Suala la Eid Mbili Litusukume Kurejesha Serikali ya Kiislam
Kwa masikitiko makubwa kumekuwa na hali ya kufanyiana kejeli na dharau miongoni mwa baadhi yaWaislamu kuhusiana na uwepo wa Eid mbili, yaani siku mbili tofauti. Ukweli hali hiyo ni natija/ matokeo ya matunda machungu ya mfumo mbovu wa kikafiri wa kibepari uliozaa nidhamu ya kidemokrasia. Mfumo ambao kwani huwagawa Waislamu kwa misingi ya mipaka ya vijinchi na athari zake kuenea mpaka katika upande wa ibada zao.
Lakini kwa upande mwengine mfumo huo huo huwaunganisha Waislamu hao hao kuwa kitu kimoja katika michakato fikra za kikafiri kama vile mchakato wa siasa za kidemokrasia. Tunashuhudia Waislamu wanavyoungana na kushikamana katika gurudumu la vyama vya kidemokrasia, ambapo hudhihirika kuwa kitu kimoja, tofauti yao ni maslahi tu.
Aidha, muungano au mshikamano kama huo hudhihirika kwa sura pana zaidi pale inapotokea agenda inayosukumwa na demokrasia, katika hali hiyo situ huwa ni mshikamano wa Waislamu baina yao bali hujumuisha watu wote huwa kitu kimoja iwe Waislamu, wakiristo au dini nyengine.
Hapa utaona ni kwa kiasi gani mfumo wa ukafiri unavyowaunganisha watu kuwa kitu kimoja katika kujilinda na kujitetea. Lakini mfumo huo huo hujenga na kuchochea mifarakano na migawanyo katika fikra isiyokuwa yao, kama hii ya swala ya Eid.
Suala la Waislamu kukebehiyana, kudharauliana na kutukanana kwa suala kama hili sio sahihi. Kufanya hivyo ni makosa makubwa na pia ni kufikia malengo wanayotaka makafiri tufikie.
Ummah wetu ulipaswa kuliangazia hili kwa upana kuwa ni gonjwa kubwa linalotuathiri katika Uislamu na tuna wajibu tulitibu kwa mujibu wa Uislamu, na si kwa mujibu wa mfumo wa kikafiri au kufanyiana kejeli na dharau, kwani hiyo sio tiba, bali ni kukuza usugu wa ugojwa na kuchochea mifarakano zaidi.
Hapana shaka kwa mwenye akili na ufahamu wa kina juu ya Uislamu ataelewa kwa uwazi kwamba Uislamu una dawa ya kila gonjwa likiwemo hili, kwani Uislamu umekamilika na una tiba ya kila gonjwa.
Na kwa udhati serikali ya Kiislamu ya Khilafah Rashidah ndio pekee yenye tiba ya kutibu gonjwa hili na mengineyo, kwani ina kila nyenzo ya kuwaunganisha Waislamu wote na mtizamo thabiti katika masuala yenye rai zaidi ya moja. Na hivyo unaufinyanga Ummah kuwa na lengo, hisia na fikra moja juu ya Uislamu wao.
#UislamNiHadharaMbadala
Na Mohamed Kombo
Maoni hayajaruhusiwa.