Tamasha la Muziki Jeddah: Mbinu ya Kuvuruga Jamii

بسم الله الرحمن الرحيم

Kesho tarehe 18/07/2019 Ufalme wa Saudia utaendelea na uovu wake kwa kufanyika Tamasha kubwa la Muziki la Msimu wa Kiangazi (Jeddah World Fest Summer Music Festival ) ndani ya jiji la Jeddah katika ardhi ya Hijaz aliyozaliwa Mtume SAAW ambayo wameipachika jina la familia yao la Saudi Arabia.

Awali katika tamasha hili alitarajiwa pia kuwepo mwanamuziki maarufu wa Marekani, aliyepindukia katika maasia Nicki Minaj, kabla ya kuukataa mwaliko huo kwa msimamo wake kuwa ushiriki wake katika tamasha la Saudia atakuwa hajawatendea vyema watu wa mapenzi ya jinsia moja, kwani serikali ya Saudia haijawaruhusu vya kutosha watu wa aina hiyo nchini humo.

Licha ya kutoshiriki Nick Minaj, bado tamasha limepangwa kuendelea kama kawaida likipigiwa debe kitaifa na kimataifa. Kiasi cha upatikanaji wa viza ya kwenda katika tamasha hilo kuwa mwepesi kupita kiasi hata kuliko viza ya kwenda Hijja au Umra. Hii inaonesha darja ya uovu kwa jina la mabadiliko ambayo utawala wa Saudi chini ya Muhammad bin Salman unaufanya. Mabadiliko yanayolenga kwa Waislamu wa Hijaz na Uislamu kiujumla, hususan ikizingatiwa nafasi ya ardhi ya Hijaz (Saudia) na fungamano lake kwa dini ya Uislamu. Ni mabadiliko ya kuuondoa Ummah kwenye hisia za Kiislamu, kuongeza ufisadi na kuupoteza katika kiza totoro cha maasia.

Kimsingi, lau watawala hawa wana mazingatio walikuwa watanabahi juu ya hatua ya mwanamuziki huyu wa Marekani kususia Tamasha hili kwa ajili tu ya kuhifadhi, kulinda na kutetea misimamo ya mfumo wao. Wao watawala hawa ambao wapo katika eneo alilozaliwa Mtume SAAW na masahaba wakubwa ni misimamo ipi ya Kiislamu wanayoilinda kiasi cha kuwasusia wengine hususan makafiri wanapoipinga na kuudhalilisha Uislamu ? Lakini wapi !!! katika maradhi ya ajabu yanayowakabili vibaraka katika nchi za Waislamu ni upofu wa nyoyo, hawazindukani amma wakishakupinduliwa au wakiwa makaburini.

Tangu Muhammad bin Salman kushikilia hatamu za kuwa mrithi wa mfalme (Crown Prince) amekuwa akijimakinisha zaidi na kujipambanua ati ni mwanamageuzi wa kijamii na kiuchumi anaelenga kuibadilisha Saudia. Mageuzi ya kuongeza ufisidifu juu ya ufisidifu katika nchi takatifu. Japo Ukweli utabakia kuwa hata kabla ya kushika kwake hatamu hizo utawala wao wa kifamilia ( Ufalme wa Saudia) umeizamisha biladi hiyo katika dimbwi la uovu, lakini ujio wa Muhammad Bin Salman umekuja kuongeza zaidi na zaidi !!

Mohammed bin Salman ambae ameshikilia hatamu hizo kama mfalme mtarajiwa mnamo mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 31 , amechukua hatua mbalimbali ili kufikia malengo ya kulinda cheo chake na kuwafurahisha mabwana zake hususan Marekani kwa kujaza ufisadi na uovu ndani ya Saudia, kukuza chuki baina ya majirani, kumwaga damu ndani ya Yemen, bila ya kutaja kueneza uovu na ili kuitikisa nidhamu ya kijamii iliyobakia katika mafundisho ya Uislamu wanayoshikilia Waislamu wa Saudia.

Katika kanuni na Sheria ya Kifalme ya mwezi Juni 2017, Muhammad Salman alianzisha ajenda ya kupambana na wapinzani wake ikiwemo kuwashikilia masheikh na wanavyuoni mashuhuri, jambo hilo limekuwa endelevu kwa sasa.

Miongoni mwa kile Muhammad bin Salman anachokiita mageuzi kwa jina la ‘Uoni wa 2030’ (Vision 2030) ni kufungua masinema na kuruhusu michanganyiko ya wanawake na wanaume katika matamasha ya miziki. Tamasha la sasa ni matokeo ya mageuzi hayo.

Imekuwa wazi zaidi sasa kufurutu ada kwa kiwango cha uasi cha watawala hawa waliopindukia uovu katika ardhi tukufu. Hata zile hukmu chache za Kiislamu zilizokuwa wanazifanya kuwa ati ni dola ya Kiislamu sasa wamezitupilia mbali !!!

Hapana shaka kutokana na ghera kubwa ya watawala hawa ya kujikomba na kujipendekeza kwa makafiri, mfumo wao na fikra zao za ‘uhuru’ inawezekana sana kuwa baada ya shinikizo la mwanamuziki Nick Minaj kukataa kushiriki tamasha lao, madhalimu hawa upo uwezekano wa watakubaliana na makafiri kwa kurasimisha mapenzi ya jinsia moja na maasia mengine ili kuepuka kile kinachoonekana kwao kuwa ni fedheha.

Wakati watawala hawa wakieneza ufuska huo wanadai kuwa matamasha hayo yatakuza utalii na kuongeza mapato. Ikumbukwe kuwa Saudia ina rasilimali kubwa ya mafuta ya Ummah ambayo familia ya Al-Saudi inaivuruga kibinafsi, kufuja katika ufuska, kumwaga damu za Waislamu ndani ya Yemen na kuwapatia makafiri hususan Marekani, hatimaye inatemegea vyanzo duni vya kidhalili na fedheha vya mapato.

Kwa hali hii ya kuruka mipaka kwa watawala hawa, tena katika ardhi tukufu ni wakati sasa wanachuoni ndani ya Saudia na ulimwenmgu mzima wa Kiislamu kuachana na ajenda za masuala ya mitagaa / matawi katika Ummah, bali ni kusimama kidete kutetea Uislamu na kuinusuru biladi aliyozaliwa kipenzi chetu Mtume SAAW. Lau wanachuoni mukhlis, wanafikra na Umma jumla tutasimama kidete kuihami dini hii na ardhi zetu tukufu basi yasingejiri kama haya yanayojiri, au walau tutaondoa dhima mbele ya Mola wetu mtukufu.

Ummah wetu leo unachohitaji ni utawala wa Kiislamu wa Khilafah na sio uvundo wa vibaraka hawa ambao hawafai kwa chambo wala kiteweo, hawana haya wala vibaya wananajisi hata maeneo matukufu.

Tunamuomba Allah Taala azuiye vitimbwi vya vibaraka hawa na awapatilize kabla ya kufikia malengo yao ya ufisadi ya kuharibu Uislamu.

وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ (الأنفال: 30).

‘Na wanapanga vitimbwi vyao, Na Mwenyezi Mungu anapangua, Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa kupangua’ (TMQ 8: 30)

Risala ya Wiki No. 48

14 Dhu al-Qi’dah 11440 Hijri /17 Julai 2019 Miladi

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

https://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.