Mauaji Syria

Ripoti kutoka Nchini Syria zinasema zaidi ya waislamu 3000 waume, wanawake na watoto wameuliwa kwa mabomu ndani ya masaa 48.

Haya ni mashambulizi yaliyoratibiwa na vibaraka wa wamagharibi, vibaraka ambao walisikika kutoa rambirambi kwa waislamu waliouwawa kwa shambulio la New zealand.

Kama itahitajika dakika 2 au ukimya, kwa ajili ya kuomboleza mauaji wanayofanyiwa waislamu leo duniani, itatulazimu tukae kimya kabisaa kwa sababu takriban kila baada ya dakika waislamu wanauwawa duniani kote. Ila huu sio wakati wa kukaa kimya, ni muda wakusema ukweli kwa kufichua maovu yafanywayo na viongozi waovu, mmoja katika viongozi hao ni Erdogan ambaye ameziruhusu ndege za kivita za Marekani na Urusi kuwashambulia waislamu wa Syria zikitokea ardhi ya Uturuki.

Ni suala la muda tu,  tunaifanyakazi ya kuirejesha Izzah ya waislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni khilafah pekee na Khalifah pekee, na hakuna nchi yoyote inayojiita kwa jina la kiislamu yenye uwezo wa kuulinda utukufu wa damu za waislamu na ardhi zao.
Utukufu wa damu za waislamu ni haramu kupuuzwa, Abdullah bin Umar r.a amesema:

“Nilimuona Mtume صلى الله عليه وسلم akifanya tawaaf, akawa akisema kulisemea Alkaaba, uzuri ulioje ulionao na harufu nzuri ilioje, ukubwa ulioje ulionao na utukufu. Naapa kwa yule ambaye roho ya Muhammad ipo kwenye mikono yake kwamba..’muislam ni mbora na mtukufu zaidi mbele za Allah سبحانه وتعالى kuliko utukufu wako (kaaba)”

Ingawa Kaaba inachukuliwa kuwa ni miongoni mwa alama kubwa tukufu za uislamu, ambapo waislamu wote duniani kote wanaielekea yenyewe mara tano kwa siku, na swala ufanyayo ndani yake ina malipo makubwa kuliko popote, lakini damu ya muislamu mmoja ni tukufu mbele ya Allah سبحانه وتعالى kuliko nyumba ya kwanza iliyojengwa kwa ajili ya kuabudiwa yeye

Kwa kuwa damu ya muislamu mmoja ni tukufu mbele ya Allah سبحانه وتعالى kuliko Kaaba, na ni tukufu kuliko dunia na vilivyomo, hivyo basi ni juu ya waislamu kutoa kipaumbele kwa waislamu na damu zao na kupuuza utukufu wa damu za waislamu ni mbaya zaidi kuliko kuvunja Kaaba.

Kulingana na hali jinsi ilivyo, jambo bora kufanywa na kila muislamu leo hii ni kulinda utukufu wa damu za waislamu wote jumla imma wawe wa Palestina, Syria, Afghanstan, Kashmir, Uygher, Burma, utukufu huu kipekee unaweza lindwa na Imam, amesema Mtume صلى الله عليه وسلم

“Hakika kiongozi ni ngao, mnapigana nyuma yake na kujikinga nae, kama ataamirisha uchajimungu na uadilifu atapata malipo kwayo….”
(Muslim)

AlKhilafah

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1561646377303688&id=646683775466624

Maoni hayajaruhusiwa.