Makubaliano ya Sweden na Athari Yake Juu ya Janga la Yemen

Swali:
Mnamo 18/12/2018, tovuti ya kituo cha runinga ya France 24 iliripoti: “Ghasia zilizuka katika mji wa
Hodeidah nchini Yemen kati ya majeshi tiifu kwa serikali na Mahouthi, dakika chache baada ya makubaliano
ya kusitisha vita yaliyofungishwa na Umoja wa Mataifa kukamilika…” (France 24, 18/12/2018). Mnamo
17/12/2018 tovuti ya Arabic.Sputniknews iliripoti:
“Mwanachama wa ujumbe wa Ansar Allah alisema kuwa makubaliano ya Sweden hayakujumuisha kuisalimisha bandari ya Hodeidah au kuondoka kwa Mahouthi kutoka mjini humo, ambapo Waziri wa Habari wa Yemen Muammar al-Iryani alijibu kwa kusema kuwa taarifa hizi zinafahamika kama mapinduzi dhidi ya makubaliano yenyewe, ambayo wino wa saini yake bado haujakauka (ungali majimaji), akisisitiza kuwa makubaliano hayo yalitaja kujiondoa kwa wanamgambo hao kutoka Hodeidah na bandari zake, Hodeidah, Salif na Ras Issa.”
Swali ni: ni vipi kuna sintofahamu katika maandishi ya makubaliano hayo wakati wino wa saini yake ungali
majimaji?! Na ni vipi ghasia zizuke dakika chache tu baada ya kutekelezwa kwake? Kwa hiyo ni kwa nini
Amerika na Uingereza zinayakaribisha makubaliano hayo? Je, janga hilo la Yemen linatarajiwa kumalizika
kwa makubaliano haya? Allah akujazi kheri.

Jibu:

Kabla ya kwenda katika kadhia ya Makubaliano ya Yemen, ambayo mazungumzo yake yalianza mnamo
Alhamisi 6/12/2018 na kumalizika kwa kupeana mikono wazi mnamo 13/12/2018, hali ya Yemen inapaswa
kufupishwa kama ifuatavyo:
Kwanza, baada ya Mahouthi kuchukua udhibiti wa Sanaa na baada ya kufurushwa kikweli kwa serikali ya
Hadi kutoka katika mji mkuu huo, na kuchukua udhibiti wa maeneo mengi ya Yemen, walikuwa na haja kubwa ya kuwa na baadhi ya “uhalali” katika utawala wao. Amerika ilijaribu kuwatafutia “uhalali”. Lakini hili halikuwa rahisi, kwa kuwa kitovu cha kisiasa cha Yemen kwa kiasi kikubwa kinaegemea kwa Uingereza, kwa hivyo matarajio makubwa kabisa ya Amerika yalikuwa ni kukubali kwa Mahouthi kuwa kama sehemu muhimu ya ramani ya kisiasa ya Yemen. Mahouthi ni wachache eneo la Kaskazini mwa Yemen hususan mjini Saada, na hawakubaliki miongoni mwa watu jumla, kwa hivyo Amerika ilifanya kazi kuwasaidia Mahouthi hawa ili wawe watu muhimu nchini Yemen ili kusiendelee utawala wowote pasi na wao, na hili ni kupitia hatua zifuatazo:

1- Iliifanya Saudi Arabia kushambulia kupitia operesheni ya angani “dhoruba kali”, sio kuwamaliza Mahouthi; vyenginevyo, wangepeleka majeshi ya nchi kavu, lakini ili kuwaonyesha Mahouthi kama watetezi wa Yemen mbele ya ndege za kivita, wakionekana kama waliodhulumiwa na wakati huo huo kama mashujaa, na hivyo basi kupata umaarufu wa kukubaliwa na rai jumla.

