“Na hawajaona baya lolote kwa wislamu ila ni kumuamini Allah mwenye kushinda na mwenye kusifiwa”

0

وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ

“Na hawajaona baya lolote kwa wislamu ila ni kumuamini Allah mwenye kushinda na mwenye kusifiwa”

[A-Buruj:8]

Shirika la ulinzi la nchi ya jordan limemshikilia ndugu Ismail Al-Wahwah ( abu Anas ) katika sehemu ya kuingilia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa malkia Alia mnamo tarehe 25/7/2018, na wamemuwekakizuizini hadi muda huu.
Sisi Hizb ut Tahrir Tunauwajibisha utawala wa jordan na katiba yake juu ya afya na usalama wa ndugu yetu Abu Anas, mlinganiaji wa daawa ya haki inayobeba ajenda ya Ummah ya kurejesha Khilafah.
Na kama Abu Anas angelikua ni miongoni mwa mafisadi wanaoiba utajiri wa nchi na kunyonya jasho la wananchi, kama ingelikua hivyo, basi angekua anaingia na kutoka katika nchi akiwa analindwa na vyombo hivi vya dola ambavyo vinawalinda mafisadi na kuweza shughuli zao, halafu badala yake wanawakamata walinganizi wasio na hatia wanaolinginia na kuwaita watu katika “La ilaha illa Allah” (hakuna mungu ila allah pekee), Ambao wanafanya kazi kwa ajili ya kutabikisha hukmu za Allah.
Tunawahakikishia watu wa usalama wa serikali ya Jordan kwamba, mbinu hizi wanazotumia kuwazuia watu katika njia ya Allah kamwe haziwezi kuwarudisha nyuma Hizb ut Tahrir na mashabab wake kuachana na ulinganizi kwa Ummah na wataendelea hadi pale ahadi ya Allah na Mtume wake itimie ya kusimamisha khilafah rashidah kwa kupitia njia ya utume.
#UislamNiHadharaMbadala

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.