Tofauti ya Rai za Kifiqhi Kwa Mfano Kuthubutu Kuanza kwa Kufunga Ramadhan

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir “Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa “Kifiqhi”

Jibu la Swali

 Tofauti ya Rai za Kifiqhi

Kwa Mfano Kuthubutu Kuanza kwa Kufunga Ramadhan

Kwa Asadullah Al Qurashi

(Limetafsiriwa)

Swali:

Assalam Aleykum wa Rahmatullah wa Barakatuh

Swali kwa Emir wetu na Sheikh wetu, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, Sheikh Ataa bin Khalil Abu Al-Rashta, Mungu amhifadhi, na aujaaliye ushindi wa Uislamu na utukufu wake mikononi mwake na mikononi mwa kundi la waumini miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut-Tahrir pamoja naye.

Sheikh wetu mkubwa, nina swali juu ya rai za kifiqhi za maimamu wanne na mujtahidi wengine ambao wanatofautiana na sisi kuhusu rai za kifiqhi zilizo tabanniwa katika Hizb, na ambazo zinaingia katika ile inayoitwa fiqhi ya ikhtilaf. Mfano: Kuthubutu mfungo wa Ramadhan kupitia hesabu ya falaki, na ambayo baadhi ya mafuqaha (wanachouni wa fiqh) wa zamani, kama Ibn Sarij al-Shafi’i na wengineo miongoni mwa mafuqaha, kama Sheikh Ahmed Shaker al-Masri na Sheikh Mustafa al-Zarqa al-Halabi al-Hanafi, walisema kwa kina rai yake kwa vile ninavyo dhani mimi. Swali ni: Je! Tutaamiliana vipi na rai hizi zinazo tofautiana na zile tulizozitabanni katika Hizb, haswa ikiwa ni za maimamu mujtahidina wakubwa? Kwa mfano, je! Tukubali suala la kuthubutu kufunga kwa njia ya hesabu ya falaki, kwamba katika suala hili kuna rai mbili na kwamba rai ya wengi ni kwamba inaruhusiwa na sio lazima, na tukubali kauli ya yule mwenye kusema “Usinilazimishe katika suala ambalo kuna ikhtilafu baina ya wanachuoni wa fiqh; rai yoyote ninayoifuata mimi kati ya hizo ni sawa”?

Kusudi la swali hili ni kutilia nguvu ufahamu wangu wa fiqhi ya ikhtilaf, na ni wakati gani rai ya pili inakuwa na nguvu, kwa mfano, na ni wakati gani rai ya pili inakuwa ni yenye kukataliwa na kupaswa kupigwa vita, na ni wakati gani, kwa mfano, rai ya pili inakubali ikhtilafu hata kama ni yenye nguvu kwa mtazamo wetu? Kwa mfano: Je! Kuna tofauti gani kati ya suala la kuthubutu kufunga Ramadhan kwa hesabu ya falaki katika upande wa kukubali rai ya nyengine na baina mfano uchi wa mwanamke kuhusiana na mwanamume yenye kuhitilafiana na rai ya Hizb ambayo inasema kuwa uso na mikono ni uchi ?

Naomba radhi kwa kurefusha. Lakini natarajia ufafanuzi wa ni kwa nini mtazamo ume tofautiana, kwa kweli kwa mtazamo wangu, “na naomba radhi ikiwa nimekosea”? Je! Sababu ni ukaribu na umbali wa hukmu hizi kutoka kwa umoja wa Khilafah na kuungananisha mtazamo kwake, au ni kitu kingine?

Mwenyezi Mungu awalipe kheri, Wassalamu aleykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Jibu:

Wa aleykum Salaam wa Rahmatullah wa Barakatuh,

Mwenyezi Mungu akubariki kwa dua yako nzuri kwetu nasi tunakurudishia dua ya kheri na baraka…

