Mradi Mpya Juu ya Syria

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali

Yaliyotokea mjini Daraa kutokana na serikali kuyavamia kwa haraka maeneo yaliyo hamwa kwa miaka, na kufuatiwa na Quneitra na kabla ya hapo Ghouta na kabla yake Aleppo na dada zake, na macho yote sasa yanaelekea Idlib, hii inaonesha kuwa yapo mambo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti na utambuzi. Na tumeona dori ya Amerika na njama zake na dori ya vyama vinavyoiunga mkono na njama zake na kuidhinisha kisiri kwa Dola wadhamini uzuiaji wa ongezeko la ghasia, mithili ya Uturuki, au kushiriki ndani yake kivitendo mithili ya Urusi. Ni yapi yaliyojiri au yanayojiri? Ni vipi nchi hizi zimeweza kuyaingilia mapinduzi ya Syria kwa njia hii? Ni dori gani zilizocheza? Na ni kipi kifuatacho?

Jibu

  1. Baada ya kuzinduliwa kwake mnamo 2011 na tishio lake la kumng’oa Bashar, kibaraka wa Amerika, na kuenea kwa hamasa za Kiislamu, na tishio lake la kubadilisha sura ya eneo hilo kuwa ya Uislamu, mapinduzi ya Syria yalikuwa ni tukio la mabadiliko katika ncha mbili zenye umuhimu mkubwa sana; kwa ncha ya kwanza yaliangazia nguvu imara za kieneo zisizofuata Amerika wala Ulaya. Hivyo basi, kwa mara ya kwanza katika kiwango hiki kulikuwepo na nguvu ya kipekee iliyochipuza ndani ya Umma pasi na mamlaka ya makafiri juu yake. Kwa ncha ya pili, Amerika, Dola kuu nchini Syria na ulimwenguni, ilishindwa kuyakomesha. Ilikuwa mithili ya miujiza!

Syria haikuwa chini ya mzozo wa kimataifa. Lakini mzozo ni kati ya Amerika na wafuasi wake na vibaraka wake, upande mmoja, na watu wa Syria upande mwengine, Ulaya haina ushawishi wowote juu ya Syria, kama ilivyo nchini Yemen na Libya kwa mfano. Amerika inaidhibiti serikali hiyo, wafuasi wake na vibaraka wake. Mzozo huo ni kati ya Amerika, wafuasi wake na watu wa Syria wenye ikhlasi.

Lakini, mapinduzi ya Syria yameikosesha usingizi Amerika, hata Raisi Obama alitaja kuwa nywele zake ziligeuka mvi: “Nina imani sana kuwa kiasi kikubwa cha mvi zangu kimetokana na mikutano yangu ya Syria” alisema. (Ra’I Al Youm, 5/8/2016)

  1. Amerika imechukua njia mbili tofauti kufikia lengo kubwa kabisa la Amerika katika eneo hilo, nalo ni, kuyamaliza mapinduzi ya Syria, na kuendeleza utawala wa kibaraka:
  2. Njia ya kwanza: ni kutoa usaidizi wote wa kifedha na kijeshi kwa serikali hiyo jijini Damascus ili isiporomoke, ikiwemo kuisukuma Iran na wanamgambo wake kwenda Syria kupigana bega kwa bega na Bashar, na kisha kuisukuma Urusi kwa njia hiyo hiyo. Raisi wa Urusi, Putin, alitangaza kuingilia kati kwa Urusi nchini Syria mwishoni mwa Septemba 2015 punde tu baada ya mkutano wake na aliyekuwa Raisi wa Amerika Obama jijini New York. Amerika imepiga marufuku mashirika na taasisi zote za kimataifa kutokana na tuhuma zozote za kihakika kwa serikali ya Bashar licha ya uzito wa uhalifu wake uliofikia kutumia silaha za kemikali.

Ingawa iliitishia serikali hiyo endapo ingetumia silaha za kemikali, lakini haikufuatilia vitisho vyake kwa kuhofia serikali hiyo. Na hili ndilo lililotokea: Pindi serikali hiyo ilipotumia silaha za kemikali mjini Ghouta mnamo 21/8/2013, Amerika ilituma manuari zake za kivita kushambulia serikali hiyo, lakini ikasita kufanya hivyo ili kutoathiri dhati ya serikali hiyo kwa mashambulizi haya! Na kuipelekea kuporomoka kabla ya kupatikana kwa kibaraka badali, kwa sababu haijamuona katika Muungano wa Kitaifa wa Syria, ambao umethibitisha uwezo wa kujaza pengo hilo, hususan kwa kuwa umejianika wazi kutokana na mahusiano yake na Amerika na vibaraka wake, hivyo basi ndio sababu Amerika imerudi nyuma, na kukataa kwake ni dalili wazi kwa kila mwenye macho kuona kuwa Amerika inataka kuihifadhi serikali hiyo, licha ya shambulizi la kinyama la kemikali la serikali hiyo… Licha ya hayo mapinduzi nchini Syria yangali imara na hata kuimarika uwanjani.

  1. Njia ya pili, ambayo ndiyo ya hatari zaidi, ni kuyadhibiti (mapindizi hayo); Amerika ilitangaza kuwa iko pamoja na mapinduzi ya Syria, kwa kuyahadaa makundi ya wapiganaji kwa sababu haikuyapiga vita hadharani, lau wangekuwa na utambuzi wangejua kuwa inawatumia wengine kwa kazi hii! Tayari tushawahi kutaja hili katika toleo lililochapishwa mnamo 11/10/2015, linalosema: “… hili hapa ndilo janga; Amerika inajionesha kuwa pamoja na wanamapinduzi, na ni vigumu kuwapiga vita hadharani, na wamesababisha uharibifu kwa serikali, lakini badali ya Amerika bado haijapatikana. Hivyo basi imeanzisha mchezo mchafu hatari wa kuipa Urusi kazi hii, ya kuisaidia serikali hiyo hadharani na kupigana na wanamapinduzi hadharani, na vita vyake vimehalalishwa, na serikali hiyo ilikuwa tayari kuiita Urusi, kwa agizo kutoka kwa Amerika, na hili ndilo lililotokea … Urusi ilikubali dori hii chafu na ovu nchini Syria ili kuihudumia Amerika!”