2- Hadi, Raisi wa Yemen mtiifu kwa Waingereza, alifanywa kama mateka nchini Saudi Arabia, na hivyo
wanaweza kumtia shinikizo kwa urahisi kila mipango hiyo inapohitaji.

3- Ililishawishi Baraza la Usalama kutuma wajumbe nchini Yemen walio na utiifu kwa Amerika, na kufaulu
katika hili, hivyo basi, Jamal bin Omar, na Ould Cheikh walitumwa.
Uingereza, ambayo imekuwa na ushawishi nchini Yemen kwa miongo kadhaa, inajua kuwa harakati ya
eneo la kusini na Mahouthi eneo la kaskazini ni vyombo vya Amerika vya kupenyeza ushawishi wake mkubwa nchini Yemen. Kupitia kuingia kwa Mahouthi jijini Sanaa na kwengineko nchini Yemen na kufaulu kwao kupata usaidizi mkubwa wa kijeshi wa Iran, Uingereza iliona kuwa ushawishi wake nchini Yemen umeanza kuyumba, hususan baada ya dori ya Saudia nchini Yemen, hivyo basi Uingereza ilikimbilia kujibu mipango na ala za Amerika:
a- Dori iliyochezwa na Imarati sambamba na ile dori ya Saudia. Hakika, Imarati ilicheza dori muhimu sana
katika kurudisha mji wa Aden na miji mengineyo eneo la kusini kutoka mikononi mwa Mahouthi, na kupitia dori hii iliunda harakati ya eneo la kusini iliyo wapunguza makali vibaraka wa Amerika katika harakati hii na kuifanya dori yao kushika nafasi ya pili, na kuidhibiti kusini.
b- Ilimleta kibaraka wa zamani, Ali Saleh, eneo la kusini katika safu ya Mahouthi. Akawa ni mshirika wao na
katika ngazi zao, ili Uingereza ishiriki katika dori na Mahouthi endapo watachukua mamlaka, na alikaribia
kufaulu katika misheni yake kabla ya kumuua.
c- Ilifanya bidii kutuma mjumbe wa UN aliyemtiifu kwake, na iliweza kufanya hivyo, kwa hivyo Muingereza Martin Griffith aliteuliwa kama balozi mpya wa kimataifa nchini Yemen.

Pili: Uingereza ilijua kuwa uti wa mgongo wa Mahouthi ni usaidizi wa Iran. Baada ya kufungwa uwanja wa ndege wa Sanaa na kudhibitiwa kwa bandari za kusini, bandari ya Hodeidah ilikuwa ndio ya pekee yenye mwanya nusu wa iran wa kusaidia Mahouthi. Hii ndio sababu Imarati ilikwenda Hodeidah ili kuidhibiti. Makabiliano na vita maeneo ya Hodeidah yalikabiliwa na upinzani  mkubwa wa Amerika chini ya kisingizio cha ubinadamu, na kwamba bandari ya Hodeidah inaipa Yemen msaada kwa mamilioni ya Wayemeni kana kwamba Amerika inajali binadamu. Iliwavunja vunja vibaraka wake nchini Syria chini ya Umoja wa Mataifa kwa kuizingira miji iliyo taabani na kwa ulipuzi wa makombora.

Lakini ilitaka kutafuta uhalalishaji wa kuifanya bandari ya Hodeidah kuwa wazi kwa usaidizi wa kijeshi wa Iran, ambao kwa mwaka au zaidi ulijumuisha makombora ya angani ambayo Mahouthi walianzisha juu ya
Saudi Arabia, pamoja na ndege zisizokuwa na rubani (drones) zilizo rushwa kwa kulenga maeneo makhsusi
nchini Imarati. Kinyume na hayo, Saudi Arabia ilikuwa ikizungusha ndege zake pasi na mashambulizi ya
kihakika ya kambi za Mahouthi, kwa mfano majeshi ya Mahouthi yaliizingira Taiz na maeneo ya vikosi vyake vya kijeshi yalianikwa kwa udhibiti wa angani na hivyo basi kambi hizo hazikuwa vigumu kuzishambulia na kuondoa mzingiro huo, ingawa mzingiro huo bado ungalipo! Kihakika Imarati ilikuwa ikipigana na Mahouthi hadi ikakaribia kuwatoa Mahouthi nje ya Hodeidah lau si kwa shinikizo la Amerika juu ya Saudi Arabia!

