Manufaa ya Hijja ya Leo Sio Kamilifu

Tukiwa katika msimu wa ibada tukufu ya Hijja, ibada kongwe ambayo Allah mtukufu Alimuamrisha baba wa Mitume Ibrahim As kuitangaza ili iwafikie watu :
وَأَذِّنْ فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالاً وَعَلَى كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِنْ كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ
(الحج: 27)

“Na watangazie watu Hijja, watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali kabisa”.
(Hajj : 27)

Allah, Al Aziz Ar Rahim Ametuwekea ibada mbalimbali (ibada khassa) kama hii ya Hijja, Swalah, Swaum nk. Ndani ya ibada hizo Allah SW Ameweka manufaa makubwa kwetu, sawasawa yawe tunayoyajua au tusiyoyajua, yenye kushikika na yasiyoya kuhisika.

Miongoni mwa manufaa makubwa ya Hijja kama zilivyo ibada zingine ni kutimiza amri ya Allah SW, kwani Yeye (SWT) Amewajibisha ibada hii kwetu (faradhi).
Kilele cha utekelezaji wa Hijja ni kupata ucha Mungu (taqwa), pia ibada hii huambatana na kuchinja wanyama na kutoa sadaqa mbalimbali ili kujikurubisha zaidi kwa Allah Taala, na manufaa ya matumizi vichinjwa hivyo hupaswa kuwafikia Ummah mashariki na magharibi hususan maskini, mafukara, mayatima n.k Allah anatuthibitishia hilo kwa kauli yake:
لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الأَنْعَامِ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ
(الحج: 28 )

Ili washuhudie manufaa yao, na walitaje jina la Allah katika siku maalumu juu ya wanyama hao Aliowaruzuku. Basi kuleni (katika hao wanyama) na mlisheni mwenye shida aliyefakiri”
(Hajj : 28)

Aidha, kiwango fulani cha ucha Mungu kinachopatikana kwa mahujaji huporomoshwa kwa makhatibu katika viwanja vya Hijja na siku ya Eid kutoa khutba za kuulaza Ummah badala ya kuangazia qadhia nyeti kwa Umma kama kumtafuta Amir (Khalifah) mmoja wa Umma, uvamizi katika ardhi za Waislamu, kupambana na fikra za uaswabia nk.
Tusisahau pia Mahujaji hukabiliwa na vitendo vya ubaguzi na vitisho kutoka kwa watawala wakizuiwa wasiongeze siku za kubakia ndani ya mji mtukufu baada ya Hijja kumalizika. Maeneo ambayo Waumini wote wana haki sawa :
وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاءً الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِي

“…Na Msikiti mtakatifu ambao tumeufanya kwa ajili wote (kuwa na haki) sawa sawa, (ni sawa) kwa ajili a wakao humo na wageni… “
(Hajj : 25)

Kwa upande mwengine ibada ya Hijja imegeuzwa kuwa mtaji wa watawala wa kifalme wa Saudia na familia zao kiasi cha kupaisha juu gharama zake. Kwa hapa Tanzania inafikia hadi dolari 4500 au zaidi, takribani shilingi milioni 10. Pamoja na hivyo watawala wamesheheni uzembe katika usimamizi na kutojali maisha ya mahujaji kiasi cha kupelekea ajali kubwa na majanga ya hatari ambayo huangamiza maisha ya Waislamu wengi.
Kiudhati manufaa ya Hijja na ibada zingine zote yatafikiwa kwa ukamilifu wake pale Waislamu watakapokuwa chini ya usimamizi/ kiongozi thabiti wa Kiislamu(Khalifah) ambaye atasimamia ibada hii ya Hija na ibada nyingine zote.
Wakati tukiwemo katika mchakato wa kuifanikisha ibada ya Hijja, ni wajibu kutafakari na kuchukua hatua madhubuti juu ya qadhia nyeti ya kurejesha tena maisha ya Kiislamu ulimwenguni kwa kurejesha dola ya Khilafah Rashidah kwa kuanzia katika nchi kubwa za ulimwengu wa Kiislamu.
Tunawatakia kila la kheri mahujaji wote.

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

26 Dhu al-Qidah 1439 Hijri | 06-08- 2018 Miladi

Front Page

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.