilafah inaendelea mpaka itakaposimama na moja wapo haisimamishwi na nyengine kwani haya ni masuala mawili tofauti na huchambuliwa (بحث) kila suala katika dalili zake za kisheria, na hufanyiwa (istinbat) uvuaji kwahio hukmu ya kisheria maalumu kulingana na kanuni zinazofuatwa.
Na ndio maana Hizb ut Tahrir imejifunga na njia ya Mtume (saw) ambayo ameibainisha katika mji wa Makkah mpaka aliposimamisha Dola Madina na Rasulullah hakutumia matendo ya kivita katika marhala zote tatu za Da’wah ya kusimamisha Dola.
Na ibainike wazi kwamba, katika dalili za kusimamisha Dola hakuna ila zile alizozibainisha Mtume (saw) katika mji wa Makkah mpaka aliposimamisha dola katika mji wa Madina.
Kwa hiyo, katika masuala ya twariqa/njia ya kusimamisha Dola hakuna njia aliyobainisha Mtume (saw) isipokuwa ile ambayo iko katika seera yake ndani ya Makkah, na lau suala litakuwa ni katika kazi za Dola ya Kiislamu na muundo wake… basi tungelizichukua kutokana na dalili ambazo amezibainisha Mtume (saw) katika mji wa Madinah kwani ndiko dola ilikosimama.

Kwa ufupi:
– Hakika hukmu yoyote juu ya jambo fulani huchukuliwa kutokana na dalili zilizokuja katika hilo jambo iwe ziliteremka Makkah ama Madinah, hukmu za saum katika dalili za saum, hukmu za swala katika dalili za swala, hukmu za Jihad katika dalili za Jihad na hukmu za kusimamisha Dola katika dalili za kusimamisha Dola…
-Kwa hiyo hatuna budi kujilazimisha na twariqa ya Rasul (saw) katika mji Mtukufu wa Makkah katika kusimamisha Dola nayo ni kwa kuwa hakuna dalili za kusimamisha Dola ila hiyo katika Makkah … na lau kungekuwa kuna dalili zilizokuja Madina za kusimamisha Dola ingekuwa tuzichukue kama dalili nazo pia.
Mwisho tunamuomba Allah Taala msaada na tawfiq ya kusimamisha Khilafah Rashidah, ili wapate izzah Waislamu na Uislamu na wadhalilike makafiri na ukafiri na ienee kheri katika pembe zote za ulimwengu na hilo si zito kwa Allah mtukufu.

27 Dhul-Qaada 1434 H
22/9/2013 M

Maoni hayajaruhusiwa.