Hivyo basi Amerika ilisema kuwa inausaidia upinzani kwa pesa na silaha, lakini yalikuwa ni maneno matupu bila ya vitendo! Kwa sababu Amerika inazuia kuwasili kwa silaha zozote zenye athari kwa mapinduzi hayo kupitia Uturuki au Jordan, na ilituma baadhi tu ya usaidizi kama makoti ya kuzuia risasi pekee ili kumakinisha ile dhana kuwa imesimama pamoja na mapinduzi hayo. Na ilitangaza kusaidia na kutoa mafunzo, yaliyonufaisha watu wachache pekee, na wakati mwengine wasiozidi watano. Lengo la hili lilikuwa ni kuyavutia makundi hayo kwake. Amerika ilitarajia kuwa madai haya yangefichuka wakati wowote, hivyo basi ilitumia wafuasi wake katika eneo hilo, hususan Uturuki na Saudi Arabia katika enzi ya Mfalme Salman, mwanzoni mwa 2015, nchi hizi zilipewa kazi ya kuyadhibiti mapinduzi hayo, na kupata utiifu kutoka kwa viongozi wa makundi hayo na kuyayusha kitambulisho cha Uislamu katika mapinduzi hayo, na nchi mbili hizi zikatumia vyombo vyao vya ujasusi kufikia hili. Pamoja na ufadhili mchafu wa kifedha, mashekhe (walinganizi) waovu, na kutoa nafasi, hifadhi, jukwaa la vyombo vya habari, na pesa zenye sumu.

  1. Kwa sababu mapinduzi hayo nchini Syria wakati huo yalikuwa imara katika malengo yake na Uislamu, ilikuwa ni muhimu kuongeza zaidi matumizi ya vyombo hivi vya ushawishi wa Amerika, baadhi ya duru hata pia zimeripoti kuwa baadhi ya makundi nchini Syria yalipokea karibu dolari bilioni moja! Kupitia usaidizi wa kifedha,na kupewa jukwaa la vyombo vya habari na umuhimu wake, na hifadhi na uzito wake, wafuasi wa Amerika “Saudia na Uturuki” ziliweza kupata ushawishi juu ya upinzani na makundi ya kijeshi, na zikayaunganisha na ujasusi wa nchi hizo, mpaka kila moja ya nchi hizo mbili, hususan kupitia nukta za kifedha na nguvu ya vyombo vya habari, ziliweza kuwaangazia viongozi wake na kunyanyua vyeo vyao, na kuyadhibiti makundi hayo kupitia wao! Amerika, kwa kutumia vibaraka wake wote na vyombo vyake eneo hilo, inataka kuyapotoa mapinduzi ya Syria na kuyakoroga malengo yake.

Ilitangaza kuwa lengo lake nchini Syria na katika muungano wa kimataifa ni kupigana na ‘ugaidi’ yaani kupigana na makundi ya mapinduzi ya Syria. Licha ya kujiingiza kwake katika vita nchini Syria tangu 2014, mashambulizi yake ya mabomu yalifungika kwa kuyashambulia makundi inayoyaita ‘ya kigaidi’. Kamwe haishambulii majeshi ya Bashar, na inashirikiana na Urusi. Lakini, viongozi wengi wa makundi ya wanamgambo wanaiamini (Amerika) na kushirikiana katika oparesheni zao pamoja na vyombo vya ujasusi, MOM na MOC, na hata kujihusisha na vita inavyoviita “vita dhidi ya ugaidi”, hivyo basi kuanzisha mapigano ya kindani na umwagaji damu haramu. Hili liliyakanganya mapinduzi ya Syria, ambayo yalianza kupigana kwa sura mbili, sura ya Amerika dhidi ya “ugaidi”, iliyoongezwa ile sura asili ya “kuing’oa serikali hiyo”. Makundi hayo ya wapiganaji yalikuwa chini ya shinikizo kutoka Uturuki na Saudi Arabia juu ya shinikizo zaidi la kimataifa la kuendelea zaidi na kujihusisha na sura ya Amerika, na kuyaondoa kutoka katika sura asili!

Kuingilia kati kwa Uturuki, “Ngao ya Furat” kulikuwa ndio hatima ya muondoko huo. Uturuki iliyataka makundi yake kujiondoa kutoka katika vita vya Aleppo na kuelekea kaskazini kupigana na ISIS. Hivyo basi, majeshi ya Bashar na washirika wake, Urusi na Iran yakafaulu kuukalia mji wa Aleppo mwishoni mwa 2016, katika oparesheni iliyofanana na Uturuki kuikabidhi Aleppo kwa Warusi na kisha kwa serikali! Majibu ya makundi ya kisilaha ya Uturuki na kujiondoa kwao katika vita vya Aleppo na kujihusisha kwao na sura ya Amerika dhidi ya “ugaidi” ilikuwa ni dalili hatari mno, kwani ilionyesha wazi wazi kuwa uongozi wa makundi hayo ulikuwa ukilishwa mamilioni ya dolari, na kuwa na ushawishi mkubwa juu ya makundi yao. Na kwamba iliiwezesha Amerika, baada ya kusubiri kwa muda mrefu, kufungua ukurasa wa matumaini ya kuyamaliza mapinduzi hayo ya Syria.

Sera ya Amerika iliendelea kuuongoza uwanja wa Syria katika mwelekeo wa kuyamaliza mapinduzi hayo, lengo ambalo Amerika ililiona lawezekana baada ya kufaulu na wafuasi wake kuchukua utiifu wa viongozi wengi wa makundi ya kijeshi.

Kisha Erdogan akarudia mandhari ya “Ngao ya Furat”, akavumbua “Tawi la Zaituni” ili kuirahisishia serikali kuingia Idlib. Pindi serikali ya Syria ilipoanza kuisongelea Idlib na kuizunguka kambi ya anga ya Al-Duhur, Erdogan alivisukuma vita kuelekea Afrin! Karibu wapiganaji elfu 25 wa upinzani walishiriki, na kiongozi wa kijeshi eneo la Failaq Ash-Sham, Yasser Abdul Rahim, akathibitisha kuwa takriban wanajeshi elfu 25 kutoka Jeshi Huru la Syria wanashiriki katika oparesheni ya kijeshi ya Uturuki mjini Afrin … (Russia Today: 23/1/2018), hili lilifanyika kwa utambuzi wa Amerika na ridhaa yake. Waziri wa Kigeni wa Uturuki Mouloud Gaoucheğlu alisema kuwa “alijadili juu ya mgogoro wa Syria na kadhia ya vitengo vya usalama mipakani pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Amerika James Matiss mnamo Jumatatu jioni (15/1/2018) nchini Canada,” (Anadolu Agency 17/1/2018). Haya yalithibitishwa na taarifa za Amerika, zinazoashiria kuwa Tawi la Zaituni na kadhia ya Afrin na harakati za jeshi la Uturuki zilifanywa kwa ridhaa kamili ya Amerika na kwa mawasiliano ya Urusi na Amerika, na kutokana na taarifa hizi: “Kitengo Kikuu cha Utoaji Amri za Kijeshi cha Amerika kilisema kuwa Uturuki iliwadokeza juu ya oparesheni ya kijeshi katika mji wa Syria wa Afrin.” (Quds Press, 21/1/2018)

  1. Mpangilio wa sera ya Amerika nchini Syria baada ya kusalimishwa kwa Aleppo ni kama ifuatavyo:
  2. Kutuliza uwanja wa Syria: anwani kuu ya lengo hili ni mbinu ya Astana, ambapo Uturuki inayalazimisha makundi yanayoegemea upande wake, kujadiliana na Bashar, Iran na Urusi kusitisha vita. Mtindo huu ulimalizikia kwa yale yanayoitwa makubaliano ya “kupunguza joto la kivita”, yaliyokuwa yanakwenda kutoka eneo moja hadi jengine.

