Utawala wa Urusi umemuhukumu Jannat Bespalova miaka mitano Jela!

0

Mnamo tarehe 18 mwezi wa saba , katika mji wa St.Petersburg, mwanamke wa kiislamu Jannat Bespalova alikutwa na hatia kwa kushiriki shughuli za hizb ut tahrir na Bespalova akakiri hilo shitaka dhidi yake na akapinga adhabu hiyo lakini madai yake hayakuzingatiwa.
Jannat akatumia fursa hiyo ya kuwepo kwa vyombo vya habari mahakamani hapo kwa kutoa shukran kwa wale wote waliomsaidia katika kesi yake na akasema “Allah atawalipa yaliyobora zaidi”.
Kwa upande mwingine, tunawashukuru waislamu duniani kote ambao wamemsaidia dada yetu muislamu mwenzetu na wakapinga kukamatwa kwake na wakapinga sera kandamizi za Urusi dhidi ya uislamu.
Mwaka mmoja uliopita, mume wa Jannat, Issa Rahimov, alishikiliwa kwa kosa la kuandaa na kusimamia shughuli za hizb ut tahrir. Na yeye alihukumiwa kwenda jela miaka 12 na kufanya kazi ngumu, na sasa imekua ni zamu ya mke wake kutupwa jela. Haya yote yanaonyesha wazi sura ya Urusi ya sasa ambapo mambo huenda kinyume; wahalifu wanapewa nguvu na kinga ya kutoshtakiwa kisha waislamu wasio na hatia wanatupwa jela kwa sababu wanataka kuishi kwa kufuata maneno ya Allah “la ilaha illa llah” (hakuna Mungu ila Allah pekee)

Allah (swt) anasema:
﴿ﻭَﻣَﺎ ﻧَﻘَﻤُﻮﺍ ﻣِﻨْﻬُﻢْ ﺇِﻟَّﺎ ﺃَﻥْ ﻳُﺆْﻣِﻨُﻮﺍ ﺑِﺎﻟﻠﻪِ ﺍﻟْﻌَﺰِﻳﺰِ ﺍﻟْﺤَﻤِﻴﺪِ﴾
“Na hawajaona wala kukuta baya lolote kwa hao waislamu ila kwa kumuamini kwao Allah Mwenye Kushinda na Mwenye Kuona kila kitu.”
[A-Buruj:8]

Ofisi Kuu ya habari Hizb ut Tahrir

http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/press-re…/russia/15750.html

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.