Takhreej (Upokezi na Usahihishaji) wa Hadith “Pokea Zawadi maadamu ni Zawadi”
بسم الله الرحمن الرحيم
Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, Tunamuomba Mwenyezi Mungu kuturuzuku afya na mafanikio katika kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na aulete ushindi na tamkini na izza ya Dini kupitia mikononi mwako
Tafadhali waweza kutoa upokezi na usahihishaji wa Hadith hii katika upande wa usahihi, nguvu, udhaifu, na kuitumia kwake kama dalili, shukran:
Kutoka kwa Mu’az Ibn Jabal, amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:
«ﺧُﺬُﻭﺍ ﺍﻟْﻌَﻄَﺎﺀَ ﻣَﺎ ﺩَﺍﻡَ ﻋَﻄَﺎﺀً، ﻓَﺈِﺫَﺍ ﺻَﺎﺭَ ﺭِﺷْﻮَﺓً ﻓِﻲ ﺍﻟﺪِّﻳﻦِ ﻓَﻠَﺎ ﺗَﺄْﺧُﺬُﻭﻩُ، ﻭَﻟَﺴْﺘُﻢْ ﺑِﺘَﺎﺭِﻛِﻴﻪِ؛ ﻳَﻤْﻨَﻌْﻜُﻢُ ﺍﻟْﻔَﻘْﺮَ ﻭَﺍﻟْﺤَﺎﺟَﺔَ، ﺃَﻟَﺎ ﺇِﻥَّ ﺭَﺣَﻰ ﺍﻟْﺈِﺳْﻠَﺎﻡِ ﺩَﺍﺋِﺮَﺓٌ، ﻓَﺪُﻭﺭُﻭﺍ ﻣَﻊَ ﺍﻟْﻜِﺘَﺎﺏِ ﺣَﻴْﺚُ ﺩَﺍﺭَ، ﺃَﻟَﺎ ﺇِﻥَّ ﺍﻟْﻜِﺘَﺎﺏَ ﻭَﺍﻟﺴُّﻠْﻄَﺎﻥَ ﺳَﻴَﻔْﺘَﺮِﻗَﺎﻥِ، ﻓَﻠَﺎ ﺗُﻔَﺎﺭِﻗُﻮﺍ ﺍﻟْﻜِﺘَﺎﺏَ، ﺃَﻟَﺎ ﺇِﻧَّﻪُ ﺳَﻴَﻜُﻮﻥُ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢْ ﺃُﻣَﺮَﺍﺀُ ﻳَﻘْﻀُﻮﻥَ ﻟِﺄَﻧْﻔُﺴِﻬِﻢْ ﻣَﺎ ﻟَﺎ ﻳَﻘْﻀُﻮﻥَ ﻟَﻜُﻢْ، ﺇِﻥْ ﻋَﺼَﻴْﺘُﻤُﻮﻫُﻢْ ﻗَﺘَﻠُﻮﻛُﻢْ، ﻭَﺇِﻥْ ﺃَﻃَﻌْﺘُﻤُﻮﻫُﻢْ ﺃَﺿَﻠُّﻮﻛُﻢْ». ﻗَﺎﻟُﻮﺍ: ﻳَﺎ ﺭَﺳُﻮﻝَ ﺍﻟﻠﻪِ، ﻛَﻴْﻒَ ﻧَﺼْﻨَﻊُ؟ ﻗَﺎﻝَ: «ﻛَﻤَﺎ ﺻَﻨَﻊَ ﺃَﺻْﺤَﺎﺏُ ﻋِﻴﺴَﻰ ﺍﺑْﻦِ ﻣَﺮْﻳَﻢَ، ﻧُﺸِﺮُﻭﺍ ﺑِﺎﻟْﻤَﻨَﺎﺷِﻴﺮَ، ﻭَﺣُﻤِﻠُﻮﺍ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟْﺨَﺸَﺐِ، ﻣَﻮْﺕٌ ﻓِﻲ ﻃَﺎﻋَﺔِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺧَﻴْﺮٌ ﻣِﻦْ ﺣَﻴَﺎﺓٍ ﻓِﻲ ﻣَﻌْﺼِﻴَﺔِ ﺍﻟﻠﻪِ».
“Pokeeni zawadi maadamu ni zawadi. Na pindi inapokuwa ni rushwa katika Dini, basi msipokee, na hamtaiwacha; kwa kuzuiwa na ufukara na haja, hakika inzirani za Uislamu ni zenye kuzunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka, hakika Kitabu na Mtawala vitatengana, basi msitengane na Kitabu, hakika yake kutakuwepo na viongozi juu yenu watakaojipendelea mambo nafsi zao ambayo hawawapendeleeni nyinyi, mkiwaasi wanawauwa na mkiwatii wanawapoteza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tufanye nini (wakati huo)? Akasema: “Kama walivyo fanya watu wa Isa Ibn Maryam, walikatwa kwa misumeno, na wakabebwa juu ya mbao. Kifo katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko uhai katika kumuasi Mwenyezi Mungu.”