Yalifika kusini, ambako mwanzoni makundi yake hayakushiriki katika majadiliano ya Astana, lakini hatimaye yakashiriki. Katika kipindi cha miaka miwili ya majadiliano hayo, Uturuki iliibuka kama mdhamini wa makubaliano hayo pamoja na Urusi na Iran. Nguvu za mapinduzi hayo za miaka yake ya mwanzoni zilizuia kusitisha vita kwa aina yoyote. Lilikuwa ni lengo lisilofikika la utawala wa Obama, lakini lilianza kupatikana kufikia mwishoni mwa utawala huo mnamo 2016 na kisha utawala wa Trump ukawasili.

Kutuliza uwanja wa Syria kulimaanisha kuwa Amerika ilitoa mwanya wa majadiliano pasi na vitisho vya moja kwa moja vya kuiondoa serikali ya Bashar kijeshi, lakini kwa majadiliano yanayothibitisha uhalali wa serikali hiyo na hivyo basi hakuna lolote katika maamuzi yake lililoashiria kuondolewa kwa Bashar. Hii ni kwa sababu Amerika iliutumia Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, inalolidhibiti, na kuwatuma wafuasi wake, wajumbe, weusi, kijani na weupe, kuanzia Kofi Annan hadi Lakhdar Brahimi mpaka de Mistura, na ikaweka makongamano ya Geneva kuuleta pamoja upinzani wa serikali hiyo, kuanzia Kongamano la Geneva 1 mnamo 30/6/2012, yote yakiwa ni kuitambua serikali hiyo na kuihifadhi. Vile vile makongamano yaliofanywa Vienna, Vienna 1 na 2 mnamo 2015. Mojawapo ya mambo muhimu katika makongamano yaliyofanywa jijini Vienna, Vienna 1 na 2 ni kuhifadhi sura ya kisekula ya dola ya Syria na taasisi zake. Uamuzi wa hivi karibuni zaidi wa kimataifa ni ule uamuzi uliofanywa na Amerika yenyewe mnamo 18/12/2015 na kukubaliwa kwa pamoja na Baraza hilo, ni uamuzi unaofupisha maamuzi yote na natija za makongamano ya Geneva na Vienna kuhusiana na Syria, na kuyafupisha kwa azimio moja, nambari 2254.

Uamuzi huu umekuwa ndio maregeleo ya hali ya kisiasa nchini Syria, na nchi zote zinalingania kutekelezwa kwake yakiwemo makundi ya kisilaha chini ya ushawishi wa nchi saidizi zinazolingania wito huo. Azimio hili halilinganii kuondolewa kwa Bashar! Thibitisho la ulinzi wa Amerika kwake yeye na serikali yake, hii ndio hali iliyokuwa hadi Aleppo ilipokabidhiwa, na kisha kuyalazimisha makundi ya kisilaha kutofungua mipaka kukawa hakuna budi, na kisha kuyashinikiza kufikia hilo na kujifunga na kusitisha vita kikamilifu, na kuiacha serikali pamoja na Urusi na Iran (wadhamini wengine wa kupunguza joto la mapigano) kuliteka eneo la wanamapinduzi hao, moja baada ya jengine. Mdhamini wa tatu, Uturuki haikutoa kidole juu ya ukiukaji huo! Serikali ililipua kwa mabomu eneo la Bonde la Barada, hata kabla wino wa makubaliano ya kwanza ya kupunguza joto la kivita mwanzoni mwa 2017 bado haujakauka, huku mdhamini huyu ikitazama wazi wazi! Lakini kujihusisha kwao kulifikia kuhusisha ujasusi wao, pindi serikali hiyo ilipochochea vita vya Ghouta mashariki, katika oparesheni za “kupambana na ugaidi” mjini Ghouta “msemaji wa raisi wa Uturuki Ibrahim Kalin katika mkutano wa waandishi habari mnamo Jumatano katika idhaa ya habari ya TRT alisema kuwa Uturuki haitaki uwepo wa mashirika ya misimamo mikali eneo la Ghouta mashariki.” (Reuters, 15/3/2018) Alisema haya huku serikali hiyo, Urusi na Iran na wafuasi wao wakiilipua Ghouta kinyama kwa kwa mabomu, kana kwamba Erdogan wa Uturuki anahalalisha kitendo chao!

  1. Kuhusisha sera ya Amerika kwa jina la “kupambana na ugaidi”: Baada ya Raisi wa Amerika Trump kutangaza nia yake ya kuimaliza ISIS, na katika kupanua vita vya Mosul, Amerika ilifuata sera hii kwa sura nne:

– Sura ya kwanza: jeshi la Amerika liliyaongoza makundi ya Kikurdi, yanayosaidiwa na Amerika kuitoa ISIS kutoka Raqqa, na pia liliyaongoza makundi mengineyo eneo la mashariki mwa Syria kupigana na ISIS. Hivyo basi Wakurdi walikuwa na udhibiti mkubwa kaskazini mwa Syria, haswa katika maeneo ya Kikurdi nchini Syria. Nguvu kuu za Kikurdi zilikuwa ni Chama cha Kidemokrasia cha Kikurdi (KDP). Kwa usaidizi kutoka Amerika kiliweza kulimiliki tena eneo kubwa zaidi kutokana na udhibiti wa ISIS na kuyachukua maeneo yote ya mashariki mwa Furat; yaani asilimia 18 ya ardhi ya Syria, na ndio eneo lililo na utajiri mkubwa zaidi wa mafuta na gesi, pamoja na maji na rasilimali za ukulima, kuanzia Kobani hadi Raqqa, eneo la Bukamal na maeneo ya Deir al-Zour. Na hili halikuiathiri serikali hiyo. Majeshi ya Kikurdi huenda kwa mujibu wa maagizo kutoka kwa Amerika na hivyo basi hayakusimama usoni mwa serikali hiyo. Vyombo vingi vya habari hivi majuzi vilisambaza ripoti za kukabidhiwa maeneo kwa Vitengo vya Usalama vya Raia, kiungo kikubwa chenye nguvu za kidemokrasia ndani ya Syria, kutokana na maagizo ya Amerika, kwa serikali ya Syria; kwa msingi wa makubaliano yaliyofanyika jijini Damascus na Qamishli.