Hivyo basi, mipango ya Amerika na ala zake haikuafikiana na mipango ya Uingereza na ala zake.
Amerika iliegemea upande wa suluhisho la kisiasa baada ya kuudhamini udhibiti wa Mahouthi juu ya sehemu muhimu za Yemen. Uingereza ilikuwa ikisubiri kushindwa zaidi kwa Mahouthi ili kukubali kujiondoa, ambako kungewafanya kurudi katika makubaliano ya Saada kabla ya kwenda katika suluhisho halisi la kisiasa. Hivyo basi, majadiliano yote ya nyuma hayakuwa chochote zaidi ya “michezo” ya kisiasa ya kupitisha wakati. Hivyo basi, mazungumzo kama hayo hayakufaulu, kama vile majadiliano ya Kuwait na majadiliano ya Geneva mwanzoni mwa Septemba, pindi ujumbe wa Mahouthi ulipo kosa hata kufika … nk. Kwa hayo, majadiliano hayo yalifeli na Mahouthi wakasimama mbele ya hatari kubwa ya kukaribia kuchukuliwa Hodeidah na bandari zake na majeshi yanayo saidiwa na Imarati, baada ya kuweko pambizoni mwake. Wakati huo huo, dori kubwa zaidi ilikuwa kwa Imarati, iliyo wapeleka na kuwasajili wanamgambo wanati kwa ajili ya vita vya Hodeidah. Saudi Arabia ilikuwa katika hali ya kufedhehesha; haikuweza kupinga mwelekeo huu wa Imarati kwa sababu ni “washirika” walio uwanjani katika vita vya Yemen dhidi ya lengo lililo tangazwa na Mahouthi! Na kwa sababu Amerika inazuia shambulizi juu ya Hodeidah, Imarati, na nyuma yake Uingereza, ilichagua muda ambapo Amerika ilijiingiza katika kadhia iliyo na shinikizo zaidi kwake. Vita vya Hodeidah vilizuka mnamo 8 na 9/6/2018 (Alhurra 10/6/2018) katika wakati ambao Amerika ilijiingiza pakubwa kwa matayarisho ya Kongamano la Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini lililofanyika nchini Singapore mnamo 12/6/2018.

Yaani, ilichagua muda ambao Amerika takriban imepooza kutokana na kusitisha shambulizi hilo. Na ndivyo ilivyokuwa … Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifeli kusitisha mapigano ya Hodeidah: “Mnamo
Alhamisi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kukubaliana juu ya kukomesha mara moja
mashambulizi ya Muungano wa Waarabu unao ongozwa na Saudi Arabia na Imarati juu ya mji wa Hodeidah.” (Al Jazeera Net 15/6/2018). Vita vya Hodeidah na uwezekano wa udhibiti wa Imarati na wanamgambo wanaosaidiwa nao juu ya bandari ya Hodeidah lilikuwa ndio tishio kubwa zaidi kwa utawala wa Mahouthi nchini Yemen. Hivyo basi, Mahouthi walipeleka majeshi yao yote ili kuzuia kutokea kwa haya, na Amerika ilipeleka maafisa wake kulalamikia kuhusu hali ya kibinadamu nchini Yemen na juu ya bandari ya Hodeidah kwamba ndio mwokozi wa kukomesha baa la njaa nchini Yemen. Imarati na washirika wake wa eneo walikuwa wakisubiri fursa za kimataifa ili kuanzisha mashambulizi zaidi na kujaribu kusonga mbele ardhini katika kulazimisha uhalisia uwanjani juu ya mji huo na bandari hiyo, ambao ulipatikana nusu yake na kuwa tishio kubwa kwa Mahouthi na hivyo basi kuwa ushawishi mwengine wa Amerika nchini Yemen. Katika miezi ya hivi karibuni, kuzuka kwa mapigano ya mara kwa mara maeneo ya Hodeidah imekuwa ni sehemu ya vita hatari zaidi vya Yemen. Hususan, Amerika imeshindwa kuuvuruga Muungano wa Saudia na Imarati nchini Yemen, kama ilivyo shindwa kusitisha vita katika upande wa Saudi Arabia pekee, ikiwemo uharibifu kutokana na dori ya kiuongozi ya Saudia ya dola za Ghuba, na hali ikabakia hivyo hivyo hadi ilipotokea kadhia ya fedheha kubwa sana kwa Saudi Arabia, iliyofuatiwa na kuuliwa kinyama kwa mwandishi habari wa Saudia Jamal Khashoggi mwanzoni mwa Oktoba 2018.