Hakika hukmu ambayo imevuliwa kutokana na dalili za kisheria kupitia ijtihad sahihi ya kisheria ni hukmu ya kisheria katika haki ya mmiliki wake, na ni rai ya Kiislamu hata ikiwa inatofautiana na rai tunayoisema na rai tunayoitabanni, haswa ikiwa rai hii ni rai ya mujtahid miongoni mwa maimamu wa madhehebu mashuhuri kwa elimu na ucha Mungu, kama vile ijtihad za maimamu wa madhehebu manne na mujtahidina wa madhehebu hayo … Na tumebainisha jinsi ya kuamiliana na rai za kifiqhi ambazo zinatofautiana na rai za kifiqhi tulizozitabanni katika zaidi ya kitabu kimoja miongoni mwa vitabu vya thaqafa ya Hizb, na nakunukulia kutoka katika sehemu mbili yale ambayo yatafaa kuwa ni jibu la swali lako, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu:

1- Katika kitabu cha “Mafahim ya Hizb ut-Tahrir” yamekuja yafuatayo: [Na kuamini Uislamu ni kando na kuzifahamu hukmu na sheria zake, kwa sababu kuuamini kumethubutu kupitia njia ya kiakili, au kwa njia ambayo asili yake imethubutu kiakili, na kwa hivyo hakuna nafasi ya shaka kwa hilo. Ama kuhusu kuelewa hukmu zake, haimalizikii na akili peke yake, bali inategemea ujuzi wa lugha ya Kiarabu na uwepo wa uwezo wa kufanya uvuaji, na maarifa ya hadith sahihi kutoka kwa dhaifu. Kwa hivyo, wabebaji wa da’wah wanapaswa kuuchukulia uelewa wao wa hukmu kama uelewa sahihi unaoweza kuwa na makosa, na wauchukulie uelewa wa wengine kuwa ni wa makosa unaoweza kuwa sawa, ili waweze kuulingania Uislamu na hukmu zake kulingana na uelewa wao na uvuaji wao kwake, na kuhamisha uelewa wa wengine ambao wanauchukulia kuwa wa makosa na wenye uwezekano wa kuwa sawa hadi katika uelewa wao ambao wanauchukulia kuwa sahihi wenye uwezekano wa kuwa na makosa. Kwa hivyo, sio sahihi kwa walinganizi wa da’wah kusema kuhusu uelewa wao, kwamba hii ndio rai ya Uislamu. Badala yake, wanapaswa kusema kuhusu rai yao, kwamba hii ni rai ya Kiislamu. Watu wa madhehenu miongoni mwa mujtahidina wanauchukulia uvuaji wao wa hukmu kuwa sahihi na wenye uwezekano wa kuwa na makosa. Na kila mmoja wao anasema: “Pindi inapo swihi hadith basi ndio madhehebu yangu, kisha yapigeni maneno yangu ukutani”. Vivyo hivyo, wabebaji da’wah wanapaswa wazingatie rai zao wanazozitabanni, au wanazozifikia kutoka katika Uislamu, kwa kuzingatia uelewa wao, kuwa ni rai sahihi zenye uwezo wa kuwa na makosa.] Mwisho.

2- Na imekuja katika kjiitabu cha Kuingia kwa Jamii yafuatayo: [… Ama kwa upande wa kuingia, inapaswa kutoruhusiwa isipokuwa kuingia kwa Uislamu peke yake, bila kasoro zote, kwani makafiri, watawala na wanasiasa watajaribu kuingiza fikra zisizokuwa za Kiislamu kwa jamii chini ya jina la Uislamu, ili waweze kutia shaka katika jamii kwa upande wa Uislamu, kwa hivyo Waislamu lazima wawe juu ya utambuzi kamili katika upande huu. Kwa hivyo washambulie fikra yoyote inayo halifiana na Uislamu kama ambavyo wanapaswa kushambulia fikra yoyote ya ukafiri, kwa sababu ni ukafiri ulio wazi.