“Kiongozi wa Baraza la Kitaifa la Kikurdi nchini Syria, Fuad Aliko, alifichua sababu na mabadiliko yaliyokishajiisha Chama cha Kidemokrasia cha Muungano wa Kikurdi “PYD” kufanya makubaliano ya kisiri na serikali ya Syria, na serikali hiyo kupokea maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa majeshi ya Kikurdi kwa msingi wa masharti na mambo yaliyo katika makubaliano hayo, ikiwemo mtaa wa An-Nashwa katika mji wa Hasaka, na maeneo mengine mashariki mwa Mto Furat.” (https://arabi21.com, 16/07/2018) Na tovuti ya Herapolis (http://www.hierapolis.net) ilinukuu duru binafsi isiyo jina, kuwa mkutano ulifanywa Jumamosi iliyopita, “baina ya vinara wa wanamgambo wa KDP wanaowakilisha baraza lake la kijeshi la Munbaj, na maafisa wa serikali ya Assad katika makao makuu ya Chama cha Baath jijini Aleppo”. Aliongeza kuwa walijadiliana “kulikabidhi eneo la usalama katika jiji la Manbaj kwa wanamgambo wa serikali pamoja na Bwawa la Mashahidi (Bwawa la Tishreen) kusini mashariki mwa jiji hilo.” (www.qasioun-news.com, 11/07/2018)

Na viongozi hao wa makundi ya Kikurdi eneo la kaskazini mwa Syria wako chini ya udhibiti wa Amerika, ikiwa Amerika itawataka warudi katika mikono ya kibaraka wao Bashar, hawatakataa. Ipo ishara ya hili, gazeti la mtandaoni la “Ra’i Al-Youm”, 7/6/2018 lilimnukuu kiongozi mkuu wa Wakurdi Salih Muslim akizungumzia kuhusu kukimbilia kujadiliana na serikali hiyo, alisema: “Milango yetu daima imekuwa wazi kwa kila mtu na tumeona tofauti katika mazungumzo ya Assad ya hivi karibuni. Haya ni maendeleo … na kama vile kila mtu anavyoyafikiria maslahi yake sisi pia tutafanya vivyo hivyo”. Taarifa ya Waziri wa Kigeni wa serikali ya Syria, Walid al-Muallem ilinukuliwa na gazeti la Al-Arab lililo na makao yake jijini London, 27/9/2017: “Wakurdi wa Syria wanataka muundo wa kujitawala wenyewe ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria, na hii ndio kadhia ya majadiliano na mazungumzo”. Serikali hiyo na Wakurdi ni karata za Amerika ambazo haziwasilishi vikwazo vyovyote kwa hali ya kisiasa. Kile Amerika inachotaka kwao wao hawakipingi wa serikali hiyo haikipingi, ima wabakie kama walivyokuwa, kabla ya 2011 au pamoja na utawala wao huru ndani ya Syria.

– Sura ya pili: iliongozwa na Uturuki katika vita vya Ngao ya Furat kaskazini mwa Aleppo mnamo 24/08/2016 na kisha Tawi la Zaituni mnamo 20/01/2018, iliirahisishia serikali kuingia Aleppo na kusini mwa Idlib. Ni kwa sababu makundi haya yaliagizwa na Uturuki na kuacha mapigano na serikali, na kujihusisha na kupigana katika ngao na tawi hilo, Aleppo na kusini mwa Idlib zilipotezwa au karibu na kupotezwa! Kabla ya hapo, Uturuki, ambayo inaendelea mpaka leo chini ya maelekezo kutoka kwa Amerika, katika kucheza dori nyengine mjini Idlib na kuingia eneo hilo kwa vikosi vya upelelezi kuanzia 7/10/2017 na kisha kupeleka majeshi yake na kuunda vituo vya uchunguzi ndani ya makubaliano ya kupunguza joto la kivita pamoja na Urusi na Iran … Baada ya hapo mkutano wa Erdogan pamoja na Raisi Trump ulifanyika mnamo 21/9/2017 jijini New York, Trump alimsifu Erdogan wakati huo kama: “rafiki yangu” (Anadolu, 21/9/2017) na mazungumzo baina yao yaliangazia hali nchini Syria. Trump alikubali Uturuki kuingia Idlib “jeshi la Uturuki limeanza oparesheni ya utafiti katika mkoa wa Syria wa Idlib kwa lengo la kubuni eneo la kupunguza uhasama chini ya makubaliano ya Astana. (Sky News Arabia 09/10/2017). Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Inab bakadi mnamo 13/5/2018, oparesheni ya Uturuki ingali inaendelea, ilisema: “Uturuki imekamilisha hatua zilizoanzishwa mkoani Idlib na inakwenda kwa mielekeo miwili wa kwanza ni utumizi wa vituo vya udhibiti vilivyo kuafikiwa katika makubaliano hayo ili kuhafifisha uhasama katika Astana, na mwengine ni uandaaji muundo wa kijeshi wa makundi yanayofanya kazi yasiyo kuwa na maelewano na makundi ya Kiislamu hadi leo …” Tovuti hiyo iliongeza pia: “Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, vituo vya uchunguzi vya Uturuki vimetumiwa mjini Idlib katika mpaka ulio mashariki mwa Idlib kando na eneo la magharibi, ambayo imeibua maswali kuhusu sababu zilizopelekea kuviweka vituo hivyo upande wa mashariki pekee!” kwa mujibu wa duru, makundi hayo yalipokea usaidizi wa Uturuki mara moja pekee fv…

Licha ya hatua za Uturuki, mashambulizi ya anga ya Urusi yanaendelea, ambayo ndio kadhia chungu katika mandhari ya kila siku mjini Idlib. Kwa mujibu wa wanahabari wa ‘Inab Baladi mjini Idlib na viunga vyake: “mashambulizi ya anga ya Urusi yanalenga eneo la kusini mwa Idlib kwa makombora yenye vilipuzi vikali mno yanayosikika kote Idlib.”

– Ama kuhusu sura ya tatu, Amerika imeiingiza serikali ya Saudi, iliyo shiriki nayo katika muungano wa kimataifa, na kutangaza kwamba iko tayari kutuma majeshi yake ya ardhini hadi Syria kwa ajili ya Amerika na uongozi wake.

