Wako Wapi Mashupavu wa Vizazi na Mashujaa Katika Uislamu?
Mnamo siku ya ijumaa, mwezi wa 9 tarehe 30, gazeti la uingereza la Guardian na baadhi ya magazeti yaliripoti kwamba mkuu wa zamani ambae anahusika na timu ya mpira ya wanawake Afghanistani amedai kwamba kuna unyanyasaji wa kingono ndani ya Afghanistan, hii ikijumuisha makao makuu ya shirikisho hilo, na katika kambi ya mazoezi iliyopo nchini Jordan mnamo mwezi wa pili mwishoni. Kutokana na madai hayo Ofisi ya jaji mkuu wa Afghanistani imedai kwamba itachunguza madai yote ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kingono ambao umetokea katika shirikisho la mpira wa miguu la Afghanistan (AFF). Khalida Popalzai, mchezaji na mkuu wa zamani wa idara ya soka la wanawake AFF, alisema kwamba yeye na baadhi ya wachezaji wanawake wapo tayari kutoa vielelezo na ushahidi katika ofisi ya jaji mkuu. Wanapicha mnato na video zilizorikodiwa kama ushahidi na tayari ameshaziwasilisha katika “shirikisho la mpira la dunia FIFA” pia aliongeza.(rejea: Radio Azadi)
Kila mmoja, amefahamu kwamba unyanyasaji wa kingono na udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake unazidi kukua katika nyanja zote za kijamii na uhusiano wa binadamu mmoja na mwingine chini ya mwamvuli wa mfumo wa kikafiri uliopo sasa. Muda mwingine chuki na uhasama binafsi kati ya mtu mmoja mmoja, hivyo muda mwingi, hatua zinazochukuliwa na mashirika yasiokua yakiserikali na ajenda zilizotengenezwa na makafiri zimewezesha kufichua mambo hayo mabaya katika jamii ya kiislamu lengo la ufichuzi huo ni kupata rai amma au uungwaji mkono wa maslahi yao. Makafiri wamefanikiwa kupotosha na kuhamisha rai amma katika jamii ya waislamu katika mambo ya msingi na hili ni moja kati ya njia hizo.
Kigezo cha uhasama, na shinikizo la kisiasa katika demokrasia wako wapi mashupavu wa vizazi na mashujaa katika uislamu?
Ukweli ni kwamba ukosefu wa dola ya kiislamu Afghanistan, wanawake wamekua wakiripotiwa mara kwa mara katika janga hilo , udhalilishaji na unyanyasaji, hata hivyo wanawake wenye heshima, utu na wapenda haki wamekua wakionekana kama kitisho kwa waafghan ambao kibla chao ni U.S na NATO walioichukua afghanistan kwa miaka 18, Wanawake na waislamu kwa jumla wamekua wakilengwa na mabalozi ya makafiri na mawakala wao ambao kimkakati wamekua wakiwekwa kupitia mataasisi ya misaada ya kimataifa, mashirika binafsi na taasisi za serikali ya Afghanistan. Hii imepelekea kwamba hakuna mpango wa kimaendeleo ila hadi ufate sera za Marekani na magharibi hata mkutano wa hivi punde uliofanyika Geneva umeweka wazi hilo. Sasa basi, hii ndio Marekani na magharibi ambazo kwa msaada wa serikali na mashirika ya kibinafsi ya Afghanistani yamepelekea hali mbaya kwa wanawake wa kiislamu.
Mashaka yote haya dhidi ya wanawake yanapewa nguvu na misemo maarufu ambayo kiuhalisia ni uongo tu “Haki za wanawake” n.k kama mtu atafanyia tafakari na uchunguzi ajenda zote hizi atagundua kwamba zinakusudia kuondoa thamani ya uislamu katika maisha ya waafghani na kupandikiza fikra za kimagharibi na nidhamu zake katika mabongo ya waafghanistani wakike na wakiume ili waweze kuachana na uislamu wao, watembee uchi katika masoko na huo ndo “uhuru binafsi ” unaopigiwa debe na serikali za kidemokrasia. Wachanganyike na wanaume katika viwanja bila nidhamu na kurahisisha uzinifu, na kufikia mahala wanaume wao washindwe kuwasimamaia na kuwazuia.
Uislamu unamtizama “mwanamke” kama kiumbe mwenye heshima kubwa na mwenye utu ambae kumlinda ni faradhi katka uislamu. Mwanamke ndio mlezi wa mume na familia yote kwa ujumla katika uislamu. Yeye ndio chanzo cha kizazi na mashujaa katika ummah huu. Mwanamke ndio kiumbe wa heshima kubwa ambae anaekamilisha nusu ya maisha ya mwanaume kama Mtume ﷺ alivyoagiza kwamba “ishini na wanawake kwa wema”.
Wamagharibi wamemteka mwanamke kutoka katika asili ya utofauti wake wa kijinsia na kudai kwamba mwanamke na mwanaume wanaweza kutekeleza jukumu moja katika jamii. Hata sasa wamagharibi wanafanya mipango ya ubadilishaji wa jinsia ambayo mikakati hiyo imeleta mashaka na majanga makubwa katika maisha ya kijamii ya mwanadamu, na kanuni za kutengeneza ndio zilizomtoa mwanamke kutoka katika mtu ghali na wathamani kuwa mtu asiekua na thamani kupitia matangazo ya kibiashara, matangazo ya urembo, fasheni, muziki, pati, michezo n.k
Uislamu ndio dini ya Muumba, aliyemuumba kila mwanadamu na ndie aliempa mwanamke heshima yake. Mwanamke katika uislamu anachukuliwa kama mwanamke sio bidhaa, tena ni mtu mwenye heshima sio dhalili, ni mama ambae pepo ipo chini ya miguu yake. Kuwalinda wanawake ni faradhi kwa wanaume, ambayo kwa hakika ni kulinda heshima yao, utu wao na utakasifu wao. Muislamu anatakiwa kuwalinda wanawake hata kama hilo litampelekea katika kifo, na hata akifa huku akimtetea mwanamke atahesabika kafa shahidi. Fikra hii itasaidia kuondoa udhalilifu, umalaya na utovu wa maadilli katika jamii. Vinginevyo matokeo ya kila mwanamke na msichana itakua ni unyama na udhalilishaji katika dunia na akhera.
Oh, dada wa kiislamu! Oh,watu waerevu wa afghanistani! Nyanyukeni na simameni dhidi ya malengo na misemo na mipango ya makafiri wa kikoloni, vibaraka wa serikali ya Afghanistani na taasisi zao kwa kuirejesha dola ya kiislamu ya khilafah amabayo itatabikisha uislamu jumla na kutokomeza mipango yote miovu dhidi ya wanawake, familia na maisha ya kijamii ya waislamu na kuondoa uzinifu na udhalilishaji wote na umalaya katika jamii na hivyo kumridhisha Allah muweza hapa duniani na huko akhera pepo ni kubwa kuliko ukubwa wa mbingu na ardhi.
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi ofisi ya habari ya Hizb ut Tahrir in Wilaya ya Afghanistan
Imetafsiriwa kutoka: https://www.facebook.com/646683775466624/posts/1482896618511998/
Maoni hayajaruhusiwa.