Tatu: kuuliwa kwa mwandishi habari wa Saudia Khashoggi jijini Istanbul kulipelekea kuibuka kwa dhurufu
mpya zilizoizunguka Saudi Arabia ambazo huenda zilitumiwa kwa maslahi ya Amerika:

1- Huduma za usalama za Saudia zilitekeleza kitendo cha kinyama katika ubalozi wao jijini Istanbul, kilicho
pelekea kampeni ya kimataifa dhidi ya Saudi Arabia, kisiri na wakati mwengine kidhahiri, ikitoa wito wa
kuhesabiwa Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Muhammad Bin Salman kwa kutekeleza kitendo cha kinyama dhidi ya maadili yoyote ya kibinadamu. Ingawa Saudi Arabia na watawala wengine wahalifu katika eneo la Waislamu wametekeleza maafa dhidi ya raia wake kuliko kuuliwa kwa mwandishi habari wa Saudia jijini Istanbul, lakini kitendo hiki kimezalisha hamasa za kutosha, ambazo zimepelekea shutuma kali za nchi nyingi. Nchi za Ulaya zilitaka kuzitumia ili kumdhoofisha kibaraka wa Amerika, Bin Salman, au ikiwezekana kumng’oa mamlakani, lakini Amerika ilifanya haraka kupeana sitara ya kimataifa kwa Bin Salman, kupitia tweet za Raisi Trump zilizo onyesha imani kwa kile anachosema mfalme mtarajiwa wa Saudia, hivyo basi kuondoa tuhuma hizo. Trump alisema parwanja kuwa hataachana na mikataba ya silaha na Saudi Arabia kutokana na manufaa ya kudhibiti ukosefu wa ajira nchini Amerika, ambayo imeongeza shinikizo la
wabunge wa Congress kwa utawala wa Trump, ambao waliutuhumu kupigia debe kile ambacho wanachama
wa bunge la Congress wanakiita “maadili ya Kiamerika” kwa ajili ya pesa za Saudia. Bunge hilo la Congress
kisha likatoa makemeo ya nadra ya kihistoria dhidi ya utetezi wa Raisi Donald Trump kwa Muhammad Bin
Salman: (Katika makemeo ya kihistoria ya kumkemea Raisi Donald Trump, bunge la Seneti la Amerika lilipiga kura mnamo Alhamisi ili kumaliza usaidizi wa kijeshi wa Amerika kwa vita nchini Yemen na Mfalme Mtarajiwa Muhammad Bin Salman akabebeshwa masuliya kwa mauwaji ya mwandishi huyo wa habari. Jamal Khashoggi wa Saudia … katika hatua ya kihistoria bunge la Seneti lilipiga kura 56 hadi 41 ili kumaliza usaidizi wa kijeshi kwa kampeni inayo ongozwa na Saudia nchini Yemen. (Reuters, 14/12/2018)