Serikali hii ilicheza dori chafu, kama serikali ya Uturuki, kupitia kuyaweka makundi ya kisilaha yaliyotiwa sumu na pesa zake chini ya ushawishi wake na kuyazuia makundi haya kutokana na kwenda katikati ya jiji kuu la Damascus, ingawa ilikuwa karibu na machoni mwao na umbali wa kurusha jiwe tu! Iliyoyafanya kukubali majadiliano na serikali, ikiyafanya makundi hayo kuanguka ndani ya ushawishi wake kupitia ufadhili wake kutoka Riyadh na kukubali kushiriki katika majadiliano hayo na hivyo ndivyo ulivyokuwa mkutano wa Riyadh 1 mnamo 11/12/2015. Taarifa ya Riyadh, na kongamano la Riyadh 2 ilitolewa mnamo 22-24/11/2017; na uliundwa ujumbe wa pamoja ili kujadili pamoja na serikali jijini Geneva na Vienna chini ya uongozi na mipango ya Amerika. Serikali ya Saudi ingali iko tayari kutoa huduma kwa Amerika. Mfalme mtarajiwa wa Saudi Bin Salman alisema baada ya kukutana na bwana zake nchini Amerika, akitangaza kile walicho muagiza kusema katika Jarida la Time mnamo 6/4/2018: “Siamini kuwa Bashar ataondoka bila ya vita, na siamini kuwa kuna yeyote anayetaka kuanzisha vita hivi.”

– Sura ya nne ilikuwa ni majeshi ya Bashar, Iran na Urusi: baada ya kudhaminiwa na Uturuki “kupunguza joto la kivita” katika maeneo makuu, kama majeshi ya sura hii yalipigana vita mjini Palmyra na kufikia Deir al-Zour, yote kwa ushirikiano wa Uturuki na Saudi Arabia na ushawishi wao kwa makundi hayo, waliyapotosha mwelekeo makundi hayo kutokana na kupigana na katili hadi kupigana kwa sura nyengine chini ya kisingizio cha kupigana na ‘ugaidi’. Hivyo basi serikali ikapata pumzi ya afueni na kujikukuta vumbi la kushindwa kwingi ilikokupata wakati wote wa mapinduzi.

Iliibuka yenye nguvu katika raundi zote za majadiliano jijini Geneva pamoja na Astana, ambapo ilikuwa ikizungumza kwa msimamo imara na kujiondoa kutoka katika majadiliano hayo. Makundi hayo yalianza kuziomba nchi kutia shinikizo kwa serikali hiyo kukubali suluhisho la amani, baada ya kuwa yalikuwa ni matakwa ya serikali hiyo kukomesha kuangamizwa kwake!

  1. Kuziweka mbali sura zenye kuvuruga: pamoja na Amerika kuzitenga nchi za Ulaya kutokana na mandhari ya Syria, na kutaka kujibakisha wao na Urusi pekee kimataifa. Ingawa Urusi si umbile huru na Amerika nchini Syria, Amerika imeitumia Urusi kusimama na Bashar kama sura ya majadiliano ya kimataifa kuhusiana na Syria, ili kuzuia uingiliaji kati wa Ulaya. La muhimu pia, Amerika imetafuta kupunguza sura za kieneo zisije kutoka katika michoro, Qatar na Jordan.

Ama kuhusu Qatar, Amerika imezisukuma Saudi Arabia na Misri dhidi ya Qatar na kulazimisha kuisusia katikati mwa 2017 ikiituhumu kufadhili “ugaidi” nchini Syria, na kwa hivyo serikali hiyo nchini Qatar ilijipata chini ya tishio la moja kwa moja kutoka kwa vibaraka wa Amerika, hivyo basi ikakatiza kuingilia mambo nchini Syria, na kumaliza dori yake thabiti. Ama kuhusu Jordan, pamoja na ujasusi wake ilikuwa imeasisi mahusiano imara pamoja na makundi ya kusini mwa Syria, na hili lilikuwa kwa faida ya Uingereza kwa matarajio ya kupata baadhi ya ushawishi kwa Syria … Na kulidhibiti hili, Amerika imeanzisha hatua ya kibinafsi kufungua majadiliano pamoja na Urusi kwa ujanja wa “kupunguza joto la kivita” kusini mwa Syria, na hivyo basi ikaiwezesha serikali kuwa na takriban udhibiti kamili wa kusini na kisha kumaliza ushawishi wa kihakika wa Jordan au kukaribia kufanya hivyo.

Yaani, Amerika inakata matumaini yoyote ya ushirikiano wa makundi haya pamoja nayo ambao utayapa nguvu! Kama ilivyo nukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, inaonekana kwamba baadhi yao yamezinduka kutokana na ujinga wao, na kusema kuwa Amerika imewahadaa! Sasa ndio wametambua?

  1. Tunapoichunguza sera ya Amerika kwa makini na sera ya wafuasi wake, hususan Uturuki na Saudi Arabia, na Misri kwa kiwango kichache kutokana na matatizo ya kindani, tunapata kuwa Amerika inakwenda kwa wakati huo huo katika mipangilio yote iliyochora kwa Syria na iliyotajwa juu, inauwacha mlango wazi kwa juhudi za serikali, Urusi na Iran kuushambulia upinzani kijeshi, na kuondoa matumaini yoyote ndani ya upinzani kuwa Amerika itasimama kuyasaidia. Pindi serikali ilipoanzisha kampeni yake dhidi ya Daraa na eneo la kusini, likiungwa mkono na idara ya anga ya Urusi, Amerika ilituma ujumbe kwa makundi hayo ya Jeshi Huru kupitia ubalozi wake nchini Jordan mnamo 23/6/2018 ikisema: “Tunafahamu kuwa nyinyi ni lazima mufanye uamuzi wenu kwa mujibu wa maslahi yenu na maslahi ya familia zenu na kundi lenu kwa maono yenu, na hamupaswi kujenga uamuzi wenu juu ya dhana au matarajio ya sisi kuingilia kati kijeshi” (‘Inab Baladi website, 23/6/2018). Na maana yake ni kuwa, Amerika inakata matumaini yoyote ya ushirikiano wa makundi haya pamoja nayo kwamba itasimama kuwaokoa! Kana kwamba baadhi yao, kama ilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, wamezinduka kutokana na ujinga wao, na kusema kuwa Amerika imewahadaa! Sasa (ndio wamejua)?

Hivyo basi, Amerika inaifuata vilivyo sera ya kuyamaliza makundi ya kisilaha nchini Syria kupitia serikali, Iran na Urusi, na kwamba hayawi ni vikwazo vyovyote njiani, lakini mbele na nyuma ya hilo, ni mchango halisi wa Uturuki na Saudi Arabia! Usaidizi wa Amerika kwa makundi haya unakomea katika mipaka ya taarifa au pesa zilizolipwa kwa viongozi wake kwa mkabala wa utiifu. Kulikuwa na silaha chache zilizokuja kutoka Amerika na hazikuwa madhubuti kwa maumbile ya ulinzi (yaani hazikuwa za maangamivu), hilo lilifanyika wakati wa nyuma ili kuwakinaisha wanamapinduzi kuwa Amerika iko pamoja nao na inawaunga mkono ili wapate kuwa watiifu kwake. Leo, baada ya kuwa upande wa kijeshi wa Bashar Assad unashinda, mazungumzo yote haya yamemalizika, na taarifa za Amerika kuhusiana na hili zimekwisha; Amerika imefunga faili hili, vile vile wafuasi wake, Uturuki na Saudi Arabia.

