Watoto Wa Mashariki Ghouta Waangamizwa! Nani Atalinda Damu Zao??!!
Tarehe 22 ya Februari, Shirika la Kutetea Haki za binadamu ndani ya Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza lilitoa taarifa kwamba zaidi ya watu 400 wameuliwa, wakiwemo watoto 150 katika siku 5 za mwanzo za mashambulizi mabaya zaidi yaliofanywa Ghouta Mashariki na majeshi katili ya Syria na Urusi, ambayo yanashambulia kuwalenga makusudi raia katika majumba yao, maduka, mashule, mahospitali na masoko, mashambulizi yaliyowafanya watoto kufunikwa na kifusi cha mawe na matofali ya majengo.
Watoto wamelazimaki kujificha ndani ya mapango, mashimo au sehemu za chini (basement) za majumba yao ‘wakisubiri khatima yao ya kufa’. Madaktari wamelazimika kuwahifadhi watoto wadogo wadogo na wale wanaozaliwa katika mifuko maalum ya joto, kwa kuwa wanakabiliwa na tisho kubwa la kufa kwa baridi kali. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameielezea na kuifananisha hali hiyo kuwa ni “Jehanamu ya duniani “
Zaidi ya hayo, kuna uhaba mkubwa wa chakula, nishati na madawa kutokana na mzingiro mbaya uliowekwa kwa miaka 5 na serikali ya Syria, mzingiro uliopelekea watu kufa kwa kukosa chakula na kuwaathiri zaidi watoto. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban asilimia 12 ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo ulioshtadi.
Hali imekua mbaya kiasi ambacho wamama wanaomba Allah Achukuwe roho za watoto wao ili kuwaondolea machungu, au walau wafe ilhali wakiwa na chchote tumboni kwa sababu kwao kifo wanaona hakiepukiki kutokana na mabomu wanayopigwa.
Tunashuhudia mvua ya mabomu katika vichwa vya watoto wanaokufa kwa njaa Mashariki mwa Ghouta wakikabiliwa na maangamizi. Tunashuhudia misururu baada ya misururu ya watoto waliofunikwa sanda. Tunashuhudia machozi ya wakina mama wa Ghouta Mashariki wakilia na kutapatapa walau kupata tonge ya kuwalisha watoto wao wadogo wanaokufa kwa njaa. Na tunashuhudia maangamizi yasiyomithilika ya ardhi hii tukufu, huku kaka zetu na dada zetu wakichinjwa na kulazimishwa kusalimu amri kwa vita vya ardhini vya wachinjaji wa Assad na wauwaji wake wa halaiki, pengine ni ukatili mkubwa zaidi kuliko hata wa Allepo. Na pamoja na maangamivu hayo, Jumuiya ya Kimataifa, Umoja wa Mataifa ,watawala katika ulimwengu wa Kiislamu wote kwa pamoja wanaangalia tu. Wanajifanya kama hawana habari na umwagaji huo wa damu, na kuendelea kumpa kibali Assad na washirika wake wauaji waovu hawa wa wototo waendelee kuua bila ya kizuizi.
Wameweka pembeni miafaka na maazimio yote ya kimataifa inayodai kulinda maisha ya binadamu, hakutajwi haki za binadamu wala haki za watoto! Kwa hakika, hata unyama kama huu wa wazi umeshindwa kutikisa nyoyo na hisia zao ! na hautoshi kuamsha utambuzi wao !! Kwao mito ya damu inayobubujika kutokana na damu za watoto wa Ghouta ndio bei ya kulipia maslahi yao ya kisiasa katika eneo hili! Kwa hakika inaonekana hakuna mipaka ya unyama wanaohitaji kuushuhudia utakaowafanya kuachana na ubinafsi wa kufikia malengo yao.
Kwa hakika hakuna ushahidi zaidi unaohitajika kutufanya kuwa na walau tembe ya imani kwa serikali zisizo na utu za nchi za kimagharibi, Umoja wa Mataifa, au tawala za Ulimwengu wa Kiislamu kulinda Ummah wa Syria wakati ambapo wamewatelekeza watoto wa Ghouta katika vifo, na huku inayoitwa mipango ya amani, kuingilia kati na maazimio ya kuleta sulhu ambayo kwa yote wameendelea kumpa Assad muda wa kuendelea kujeruhi, kubaka na kuua Waislamu.Tunachoshuhudia katika luninga zetu ni maangamizi ya Mashariki mwa Ghouta, eneo ambalo lilitangazwa kuwa ni Ukanda ya usitishaji mapigano kama ilivyoamuliwa mwaka uliopita kufuatia Mchakato wa Amani wa Astana. Hii ndio sura halisi ya kile kinachoitwa Mpango wa Amani kwa Urusi, Uturuki, Iran na Jumuiya ya kimataifa!!
Kwa munasaba wa ukatili wa kutikisa nyoyo tunaoushuhudia ndani ya Ghouta, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimeanzisha Kampeni ya mtandaoni yenye anuani : “Nani atawanusuru watoto wa Ghouta”?. Ndani ya Kampeni hiyo tutawaomba Umma, hususan wenye nguvu katika majeshi ya Waislamu kwa haraka kurejesha dola ya Khilafah itakayofuata njia ya Utume, kwa sababu ni utawala wa Kiislamu pekee ndio unaojali kikweli utukufu wa maisha ya binadamu, na ndio utakaokuwa ngao ya Waumini itakayondoa kabisa maangamizi haya yanayoendelea yakiwemo pia mauaji ya halaiki na dhulma kwa Waislamu dunia nzima.
وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنْ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيرًا (النساء: 75).
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Allah, na wanaodhulimiwa wanaume, wanawake na watoto wanasema:”ewe Mola wetu tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na utujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na utujaalie wa kutunusuru kutoka kwako “ [TMQ 4: 75].
Dr. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake
Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir
Great information shared.. really enjoyed reading this post thank you author for sharing this post .. appreciated
Nice post. learn something new and challenging on blogs I stumbleupon on a daily basis.<a href="https://www.toolbarqueries.google.co.cr/url?sa=t
Greetings! Very helpful advice in this particular article!-tv kostenlos ohne anmeldung
Definitely what a great blog and instructive posts I definitely will bookmark your site.All the Best! .kathson Bird Carrier Backpack with Mat Portable Bird Travel Carrier with Perch Lightweight Breathable Transparent Outdoor Bird Cage Backpack Kit for Parrot Parakeet Cockatiel Small Birds – Hot Deals
Good article with great ideas! Thank you for this important article. – hey dudes women
Great post Thank you. look forward to the continuation.
Wow, superb blog layout! How long have you been running a blog for?
you made blogging glance easy. The full glance of your
site is excellent, let alone the content! You can see similar here sklep internetowy
Your post brings a sense of serenity, thank you! <a href="https://petitpetit.ru/bitrix/redirect.php?event1=
I was looking at some of your blog posts on this internet
site and I conceive this internet site is really informative!
Continue putting up.Raise blog range
Wonderful blog! Do you have any helpful hints for aspiring writers?
I’m planning to start my own site soon but I’m
a little lost on everything. Would you propose starting with a free
platform like WordPress or go for a paid option? There are so many choices out there that I’m totally overwhelmed ..
Any suggestions? Cheers!
I think this is among the most significant info for me.
And i’m glad reading your article. But should remark on some
general things, The website style is wonderful, the articles is really
excellent : D. Good job, cheers