2- Pindi wanachama wengi wa bunge la Congress walipoonyesha wasiwasi kuhusu haja ya kukomesha
kuamiliana na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia, “kibaraka mtiifu wa Amerika” na baadhi kutoa wito wa kukomesha upelekaji silaha Saudia, ambazo Trump anajingamba kwazo, kwa athari iliyo nazo katika kubuni ajira nchini Amerika, utawala wa Trump hatimaye ukakimbilia kuleta purukushani kutoka kuangazia kesi ya Khashoggi na kuituhumu Saudi Arabia kwa kadhia nyengine muhimu inayo onyesha kuwa Saudi Arabia inasimama na haki za kibinadamu, amani, na usalama, na kwamba inashirikiana na Umoja wa Mataifa. Ushirikiano wa mtoto wa Salman ulipigiwa debe wakati wa mazungumzo ya Sweden: “Afisa wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo ya mwisho nchini Sweden katika kusaidia juhudi za balozi wake wa amani nchini Yemen ili kuanza mchakato wa kisiasa kumaliza vita vinavyo endelea vya miaka minne. Shirika rasmi la Habari la Saudia lilisema kuwa Guterres alimpigia simu Mfalme Mtarajiwa Muhammad Bin Salman ili kujadili “mapya yanayo jiri katika uwanja wa Yemen, na juhudi zinazo fanywa juu yake.” (Reuters, 12/12/2018).

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, aliangazia juu ya mchango wa Salman: Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alifichua kwa kituo cha Al Arabiya mnamo Alhamisi dori iliyochezwa na Mfalme Mtarajiwa, Muhammad Bin Salman, katika makubaliano ya Yemen ya kihistoria
leo kati ya Ansar Allah na serikali ya Yemen … Naibu Msemaji Rasmi wa UN Farhan Haq aliwaambia
maripota katika makao makuu ya UN jijini New York mnamo Alhamisi kuwa Guterres alihisi kuwa mchango
wa Mfalme huyo Mtarajiwa “ulikuwa muhimu mno kwa matokeo ya mashauriano hayo” (Arabic.Sputniknews
13/12/2018). Hivyo basi, Amerika iliangazia dori yake kwa njia ya kustaajabisha kufikia hadi Griffith kuwajibika kuisifu dori hii: Griffith alisema katika kongamano kwa njia ya video kutoka Jordan kuwa majadiliano kati ya pande za Yemen yalifaulu kufikia mkataba na akaongeza kusema: “Namshukuru Mfalme Mtarajiwa, Mheshimiwa  Mfalme Muhammad Bin Salman, ambaye amethibitisha usaidizi wake muhimu mno wa kibinafsi kwa mchakato huu (Al-Watan News 14/12/2018) Yote haya yaonyesha kuwa Amerika inahamu ya kufanya makubaliano kwa sababu tatu:

Kwanza: kuimarisha sura ya Saudi Arabia, na pili: kuondoa fedheha ya kimataifa kutoka kwa Saudi Arabia
na kuifinika kadhia ya mwanahabari wa Saudia, na tatu: kuitishia Saudi Arabia kifedha! Hili ni muhimu zaidi
kwa Trump … kwa yakini Amerika haitaki kuimarisha sura hiyo na kuondoa fedheha machoni mwa vibaraka
wake Mohammed Bin Salman na babake, lakini kwa kitendo hiki itaonekana kuwaokoa wote wawili kutokana na “balaa” na kisha kuipatiliza katika “kuifyonza” pesa zaidi kutoka katika mafuta ya Saudia kama thamani ya kuiondoa fedheha ya kimataifa kutoka kwao, na hili linaafikiana na fikra ya “upapiaji” wa kibiashara ya Trump iliyo jengwa juu ya sera ya “tulipe”!