  1. Ama kuhusu mwelekeo wa majadiliano ya kisiasa, Amerika imekuwa ikiyaakhirisha hadi mapinduzi hayo yamalizwe na Bashar asimame tena kwa miguu yake. Hivyo basi, ilikuwa ikiwashughulisha wafuasi wake na vibaraka wake kutayarisha suluhisho kwa mazungumzo ya pembeni hadi hali za suluhisho la kisiasa zitakapokomaa na kuchukua wadhifa mkuu.

Hii ndio sababu wakati majadiliano ya kisiasa yalipokuwa yakiendelea yaliyochukua muda wa miaka miwili, vibaraka wa Amerika na wafuasi wao nchini Saudi Arabia na Uturuki walikuwa mbioni katika kupanga mikutano na makongamano ya upinzani wa Syria, na walikuwa wakiangazia viongozi katika mandhari ya kisiasa na kuwaondoa viongozi wengine. Yote haya yanafanyika hadi serikali hiyo itakaposimama tena kwa miguu yake, ndipo Amerika ichukue udhibiti juu ya hali ya kisiasa pamoja na dori ya Urusi au pasi na kuipa dori.

Lakini baada ya mafanikio makubwa ya kijeshi ya Bashar na washirika wake katika mji wa Aleppo, kisha bonde la Barada na Qalmon, kisha mashariki mwa Ghouta na kuondolewa kwa hatari kutoka pambizoni mwa jiji kuu la Damascus, na kisha katika vijiji vya Homs na Hama, na leo mjini Daraa, na pengine baadaye mjini Idlib na vijiji vyenginevyo vya Aleppo. Mafanikio haya makubwa yanaashiria kuwa suluhisho la kisiasa la Amerika linakaribia, lakini imeliakhirisha hadi baada ya Idlib. Inaonekana kana kwamba wanajitayarisha kwa hili, wamekamilisha utekelezaji wa makubaliano ya Fo’a na Zabadani; na makubaliano ya mwisho baina ya Urusi na Uturuki yaliidhinishwa mnamo 17/7/2018 na yanahusisha kuondolewa kwa wakaazi wa miji ya Fo’a na Kafriya walio watiifu kwa serikali katika mkoa wa Idlib waliozingirwa na makundi, ili makundi hayo yasimiliki karata yoyote ya shinikizo, na ili serikali isifedheheke ikiwa italishambulia eneo hilo na kutekeleza mauwaji. Hivyo basi, eneo pekee lililobakia bila ya suluhisho la kisiasa ni Idlib na pamoja nalo ni vijiji vya Aleppo, ambalo ni eneo muhimu lililo na mkusanyiko mkubwa wa wanamapinduzi, lakini Uturuki inaushawishi mkubwa juu ya mengi ya makundi ya kisilaha ndani yake, inatarajiwa kwa Uturuki kuyatia shinikizo kuzikabidhi silaha nzito kwa serikali hiyo na kufanya maridhiano nayo.

Hili ni hatari zaidi kuliko vita vya serikali, Urusi na Iran, ingawa yote ni hatari na yenye madhara … ikiwa nguvu ya kijeshi itaondolewa kutoka katika mapinduzi ya Syria, basi suluhisho la kisiasa la Amerika litakuwa chini ya matayarisho na utekelezaji … inatarajiwa zaidi kwamba Amerika inataka kumbakisha Bashar kwa muda wa “mpito” ambapo ni sehemu ya suluhisho lake la kisiasa, na kuhakikisha kipindi hicho cha umalizaji upinzani, na kisha kumleta kibaraka mithili ya Bashar atakaye endeleza kudumisha ushawishi wake nchini Syria, pamoja na kuweka usalama kwa binti yake umbile la Kiyahudi mvamizi wa Palestina. Umbile hili la Kiyahudi linataka kibaraka nchini Syria mithili ya Bashar ili kulinda usalama wake na asiyerusha hata risasi moja kwake. Netanyahu aliwaambia maripota kabla ya kuondoka Moscow mnamo Alhamisi 12/07/2018: “Sisi hatuna shida na serikali ya Assad (baba na mwana) kwa muda wote wa miaka arubaini, hakuna hata risasi moja iliyorushwa kutoka milima ya Golan. Hatupingi suluhisho la Raisi wa Syria Bashar Assad, bali tutafanya kazi juu ya kulinda mipaka yetu” (Ha’aretz, Julai 12, 2018)

  1. Nguvu za kijeshi za serikali ya Syria ni dhaifu na zisizotosheleza kudhibiti Syria baada ya suluhisho la kisiasa. Jeshi la Bashar limezidi kuwa na uchovu. Licha ya kuendelea kusambaziwa silaha kutoka katika njia tofauti tofauti za Amerika, ima kupitia Urusi, Iran au kwengineko, nguvu kazi imebakia kuwa ndio tatizo lake kubwa. Hivyo basi, inatarajiwa kuwa suluhisho lolote la kisiasa la Amerika ni lazima lijengwe juu ya nguvu itakayolilinda. Amerika huenda akafuata moja ya njia mbili zifuatazo au zote, nazo ni:
  2. Kuendelea kuitegemea Iran, chama chake na wanamgambo wake wengine, wakiwemo Wairani, Waafghani, Wapakistani nk., inayowajibisha kuwapa makao na uraia, ambapo baadhi ya habari zadokeza utekelezwaji wake leo na serikali ya Syria. Mjuzi mmoja alikisia katika shirika la habari la Ujerumani la DW, 30/4/2018, idadi ya wanamgambo hawa kuwa 45 na idadi ya chembe chembe zao kukaribia elfu 40, mjuzi huyo alisema: “Nadhani kuwa wanamgambo hawa watabakia nchini Syria … Tuliona mchakato wa kuwamakinisha katika ukanda wa Damascus. Wanamgambo wa Kishia wako katika kijiji cha Sayeda Zeinab na maeneo mengine … Nadhani kuwa Iran inajaribu, kama ilivyo hali kwa halaiki hiyo ya watu, kupewa kwao uraia au njia nyenginezo za kuwasaidia kubakia eneo hilo.”

Ingawa serikali hiyo inawalazimisha wakaazi wa maeneo inayoyadhibiti kuhudumu katika jeshi, lakini inashaka na utiifu wao jambo linaloipelekea kuwategemea wanamgambo hao waliopigana katika upande wake wakati wa kipindi cha mapinduzi.

