Tofauti ya Usimamizi wa Raia Kati ya Uislamu na Demokrasia
Leo hii imekua ni jambo la kawaida na lisiloshtusha kusikia katika vyombo vya habari mbali mbali ripoti za taarifa za Vurugu Uadui Uhasama na Mauaji baina ya Waislamu na wasiokua waislamu, jambo lililopelekea kuondoa kabisa mahusiano yaliokuwepo baina ya waislamu na jamii nyengine.
Tunashuhudia wazi wazi maeneo kama ya mashariki ya kati, Cenral Afrika, Lybya, Barani Asia na ukanda wetu wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Kenya namna waislamu wanavyodhulumiwa, machafuko na mauaji kwa misingi ya Udini.
Kwa asilimia mia moja machafuko hayo yanayovishwa guo la udini ni zao la mfumo mchafu wa demokrasia.
Ushahidi wa haya ni pale inapodhihirka waziwazi kwa baadhi ya mambo yanayopelekea magomvi na chuki hizi kati ya waislamu na jamii nyengine moja kwa moja yanatokana na miito ya Democrasia .
Kwa mfano fikra ya uhuru wa maoni ama (rai):
Hapa demokrasia humaanisha ya kwamba mtu binafsi anayo haki ya kubeba rai yoyote na fikra yoyote namna itakavyokua na anao uhuru kamili wa kuisema na kuilingania rai au fikra hio pasi na kizuizi kutoka kwa serikali au mwengine yoyote maadam haijaingilia au kuvunja taratibu za serikali husika kwa hivyo huchukuliwa kuzuia rai au maoni ya mtu ni kuhujumu uhuru wake .
Kwa kupitia muito huu kumepelekea kwa asilimia kubwa kuvunjwa heshma ya Uislamu na waislamu kutukanwa na kuchafuliwa matukufu yake bila kuhofia lolote wafanyaji wa hayo.
Lakuhuzunisha zaidi kwetu nikuona kua serikali za kidemokrasia licha ya kua baadhi ya maeneo watawala wake ni waislamu si kua tu zinakaa kimya bali zinaunga mkono kivitendo vurugu za sampuli hizi na hata kuhimiza mauaji ya waislamu kwa baadhi ya maeneo Ulimwenguni.
Nchi kama Barma, Rhohingya, Central Afrika na Ukanda wa Gaza mauaji haya ya waislamu kutoka jamii isiokua ya kiislamu yalifanyika wazi wazi yakirushwa mubashara huku jamii ziitwazo za kimataifa zikitia Baraka telee kwa kuangalia vyemaa na kuburudika kama filamu ya kuigiza
Pia tunahuzunika zaida pale tunapoona serikali zinazojinasibisha na uislamu kama Iran Saudia Turkyia n.k kutothubutu kuwanusuru waislamu.
Kiujumla tokea demokrasi kuchukua hatam za ulimwengu idadi halisi ya mauaji na umwagaji damu usiokua na hatia haitafutiki na hakuna yeyote aliewahi kuchunguzwa au kutiwa hatiani.
Aidha tumeshuhudia vikosi vinavyoitwa ati ni vya kulinda amani badala ya ulinzi vimekua waangalizi tu, na mara nyengine kushiriki kikamilifu katika hujuma na dhulma dhidi ya waislamu, ikiwemo ubakaji uporaji wa mali na mauwaji.
Tumeshuhudia pia kwa baadhi ya serikali za kidemokrasia viongozi wake kufadhilisha baadhi ya dini kwa kuzitumia kama mgongo wa kufanikisha malengo yao hili mara nyengine huwalazimu kuwalipa fadhila wanadini hao kwa namna ambayo hukuza mizozo na kuchochea hasama baina ya wanadini wanaoishi chini ya vivuli vya serikali hizo ilhali kiuhalisia serikali hizo zikiwa hazitambui wala kuamini dini yoyote.
Kwa mfano Tanzania tumekua tukishuhudia baadhi ya viongozi wa serikali wakinadi baadhi ya misimamo katika maeneo ya dini, kama tulivyoona kwa Waziri willium Lukuvi kutoa baadhi ya misimamo kanisani na waislamu kuja juu kwa uwelewa wa kwamba Serikali inaendeshwa na kanisa ama ukristo, ilhali ukiristo hauna hata taratibu za kwenda haja ndogo seuze kuendesha serikali. Na kutokana na ufahamu kama huu waislamu walienda mbali mpaka kufikia kuzaa kauli mbiu ya mfumo kristo jambo lililopalilia hasira za kidini kwa madhehebu yote ya kikiristo Tanzania huku maslahi ya wimbo huu yakiineemesha demokrasia .
Mfano mwengine ni pale mwaka 2010 katika kuelekea kampeni za uchaguzi chama cha mapinduzi CCM kilitumia turufu ya ahadi hewa kwa waislamu kuwadanganya kuwapatia Mahakama ya Kadhi kwa lengo la kuwavuta wengi zaidi
Hisia hii ilisisimua kanisa na kulifanya lisimame kidete mpaka kufikia kutoa waraka maalum (Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusiana na Muswada wa Mahakama ya Kadhi) kuhakikisha wimbo huu unapotelea angani Na hatimae bunge likatamka rasmi kutosomwa kabisaa bungeni kwa muswaada wa mahakama ya kadhi. Mwananchi 01/04/2015 .Hili nalo lilipalilia makaa ya chuki baina ya waislamu na wakristo Tanzania.
Tukirudi nyuma kabla ya demokrasia na ujamaa uliotokana nao Ukomunist.