3- Kinacho ashiria maslahi haya ya Amerika katika kufanya makubaliano hayo ni kile kinachotolewa na
maafisa nchini Amerika pamoja na kutunga mamlaka ya kile kilichotolewa, ikiwemo:

“Amerika imetoa wito wa kusitisha vita nchini Yemen ndani ya siku 30, ikisisitiza haja ya kukomesha
muungano wa Waarabu ukiongozwa na Saudi Arabia, kupiga mabomu maeneo ya wakaazi nchini Yemen.
Waziri wa Ulinzi James Matisse alitoa wito kwa pande zote za mzozo wa Yemen kusitisha vita ndani ya siku 30, Na kuingia katika majadiliano ya umakinifu ili kumaliza vita nchini humo. Matisse alisema, wakati wa hotuba yake katika warsha iliyo andaliwa na Taasisi ya Amani ya Amerika jijini Washington, mnamo Jumanne: (“Kwa ajili ya suluhisho la muda mrefu tunataka kusitishwa kwa vita, kuondoka kutoka mpakani, na kusitishwa kwa mabomu ya angani … Pande zote husika katika mzozo nchini Yemen zinapaswa kuketi katika meza ya majadiliano katika siku 30 zijazo.” Alisisitiza kuwa “pande zinazo pigana nchini Yemen ni lazima zisonge mbele kuelekea juhudi za Amani,” aliendelea kusema kuwa: “Tunahitaji kufanya hivyo katika siku thalathini zijazo, na nadhani kuwa Saudi Arabia na Imarati ziko tayari kuendelea na jambo hilo.” (Gulf Online, 10/31/2018)

– Amerika ilimtuma Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres kuhudhuria majadiliano ya Sweden na kuwatia shinikizo wajumbe wanaojadiliana ili kuhakikisha kufikia makubaliano au mwanzo wa makubaliano,
na kutomuachia mambo Balozi wa Kimataifa wa Uingereza Griffith: “Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo ya mwisho nchini Sweden kwa usadizi wa juhudi za balozi wake wa amani nchini Yemen ili kuanza mchakato wa kisiasa kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa takriban miaka minne.” (Reuters, 12/12/2018).

– Shinikizo la Saudi Arabia juu ya Raisi Hadi wa Yemen ili  kukubali makubaliano yaliyo wasilishwa: duru ziliiambia Al-Jazeera kuwa Saudi Arabia ilimlazimisha Raisi wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi ili kuongoza ujumbe wa serikali ya Yemen katika majadiliano ya Sweden ili kukubali makubaliano ya kusitisha vita katika mji wa Hodeidah na bandari zake. Duru hizo ziliripoti kuwa ujumbe wa serikali uliwasilisha waraka kwa Hadi, “anayeishi Riyadh”, ukipendekeza kutotia saini makubaliano hayo kwa sababu hayaelezi wazi wazi kuwa Mahouthi wataondoka mji wa Hodeidah na bandari zake, lakini raisi wa Yemen akaelekezwa kuyatia saini baada ya shinikizo kali kutoka kwa Saudi Arabia katika masaa machache yaliyopita, kwa mujibu wa duru hiyo (AlJazeera.net 13/12/2018)

