Ujumbe Maalum Kwa Balozi Wa Pakistani

Jana Jumatatu 20 Agosti, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania Masoud Msellem akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano wa Hizb ut Tahrir Tanzania Kaema Juma, walifanikiwa kufikisha risala na taarifa maalumu kwa Balozi wa Pakistan Tanzania.

Taarifa hiyo iliambatana na taarifa mbili za Hizb ut Tahrir Pakistan kufuatia kunyakuliwa na kutiwa nguvuni na vyombo vya dola vya nchi hiyo wanaharakati wa Kiislamu Ukhty Romana na Ukhty Roshan na mumewe. Wote wakiwa ni walinganizi wa Kiislamu kupitia Hizb ut Tahrir nchini humo. Kwa maelezo zaidi soma ::

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/pakistan/15787.html

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/pakistan/15840.html

Balozi alipokea taarifa na barua hizo, na kuahidi kuzifikisha kunakohusika.

Tunamuomba Allah SW katika masiku haya matukufu Awafariji walinganizi hao na Waislamu wote mashariki na magharibi waliomo katika mikono ya madhalimu.

Amiin

Maoni hayajaruhusiwa.