Minasaba ya Novemba
2/11 1917 – Uingereza chini ya Waziri wake wa Nje, Arthur James Balfour yatangaza kuunga mkono kuasisiwa dola ya Mayahudi ndani ya Palestina. Tamko rasmi la Waziri Balfour (The Balfour Declaration).
2/11/1844 – Kuzaliwa Khalifa Mehmed V. Alifariki mwaka 1918.
3/11 1986 – Kuibuka kwa Kashfa kubwa ya dola ya Marekani inayoitwa The Iran-Contra Affair kufuatia Marekani kuiuziya Iran silaha kwa siri ili kuachiwa huru mateka saba wa kimarekani waliokuwa wakishikiliwa ndani ya Lebanon.
3/11 1956 – Jeshi la Mayahudi latenda dhulma kubwa ya mauwaji ya Waislamu katika Ukanda wa Gazza eneo la Khan Yunis( The Khan Yunis killings) yaliyopelekea vifo 275 vya watu wazima wanaume.
4/11 1995 – Waziri Mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin auwawa na myahudi muhafidhiina mwenye misimamo mikali.
4/11 2012, Raisi Obama achaguliwa kuwa raisi wa mwanzo mwenye asili ya watu weusi.
5/11 2006 – Saddam Hussein na wasaidizi wake Barzan Ibrahim al-Tikriti na Awad Hamed al-Bandar wahukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa katika mahkama ya al-Dujail
5/11 1872 – Kupamba moto harakati za wanawake kudai haki ya kupiga kura ndani ya Marekani. Katika mchakato huo mwanaharakati Susan B. Anthony alipiga kura kwa mara ya mwanzo kwa nguvu na kupigwa faini ya dola mia moja.
6/11 1494 mwaka wa 1494 – Kuzaliwa Khalifah Suleyman Al-Qanun. Alifariki ndani ya mwaka 1566
6 /11 644 Khalifah Umar Ibnul- Khattab alifariki dunia. Baada ya kujeruhiwa vibaya kwa upanga.
6/11 1987 – Raisi wa Tunisia Habib Bourguiba apinduliwa na nafasi yake kushikiliwa na Zine El Abidine Ben Ali
6 /11 745 kuzaliwa kwa Imamu Musa al-Kadhim, Mwanachuoni Mkubwa na mtoto wa Imamu Jaffar Sadiq
7/11 1917 Ndani ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Uingereza yaupora kijeshi mji wa Gazza kutoka kwa Khilafah Uthmania katika vita vinavyojuulikana kama Vita vya Gazzah.
9/11 1953 kufariki kibaraka Ibn Saud. Alizaliwa Januari 1876
10/11 1444 – Mapambano ndani ya mji wa Varna ikiwa muendelezo wa Vita vya Msalaba chini ya mfalme Vladislaus III. Jeshi la makafiri lilipata kipigo kikali kutoka kwa Waislamu chini ya Khalifah Murad II na kupelekea Mfalme Vladislaus kuuwawa.
11/11 1985 – Mchambuzi wa kijasusi ndani ya Jeshi la Marekani Jonathan Pollard akamatwa kwa kuvujisha siri za kijeshi kwa Israel. Baadae akafungwa kifungo cha maisha.
19/11 Siku ya Kimataifa ya Wanaume ( International Men’s Day )
19/11 Siku ya Matumizi ya Choo Duniani.(World Toilet Day )
20/11 Siku ya Kumbukumbu ya Wanaobadilisha Jinsia (Transgender Day of Remembrance)
22/11 1943 – Lebanon yapata uhuru wa bendera kutoka kwa Ufaransa.
27/ 11 1095– Papa Urban II atangaza rasmi Vita vya mwanzo vya Msalaba dhidi ya Waislamu Katika Baraza Kuu la Kanisa/ Clermont (Council of Clermont)
30/11 Siku ya Sikukuu mijini kuunga mkono kukomesha adhabu ya kifo. (Cities for Life Day )
Novemba 1869 –Uzinduzi rasmi kwa Umma mfereji wa Suez na bahari ya Mediterranean na bahari nyekundu.
Novemba mwaka wa 1914, Katika mchakato wa Vita vya Mwanzo vya dunia, Dola ya Himaya ya Urusi yatangaza vita dhidi ya Khilafah Uthmania.
Novemba 2007 – China yazindua satalite yake ya mwanzo ya nguvu za jua inayoitwa Chang’e 1 iliyokwenda mwezini.
Novemba 2009 – Meja wa Jeshi la Marekani Nidal Malik Hasan awauwa wanajeshi wenzake 13 na kuwajeruhi 29 katika kambi yao ya kijeshi ya Fort Hood
Novemba 2001 – Vita vya Afghanistan: Kundi la Northern Alliance kwa msaada wa Marekani lauteka mji wa Kabul.
Novemba 2002 –Kupitishwa Azimio la Umoja wa Mataifa no. 1441 la uvamizi wa Iraq. Baada ya kisingizio cha mgogoro wa kuinyang’anya silaha Iraq.
Kila Alkhamisi ya nne ya Novemba ni Siku ya Kumshukuru Mungu ndani ya Marekani (Thanksgiving day)
Kila Alkhamisi ya Tatu ya Novemba ni Siku ya Falsafa Duniani. ( World Philosophy Day)
Maoni hayajaruhusiwa.