  1. Kutegemea majeshi ya kieneo “ili kuweka amani”, na huenda ikavileta vikosi vya Misri, Saudi na Uturuki kwa lengo hili. Hizi si habari mpya; mtandao wa Al Jazeera Net ulinukuu gazeti la Amerika, 8/4/2016: “Gazeti la ‘American Journal’, maslahi ya kitaifa yanaelekeza katika vita ambavyo vimekuwa vikitokota nchini Syria kwa miaka, na kusema kuwa nchi hiyo imetumbukia ndani ya mgogoro unaohitaji vikosi vya kuweka amani, pasi na kutilia maanani ni muundo gani mzozo huo utakaomalizika kwao.” Dhana hii ya Amerika ya suluhusho nchini Syria inayotoa wito wa kusajiliwa kwa vikosi kutoka ng’ambo, licha ya mafanikio ya kijeshi ya Bashar, haijamalizika. Mtandao wa Al Jazeera Net ulinukuu mnamo 17/4/2018:

“Gazeti la Wall Street Journal liliripoti kwamba utawala wa Raisi Donald Trump unapanga kubadilisha vikosi vya Amerika kwa vikosi vya Kiarabu nchini Syria ili kudumisha ustawi katika eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo baada ya ISIS kushindwa.

Gazeti hilo liliripoti kuwa mshauri wa usalama wa taifa wa Amerika John Bolton aliwasiliana na kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Misri Abbas Kamil ili kujua msimamo wa Cairo kuhusiana na hili; liliongeza kuwa mawasiliano hayo yalifanyika pia kwa nchi za Ghuba, ili kushiriki katika majeshi haya na kutoa usaidizi wa kifedha kwayo. Maafisa katika utawala huo wanataraji kwamba nchi za Kiarabu zitajibu ombi hili la Trump, hususan katika usaidizi wa kifedha.)

  1. Hili ndilo linaloashiriwa na ukweli uliojitokeza na unaojitokeza juu ya sera ya Amerika nchini Syria …

Na baada ya kufanya uchambuzi wake, ni wazi kuwa kuendelea kuwepo kwa serikali hiyo na wala sio kwa nini haikuanguka, kimsingi haitokamani na nguvu ya serikali hiyo au nguvu ya Amerika na wafuasi wake Urusi na Iran na wanamgambo wake, wala nguvu ya wafuasi na vibaraka wake Uturuki na Saudi Arabia, ingawa zinao ushawishi, bali sababu kuu ni khiyana au uhadaifu na ushirikiano wa viongozi wengi wa makundi katika kuiamini Amerika, kwamba iko pamoja nao, na kusahau kuwa yeye ni adui wa Uislamu na Waislamu katika matendo yake yote … pamoja na imani yao kwa wafuasi wa Amerika na vibaraka wao Uturuki na Saudi Arabia na kusahau kuwa Aleppo ilisalimishwa kupitia kufungua mpaka wa Ngao ya Furat na kuwaondoa wapiganaji huko, kisha ikaja Tawi la Zaituni iliyo waondoa wapiganaji huko, na kuiacha kusini mwa Idlib kuwa kitoweo rahisi cha Urusi na serikali.

Ama kuhusu Saudi Arabia, makundi yalisahau namna Saudi ilivyo yatayarisha kwa majadiliano na serikali ya katili katika mikutano na majadiliano yanayoitambua serikali hiyo zaidi kuliko kuing’oa. Na sasa Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Arabia amefichua lile lililokuwa limefichika na kuweka wazi kuwa Bashar anabakia … na lililo baya zaidi ni kuwa Urusi inawalipua kwa ukatili huku wao wakijadiliana nayo na kusalimisha silaha zao nzito na wastani! Ni mandhari ya uchungu kuona kuwa Urusi inapokea vifaru vyao na bunduki zao, na wanakaribia kufedheheshwa na kudhalilishwa.

Yote haya ndiyo sababu msingi ya yanayo endelea. Wamedumu kwa miaka mingi katika mapigano na serikali na kuteka maeneo yake, lakini kwa siku chache tu waliiwacha Aleppo kwa kushirikiana na Uturuki. Walitoka eneo la kusini mwa Syria, hususan kutoka Daraa kwa siku chache zaidi, kwa kushirikiana na Saudi Arabia. Katika hali zote hizi, maghala yao ya silaha yalikuwa yamejaa silaha walizoziteka nyara kutoka kwa jeshi la serikali … Hakika inasikitisha kuwa wamevumilia miaka mingi ya ulipuliwaji kwa mabomu, makombora yenye maangamivu na silaha hatari kutoka kwa serikali, Urusi, Iran na wanamgambo wake, lakini wakapeana maeneo yao bila ya vita kwa siku chache, na kuyasalimisha kwa ushirikiano na khiyana, na hata kusalimisha silaha zao nzito na wastani! Na kuacha nyumba zao na kuwa wakimbizi!

Yeyote anayefuatilizia haya ataona kuwa sababu kuu ni uaminifu wa makundi haya kwa maadui wa Uislamu na Waislamu, na uaminifu wao kwa vibaraka na wafuasi, ima viogozi wa makundi hayo walijua hilo au la, ima walidhamiria hili au walifanya kwa makosa, yote haya ni uchungu … mtu anaweza kuuliza, na ana kila haki ya kufanya hivyo, maadamu Hizb ut Tahrir ina kiwango hiki cha utambuzi, maono na ufahamu na inayajua matukio, kwa nini haikuyashauri makundi haya na kuyapa utambuzi ili yasiingie katika makosa haya?

Mimi nasema kwa wale wanaouliza swali hili, kwamba sisi tumesheheni uchovu kwa kuwapa ushauri wetu kwao na kuwaonesha uhalisia wa mambo kwa dalili na uthibitisho … miguu yetu imechoka kwa kutembea kiguu na njia kwao ili kuwashauri na kuwaongoza, kwani baadhi ya njia zakuwafikia wao zilikuwa hazipitiki magari kwa urahisi. Kwa hivyo tulitembea kwa miguu, na kutokana na mawasiliano ya mara kwa mara nao, baadhi ya watu walidhani kuwa sisi ni miongoni mwao!!! Ikiwa mtu atasoma aliyeuliza swali hili atasoma matoleo yetu, na majibu ya maswali, na yako mengi mno, atajua kuwa tumetia juhudi nyingi juu ya jambo hili, zaidi kuliko uwezo wetu, lakini wengi wa viongozi hawa hawakumuitikia au kumuogopa (Allah), walikuwa wakisema, pindi tulipo waonya kuhusu kuchukua pesa chafu walizozichukua kutoka kwa nchi hizi za khiyana: “Tutapata wapi pesa kwengine? Hizb ut Tahrir haitupi pesa.”