Isipokuwa, kwamba shambulizi hili liko tu kwa fikra za kisiasa au za kisheria, yaani juu ya fikra zinazohusiana na mahusiano ya jamii ambayo yanajadiliwa katika maswala ya dola wakati fikra inapotolewa au wakati utafiti unapofanywa. Na mfano wa hilo, ni marufuku ya kuoa wake wengi, kuhalalisha vyama vya misaada, ushiriki katika wizara, kujikaribisha kati ya watawala wa dola zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu katika kulinda kubakia kwa kila mtawala kama alivyo, Chuo Kikuu cha Kiislamu, kuinua kiwango cha maisha, kuingiza pesa za kigeni katika nchi, na kadhalika. Hizi zote ni fikra zisizo za Kiislamu ambazo huja kwa kisingizio kwamba ni za Kiislamu, au kwamba hazipingani na Uislamu. Hizi lazima zishambuliwe na kupigwa vita na zisiweze kuingia katika jamii ili kusitokee tashwishi ndani yake. Ama fikra za Kiislamu ambazo zinatofautiana na kile ilicho tabanni Hizb, hubainishwa makosa ya uelewa kwake, lakini hazishambuliwi, badala yake huwekwa wazi kuwa ni rai ya Kiislamu, lakini dalili yake ni dhaifu. Kwa mfano, miongoni mwa mujtahidina ni wale wasioruhusu khalifa isipokuwa Mquraishi pekee au kutoka kwa familia ya Mtume (aali bait), na wengine wao wanaona kuwa haikubaliki kwa mwanamke kuwa qadhi, na wengine wao wanaona kuwa inaruhusiwa kulimbikiza dhahabu na fedha ikiwa zaka yake inalipwa, na wengine wanaona kuwa inaruhusiwa kukodisha ardhi kwa ajili ya kilimo, na kadhalika. Rai hizi zote ni rai za Kiislamu na hazizuiwi kuingia katika jamii kwa sababu hakutokei ndani yake tashwishi kwa sababu ni za Uislamu kama rai zilizotabanniwa na Hizb, zinatokana na dalili au dalili madhaniwa. Inatosheleza kuhusiana na fikra hizi za Kiislamu, kuelezea tu makosa yake.

Isipokuwa kwamba Hizb katika magazeti yake, taarifa zake na majadiliano yake kamwe haibebi rai yoyote inayo tofautiana na yale iliyoyatabanni, lakini inaruhusiwa kusambaza rai ambazo haijazitabanni kama mifano ya ufahamu wa kifiqhi au wa kisheria, bila ya kunasibishwa na wale walioitoa, bali inatosheleza dalili yake. Hii ni kwa upande wa rai ambazo Hizb inazisambaza, ama inaposambazwa rai ya Kiislamu, kwa njia isiyokuwa ya Hizb, na ikawa rai hii inagongana na rai ya Hizb, basi inatosheleza kuijadili ikiwa kuna haja ya kuijadili, vinginevyo itapuuzwa. Katika haya yote, Hizb inazunguka kati ya jamii na tashwishi ambayo inaogopa isitokee ndani yake. Vita vitaendelea kati ya Uislamu na ukafiri hadi ukafiri utakaposhindwa na Uislamu ushinde.] Mwisho.

Ni wazi kutokana na kile kilichonukuliwa hapo juu kwamba Hizb haikatai kwa wengine kauli ya rai za kifiqhi ambazo zinatofautiana na yale iliyoyatabanni maadamu zimevuliwa kwa ijtihad sahihi ya kisheria, na ikiwa jambo liko hivi basi hailikatai kwao, lakini badala yake inajadiliana nao na kujaribu kuwakinaisha juu ya makosa ya rai zao na usahihi wa rai zake kwa msingi wa dalili, wala haizipigi vita rai zao wala haizishambulii, lakini inatosheka na kuelezea makosa ndani yake, na inaruhusu kuwepo kwake katika jamii kwa sababu ni rai za Kiislamu hata kama zina dosari na udhaifu katika dalili kwa upande wa Hizb…

– Na katika mifano ya hilo ni kauli kwamba uso wa mwanamke na mikono ni uchi, ni rai ya kifiqhi ya Kiislamu ambayo baadhi ya wanachuoni wa kifiqhi na mujtahidina wameizungumza, na hatuwapingi wale wanaoisema, lakini tunawaita kwenye rai yetu isemayo kwamba uso wa mwanamke na mikono sio ‘awrah, na tunawabainisha kwa dalili za Kisheria usahihi wa rai yetu, lakini hatuzishambulii rai zao hizi, wala hatuwapingi wafuasi wake kwa sababu ni rai za Kiislamu zilizosemwa na wanachuoni wa kifiqhi ambao ni mujtahidina…

