Sheikh Salman Al-Ouda Kunyongwa na Ufalme Wa Saudia
Serikali ya kidhalimu ya Saudia yapitisha hukmu ya kifo kwa mwanachuoni mkubwa Sheikh Salman Al-Aouda (62). Pamoja na kwamba mwanachuoni aliwahi kuwa mwanafunzi katika Chuo cha Burayda ambacho miongoni mwa walimu wake ni Sheikh Ibn Baaz na Sheikh Muhammad Uthaymeen, lakini amekuwa kinyume nao kwa kusimama juu ya haki na kuikosoa tawala dhalimu ya ufalme wa Saudia, kamwe hakujipendekeza kwao wala kuwapaka mafuta.
Mwaka 1994 Sheikh Al-Ouda alifungwa jela kwa kuikosoa serikali ya Saudia
Septemba 2017- Julai 2018 Sheikh Al-Ouda akawekwa kizuizini bila ya kupelekwa mahkamani, akazuiliwa kusafiri na kuonana na na familia yake kwa sababu hakukubali kuiunga mkono serikali ya Saudia kufuatia hatua yake ya kuikaba kwa vikwazo na kuibana nchi ya Qatar.
Septemba 2018 katika mchakato wa kusikilizwa kesi yake, mahkama ilitakiwa Sheikh apewe hukmu ya kifo.
Februari 2019 tayari ameshaamuliwa kupitishiwa hukmu hiyo.
Allah Sw Ampokee Sheikh Al-Ouda kwa mapokezi mema na amuingize miongoni mwa waliofuzu. Aidha, Allah Taala Afanye haraka kuwatia mkononi watawala madhalimu wa Saudia na wengine wote ambao wanatenda dhulma kwa Ummah mtukufu wa Kiislamu
Amiin
Hasbunallah waniima l wakiil
(Chanzo : Jarida la Gaza Now : http://gazaalan.live/post/27847 )
Maoni hayajaruhusiwa.