Kwa hivyo wakajihalalishia kuchukua pesa kutoka kwa Makafiri na makhaini! Tukiwaambia kuwa mutakuwa mateka wao, wao husema hapana! Kwa hivyo kilicho potea kimepotea, wamebakia vipofu katika ujinga. Tukiwaambia kuwa mutapata silaha nyingi ambazo mutaziteka kutoka kwa serikali, sasa kwa nini basi mujifedheheshe milangoni mwa wale makhaini ili kupata baadhi ya silaha? Wao wanasema, tutapata wapi silaha zetu na Hizb ut Tahrir haitupi silaha? Tukiwaambia kuwa shingo zenu zitakuwa halali yao kwa silaha hizi, wao wanasema, tunachukua kutoka kwa adui na kupigana na adui! Hatimaye wakayaona haya, lakini ilikuwa washachelewa, kuwa walinyimwa silaha hizo walizokuwa na haja nazo sana, na hata kuzisalimisha silaha zao kwa njama za makhaini hao … Kwa hivyo tuliwashauri lakini hawakuwapenda washauri hawa! Kama mfano, nilitaja baadhi ya yale yaliyomo ndani ya toleo letu la mnamo 05/04/2018:

“… Ingawa chama kilitia juhudi kunyanyua utambuzi kwa makundi haya, na kuyaelimisha kuhusu yanayojiri, lakini yalikuwa yakihalalisha kuwafuata watu hao, kwa sababu walikuwa wakiwasaidia wao kwa pesa na silaha, na kwamba Hizb haiwezi kufanya hilo, bali inawasaidia kwa ushauri pekee … wanasema kuwa ushauri pekee hausaidii inapokuja katika vita kivitendo! Hawakutambua kuwa upanga mkononi mwa mwenye kuushika, una makali pande zote mbili, ni katika mkono wa mwenye utambuzi, aliye na maono, ngao inayomlinda kutokana na uovu wa hasimu wake, na mbinu zenye nguvu ya kumshinda adui yake … Lakini mkononi mwa aliyehadaiwa anayekimbia nyuma ya usaidizi wa wahalifu itakuwa ni ngao iliyo chanika, huku nyaya zikipenya katikati yake, na kumuua kila anayeibeba kabla ya kuuliwa na hasimu wake!

Sisi tunayahutubia makundi hayo kuwa kukataa ushauri na utambuzi wetu, na kusema kuwa hausaidii wakati wa vita hivyo, na kwamba wanataka pesa na usaidizi wa silaha, wanaopata kutoka kwa makhaini wa Waislamu, Waarabu, Waturuki na Wafursi. Baadhi yao wakiongezea, hata kwa wahalifu wa Kirusi na wa Kiamerika, wakidhani kuwa kuchukua pesa hizo chafu kutoka kwao, hakutawazuia wao kutokana na kuipigania Ash-Sham … Tunawaambia wote hao: Sasa munajionea natija ya matendo yenu na maneno yenu, mumekuwa wakimbizi, muliofukuzwa majumbani mwenu na hata kwa watoto wenu!

  1. Kwa kutamatisha, tunasema: hakuna hata eneo moja lililosalia isipokuwa Idlib, na pengine Erdogan ana ngao na matawi mengineyo yaliyoipoteza Idlib yatakayoipoteza Idlib na vitongoji vyake, ambayo iko kimya na haionyeshi harakati yoyote … Sisi tunayaambia makundi haya wasidanganywe na hatua za Erdogan na katu wasiisalimisha Idlib kwa serikali … Hawapaswi kuyasahau yale yaliyowatokea Aleppo, na kukumbuka Hadith ya Mtume (saw), iliyosimuliwa na Bukhari kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) kwamba Mtume (saw) amesema:

«لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ»

“Muumini hang’atwi katika tundu moja mara mbili.” Vipi basi ikiwa atang’atwa mara nyingi?

(إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ)

“Hakika katika hilo upo ukumbusho kwa yeyote aliye na moyo au akatega sikio na yeye yupo anashuhudia (kwa kutafakari akili yake)” [Qaf: 37]

Kwa kutamatisha, tunasisitiza yale ambayo tayari tushayasema: dhurufu zitabadilika, na Ummah huu umeathiriwa na hili na majanga mengine makubwa zaidi, mithili ya Makruseda ma Matartari, na hatimaye ukarudia tena izza yake na kuamka, na kuwang’oa na kisha kuuongoza ulimwengu … Ni kweli kuwa utawala wa Kiislamu ulitabikishwa siku hizo.  Na kwamba Khilafah ilikuwepo hata ingawa ilikuwa dhaifu, Ummah ulikuwa na kiongozi aliye uunganisha kupigana na adui yake, kupata haki na kung’oa batili, ulimshinda adui yake na kuinuka tena. Leo hakuna utawala wa Kiislamu, hakuna Khilafah, na ruhusa kutoka kwa yule anaye waunganisha Waislamu kupigana, hili ndilo ambalo laweza kusemwa na mtu, na ambalo ndio wasifu wa kweli wa uhalisia, lakini kazi ya Khilafah inaendelea kwa nguvu, kwa idhini ya Allah, na imekuwa ndio matakwa ya Waislamu katika biladi zao, na wanatamani hili kwa maneno na vitendo, na wanazikabili siku zile nyeusi, 26, 27, 28 za Rajab 1342 H, zilizo husisha khiyana na uhalifu wa kuvunjwa kwa Khilafah, kuziondoa siku hizo nyeusi, na kurudisha tena Khilafah ili ing’are tena katika siku ambayo Allah (swt) ameikidhia. Hili ni rahisi kwa Allah (swt) kulitimiza. Hapo ndipo waovu, wale waliokhini, na madhalimu watakapojua mwisho wao utakuwa upi …

Waislamu hawapaswi kukata tamaa na rehma ya Allah, Ash-Sham itabakia kuwa Ash-Sham, ndio nyumba ya Uislamu: Imesimuliwa na Na’eem Bin Hammad juu ya kadhia ya fitna, kutoka kwa Khatheer Bin Murrah: aliyesema: Mtume (saw) amesema:

«عُقْرُ دَارِ الْإِسْلَامِ بِالشَّامِ» “Kitovu cha nyumba ya Uislamu kiko Ash-Sham.”

Hizb imehakikishiwa tena kwa nusra ya Allah sio tu kwa Manabii na Mitume, bali pia kwa waumini, wakweli, na sio tu kesho Akhera, bali pia hapa duniani.

 (إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ)

“Hakika, Sisi kwa yakini tutawanusuru mitume Wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na Siku watakayosimama mashahidi.” [Ghafir: 51]

Na siku hiyo waumini watafurahi kwa nusra ya Allah, na waovu watadhalilika kwa fedheha na adhabu kali kesho Akhera, na Allah ndiye mlipaji kisasi (Muntaqim), Jabari, Mwenye nguvu (Aziz) na Mwenye hekima (Hakeem).

16 Dhul Qi’dah 1439 H
29/7/2018 M

Inatoka Jarida la Uqab:21  https://hizb.or.tz/2018/10/02/uqab-21/

 

Maoni hayajaruhusiwa.