Uislamu umewahi kushika Khatamu za uongozi na kuiongoza Dunia karne kwa makarne
Katika kipindi chote uislamu uliposimama hakukuwahi kutokea mizozo magonvi na chuki zilizopelekea umwagikaji ovyo wa damu kwa jamii isiokua ya waislamu
Ukiachilia mbali vita vya msalaba ambavyo vilisukumwa na wamagharibi.
Chini ya Dola ya Khilafah waasiokua waislamu (kwa maana ya makafiri) serikali huamiliana nao juu ya vigawanyo vinne vikuu:
Kafiri Harbiy:
Huyu ni kafiri ambaye yuko vitani kivitendo dhidi ya Uislamu, Waislamu au Dola yake Hukmu ya kafiri huyu ni kifo moja kwa moja. kama alivosema Allah (sw)
Na piganeni katika njia ya Allah na Wale wanaokupigeni……(TMQ 2:190).
Kafiri Musta Ajir
Huyu ni kafiri ambae amekimbilia dola ya khilafah ili apatiwe hifadhi
Hukmu yake huyu ni kulindwa kuhifadhiwa na ni haramu kusalitiwa kwa adui yake atapewa da’awa akisilimu sawa akikataa atakua raia na atalipa jizya na akikaidi atapelekwa sehemu yeyote yenye amani kwake. Asema Allah SW
“Na kama mmoja wa washirikina akikuomba umlinde basi mlinde”(TMQ9:6).
Kafiri Musta Amin
Huyu ni kafiri ambae amefanya mkataba wa amani na serikali ya kiislamu mkataba ambao hautozidi miaka kumi. Hukmu yake ni kwa mujibu utakavokubalika mkataba akikhalifu ahadi ni Jihad kusimamishwa dhidi yake.(60:8)
Kafiri Dhimmiy
Huyu ni kafiri aliyekubali kuishi ndani ya Dola ya Khilafah na anaitii Dola na analipa Jizya nae hulindwa huhifadhiwa mali yake na hukingwa damu yake pia hupewa haki ya kuabudu kwa dini yake chini ya usimamizi wa Dola pia hupata haki ya kufunga ndoa kwa mujibu wa imani yake. (9:29)
Licha ya kuwekewa vigawanyo wasiokua waislamu vigawanyo ambavyo huondoa kabisa mizozo baina yao na Waislamu pia serikali ya Kiislamu ilizijengea misingi Thabiti huduma za kijamii na kuzitoa bure bila ya malipo yoyote na bila kujali dini rangi wala kabila.
Uadilifu mkubwa ulioneshwa na Uislamu katika kuamiliana na Wasiokua Waislamu badala ya kujenga chuki na Waislamu walikimbilia miji iliokua inatawaliwa na Uislamu bali pia wakati mwengine walikua tayari kuikingia kifua dola ya kiislamu pale walipoona jaribio la kuvamiwa
Kama ilivotokea kwa wakirsto wa jamii ya Qibti nchini Misri zama za himaya ya kiroma ya (Byzantium Empire /Eastern Roman Empire) ilipojaribu kutaka kuvamia ukanda wa misri ambao ulikua chini ya khilafah kwa kutaka kuwatumia wakristo hao wakibti (Coptic Christians) wakristo hawa walikataa kwa kuwajibu waroma …Uadilifu tunaoupata chini ya khilafah hatuwezi kuupata sehemu nyengine yeyote kwa msingi huo hatuwezi kushiriki katika kuipindua khilafah…. https://www.history.com/topics/ancient-middle-east/byzantine-empire.
Vituo mbali mbali vya elimu vya waislamu vilishamiri katika miji mbali mbali na watu kutoka pande mbali mbali za ulimwengu walifurika kuja kujisomea
Kukazalikana magwiji wa fanni mbali mbali wengine hata wasiokua waislamu kama SALEM BIN BAZ aliyebobea katika fani ya Fiqhi ya kiislamu ilhali hakuwa muislamu
Uadilifu mkubwa wa uislamu pia uliwajenga imani na mapenzi makubwa hata raia walikua nje ya mipaka ya khilafah mpaka wengine kufikia kuomba msaada kwa serikali ya kiislamu iwatoe kwenye makucha ya tawala za dhulma mateso na uonevu
Mfano mzuri ni wakaazi wa Hispania ya zamani (Andalucia) walituma ujumbe kuiomba khilafah iwakombowe kutoka kwenye dhulma ya mfalme Roderic aliyekua akiwanyanyasa kupindukia
Khilafah iliitikia wito huu na kumtuma Jemedari Tariq Bin Ziad kuwakomboa na hatimae ikafunguliwa spain ndani ya mwaka 708 au 711 miladia (http://www.khilafah.com/a-visit-to-al-andalus/) na hatimae maelfu kwa maelfu ya wa andalucia wakaingia katika uislamu.
Mwisho ni jukumu letu sasa kuudhihirishia ummah ya kwamba uislamu umekuja na nidhamu kamili ya Maisha ikijumuisha Siasa, Uchumi, Elimu na miamalati yote iliyojengwa chini ya misingi thabiti inayoweza kudhamini maisha bora kwa kila binaadamu kuondoa kabisa chuki, uadui uhasama baina ya watu na kuziba mianya yote ya ukandamizaji inayodhaminiwa na demokrasia na kubwa zaidi kuwadhamini rai kupata radhi za Allah SW kwa watakaoamini itikadi yake na kujifunga kutekeleza kivitendo bila khiana maamrisho yake
Maoni hayajaruhusiwa.