– Ama kauli ya hesabu za falaki, ina kauli nyingi kwa mujibu wa wale wanaoisema … Miongoni mwao wanaona kuwa mwezi mwandamo ikiwa utachomoza usiku, basi usiku huo ni wa kwanza wa Ramadhan … na wengine wao wanasema kwamba ikiwa mwezi mwandamo utachomoza wakati wa mchana na kupotea baada ya kutua kwa jua bila kujali muda wa kupotea, usiku huu ni wa Ramadhan … na wengine wao hujaribu kupatanisha kati ya hesabu na kuonekana, na kusema kwamba ikiwa utachomoza wakati wa mchana na kupotea baada ya jua kuchwa kwa kipindi ambacho inawezekana kuuona, basi usiku huo utakuwa ni wa kwanza wa Ramadhan … kisha wanatofautiana katika kiwango cha muda huu, je ni dakika 10, 15 au 20, na kadhalika … na mimi siegemei mwelekeo wa kuwa hii ni ijtihad sahihi. Maandiko yako wazi yakiunganisha kufunga na kufungua saumu kwa kuonekana,

صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ

“Fungeni kuonekana kwake, na fungueni kwa kuonekana kwake.”

Imepokewa na Muslim, kwa hivyo vipi wanageuza hili kwenda kwenye hesabu? Haswa Mtume (saw) Haswa kwa kuwa Mtume (saw) alijaaliya ukosefu wa kuonekana kwa sababu ya mawingu kwa mfano, hata ikiwa mwezi mwandamo uko nyuma ya mawingu, lakini mawingu yanauficha usionekane. Alijaaliya ukosefu wa kuonekana katika hali hii kuwajibisha kukamilisha Shaaban siku 30 hata kama mwezi mwandamo ulikuwa nyuma ya mawingu lakini haukuonekana.

فَإِنْ غُمِّيَ عَلَيْكُمُ الشَّهْرُ فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ

“Ikiwa kwenu mwezi utazibwa na mawingu, basi hesabuni thalathini” Imepokewa na Muslim, na yote haya yanathibitisha kuwa sababu ya kufunga na kufungua ni muonekano na sio sababu nyingine yoyote. Kwa hivyo, katika nafsi yangu nina kitu kwamba hesabu ya falaki haikuvuliwa kwa ijtihadi sahihi ya kisheria … Sisi tumetabanni muonekano wa kisheria kwa sababu umejengwa juu ya ijtihad sahihi ya kisheria kwa mujibu wa misingi sahihi ya kisheria, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

– Kwa kumalizia, sisi hatushambulii rai yoyote ya Kiislamu iliyosemwa na mujtahidina waheshimika maadamu imevuliwa kutoka kwa Uislamu kwa ijtihad ya kisheria, lakini badala yake tunajadiliana nao kwa uzuri kwa kuwa rai yetu ndio sahihi na tunazitaja dalili na kusikia kutoka wao … Lakini tunasimama kidete mbele ya wale wanaotaka kuingiza rai yasizo za Kiislamu na kupotosha watu kwazo ambazo ziko mbali na Uislamu umbali wa Mashariki mbili! Rai hizi sio sahihi katika kuelezea uongo wao, kama vile kusema kwamba faida za riba zinaruhusiwa, na kusema kwamba inaruhusiwa kushiriki katika nidhamu za kikafiri na kutawala kwa yasiyo kuwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, mpaka hali hiyo imewafikisha kusema kwamba maridhiano (amani) na Mayahudi na kusawazisha mahusiano na umbile hilo lao inaruhusiwa ﴾أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿ Tazama uovu wa wanavyohukumu!” na mfano wa hizo katika rai ambazo zimeenea katika zama zetu na ambazo hazikuvuliwa uvuaji sahihi wa kisheria. Badala yake, baadhi yake zinapingana na dalili za kukatikiwa kutoka kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume (saw), kwa hivyo mfano wa rai kama hizi hazizingatiwi kuwa ni hukmu za kisheria wala kuwa ni rai za Kiislamu, na hupingwa wale wanaozisema na kuzibeba, na kuzipiga vita na kuzuiwa uwepo wake …

Nataraji kuwa hii imetolesheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi Mwingi wa Hekima.

Ndugu yenu,

Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

25 Shaaban 1442 H

Sawia na 07/04/2021 M

Maoni hayajaruhusiwa.