Jibu:
Wa Alaikum Assalamu Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Kuhusu Hadith hii, inasemekana kuwa sehemu ya silsila yake ya wapokezi (sanad) ni dhaifu… Inasemekana kuwa ina riwaya nyengine iliyo na wapokezi wa kuaminiwa:
1- Imeelezwa katika (Jami’ Al-Ahadith) cha Jalal Al-Din As-Siuti (aliyekufa 911 H):
– [11863]
«خذوا العطاء ما دام عطاء، وإذا صار رشوة على الدين فلا تأخذوه، ولستم بتاركيه يمنعكم الفقر والحاجة، ألا إن رحى الإسلام دائرة فدوروا مع الكتاب حيث دار، ألا إن الكتاب والسلطان سيفترقان، فلا تفارقوا الكتاب، ألا إنه سيكون عليكم أمراء يقضون لأنفسهم ما لا يقضون لكم، إن عصيتموهم قتلوكم وإن أطعتموهم أضلوكم، قالوا يا رسول الله كيف نصنع؟ قال: كما صنع أصحاب عيسى ابن مريم، نشروا بالمناشير وحملوا على الخشب، موت في طاعة الله خير من حياة في معصية الله»
“Pokeeni zawadi maadamu ni zawadi. Na pindi inapokuwa ni rushwa katika Dini, basi msipokee, na hamtaiwacha kwa kuzuiwa na ufukara na haja, hakika inzirani za Uislamu ni zenye kuzunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka, hakika Kitabu na Mtawala vitatengana, hakika Kitabu na Mtawala vitatengana, basi msitengane na Kitabu, hakika yake kutakuwepo na viongozi juu yenu watakaojipendelea mambo nafsi zao ambayo hawatawapendeleeni nyinyi, mkiwaasi wanawauwa na mkiwatii wanawapoteza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tufanye nini (wakati huo)? Akasema: “Kama walivyo fanya watu wa Isa Ibn Maryam, walikatwa kwa misumeno, na wakabebwa juu ya mbao. Kifo katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko uhai katika kumuasi Mwenyezi Mungu.”
(At-Tabarani kutoka kwa Mu’adh kwa silsila hii ya wapokezi (sanad): Al-Qasim ibn Yusuf ibn Ya’qoob Al-Balkhi alitupa habari, Ali ibn Hujar Al-Marwazi alitupa habari, na Khatab bin Sa’eed Ad-Dimashqi alitupa habari, na al-Husain ibn Ishaq At-tastariu, wamesema: Hisham bin Ammar alitupa habari, wamesema: Abdullah bin Abdul Rahman bin Yazid bin Jabir alitupa habari, kutoka kwa Al-Wadayn bin Atta, kutoka kwa Yazid bin Marthad, kutoka kwa Mu’adh bin Jabal, aliye sema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema… Imepokewa na At-Tabarani(16599), Al-Haithami amesema (238/5): Yazid bin Marthad hakumsikia Mu’adh, na Ibn Hibban na wengine wamemsahihisha Al-Wadayn bin Atta, lakini akaorodheshwa kama dhaifu na kundi jengine, lakini wapokezi wake walio salia ni waaminifu.
Imepokewa kutoka kwa: At-Tabarani katika Al-Shamieen (1/379 Na. 658), na At-Tabarani katika Al-Sagheer (2/42 Na. 749). Kama unavyo ona, baadhi ya wapokezi katika sanad walionekana kuwa na tatizo na baadhi ya wanachuoni wa Hadith, lakini baadhi yao wanaonekana kuwa waaminifu na wanachuoni wengine.
2- Imeelezwa katika (Ithaf Al-Khiarata Al-Maharata) na mwandishi wake Al-Hafidh Ahmad bin Abi Bakr bin Ismail Al-Busairi, aliye fariki mwaka wa 840 H:
«خذوا العطاء ما دام عطاء، فإذا صار رشوة على الدين فلا تأخذوا، ولستم بتاركيه يمنعكم من ذلك المخافة والفقر، ألا وإن رحى الإيمان دائرة وإن رحى الإسلام دائرة، فدوروا مع الكتاب حيث يدور، ألا وإن السلطان والكتاب سيفترقان، ألا فلا تفارقوا الكتاب، ألا إنه سيكون عليكم أمراء، إن أطعتموهم أضلوكم، وإن عصيتموهم قتلوكم قالوا: كيف نصنع يا رسول الله؟ قال: كما صنع أصحاب عيسى ابن مريم، حملوا على الخشب، ونشروا بالمناشير، موت في طاعة الله خير من حياة في معصية الله»
“Pokeeni zawadi maadamu ni zawadi. Na pindi inapokuwa ni rushwa katika Dini, basi msipokee, na hamtaiwacha kwa kuzuiwa hilo na hofu ya ufukara, hakika inzirani za Uislamu ni zenye kuzunguka, na hakika inzirani za Uislamu ni zenye kuzunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka, hakika Kitabu na Mtawala vitatengana, basi msitengane na Kitabu, hakika yake kutakuwepo na viongozi juu yenu mkiwatii wanawapoteza na mkiwaasi wanawauwa.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tufanye nini (wakati huo)? Akasema: “Kama walivyo fanya watu wa Isa Ibn Maryam, walibebwa juu ya mbao, wakakatwa kwa misumeno. Kifo katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko uhai katika kumuasi Mwenyezi Mungu.”
Imesimuliwa na Ishaq bin Rahwayh kutoka kwa Suwaid bin Abdul Aziz Al-Dimashqi, ambaye ni dhaifu na imesimuliwa na Ahmad Bin Mani’, na wapokezi wake ni waaminifu, na maneno yazo ni sawa.
Kama unavyo ona, baadhi ya riwaya ni dhaifu. Ama silsila ya wapokezi (sanad) ya riwaya ya Ahmad ibn Mani’, ni waaminifu.
Nataraji hili lina tosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa Hekima
Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
9 Shawwal 1441 H – 31/5/2020 M
Maoni hayajaruhusiwa.