– Uteuzi haraka wa Jenerali wa UN ili kusimamia kusitisha vita mjini Hodeidah: “Umoja wa Mataifa,
ulimchagua jenerali wa Kiholanzi, ili kuongoza misheni ya usitishaji vita baina ya pande zote za Yemen. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Martin Griffith, alisema jenerali huyo mstaafu wa Kiholanzi, Patrick Cammaert, alikuwa amekubali kuongoza misheni ya usimamizi nchini Yemen na kuongeza kuwa Cammaert huenda akawasili eneo hilo katika muda wa siku chache.” (Yemen News, 14/12/2018). Tovuti ya maoni ya Yemen mnamo 20/12/2018 ilichapisha: “Msemaji rasmi wa UN Stephane Dujarric amesema, mwenyekiti wa kamati, jenerali mstaafu wa Kiholanzi Patrick atasafiri hadi Jordan kesho mnamo Alhamisi, kisha hadi Sanaa na kutoka huko hadi Hodeidah …” – Amerika kuyakaribisha hadharani makubaliano hayo.
Waziri wa Kigeni wa Amerika, Pompeo aliyakaribisha makubaliano hayo, akisema kuwa: “Amani inawezekana nchini Yemen” (Shirika la habari la BBC 14/12/2018). Alisema katika taarifa: “Mashauriano haya kati ya Jamhuri ya Serikali ya Yemen na Mahouthi yameashiria hatua ya kwanza muhimu … Amani inawezekana. Pande zote zina fursa ya kujenga juu ya ari hii na kuimarisha maisha ya watu wote wa Yemen na kusonga mbele, wote ni lazima waendelee kuwasiliana, kuzima taharuki, na kusitisha uhasama unaoendelea.” (Yemeni Scene, 14/12/2018)

– Mawasiliano thabiti ya Balozi wa Amerika na Mahouthi: “Balozi wa Amerika nchini Yemen, Matthew Toller,
alisema wakati wa uhudhuriaji wake katika kongamano na majadiliano jijini Stockholm: “Tulifanya mkutano rasmi baina ya mabalozi na kundi, akiwemo mwanachama wa ujumbe wa Houthi … Kivyangu nilikuwa na mawasiliano na baadhi ya watu katika timu ya Mahouthi katika sehemu walioisifu kuwa nzuri, hakika ni mkutano mzuri.” Aliulizwa kama mkutano huo pamoja nao ulikuwa wa moja kwa moja na rasmi, alisema: “Mkutano wowote ninaofanya ni rasmi, Mimi ndiye balozi wa Amerika nchini Yemen masaa 24 kwa siku” (Saudi Arabia, Middle East, Arab News 13/12/2018).

Nne: Ingawa makubaliano hayo ya Sweden yalikuwa  chini ya shinikizo la Amerika na kisha kuyakaribisha
kama tulivyosema juu, Uingereza vilevile iliyakaribisha kwa sababu Amerika ilijenga rai jumla yenye shinikizo
kubwa kuhusu malengo ya kibinadamu na majanga ya baa la njaa nchini Yemen na maradhi ya watoto kutokana na vita na wafu na majeruhi nk…, kana kwamba mambo haya yamezuka leo! Hivyo basi, mazingira
yaliyo jengwa na Amerika ili kutamatisha makubaliano hayo hayakuacha khiari kwa Uingereza isipokuwa
kuyakaribisha, lakini kwa njia yake ya kusukuma wimbi la kubadilisha kituo chake au angaa kupunguza kasi yake, iliyakaribisha makubaliano hayo: Wizara ya Kigeni ya Uingereza mnamo Jumanne, ilikaribisha usitishaji vita nchini Yemen … Waziri wa Kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt alisifu juhudi za Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Martin Griffith, katika nukuu ya tweet katika mtandao wa Twitter wa Afisi ya Kigeni ya Uingereza … (Chanzo: Yemen Net 18/12/2018)

Wakati huo huo ilisalimisha azimio kielelezo kwa Baraza la Usalama ili kujadili makubaliano hayo kwa kisingizio cha namna ya kuyatekeleza:

“Uingereza inatafuta azimio jengine la Baraza la Usalama la UN na kuwasilisha azimio kielelezo kwa Baraza hilo kwa ajili ya mazungumzo,” Mjumbe wa Uingereza katika UN Karen Pierce alisema: “Kama mshikiliaji faili ya Yemen katika Baraza hilo la UN, Uingereza itaregelea kufanya kazi na wandani wote katika azimio la Baraza la Usalama ili kuidhinisha makubaliano hayo yaliyofikiwa na pande zote, kusaidia utekelezwaji wake na kuwezesha Umoja wa Mataifa kusimamia utekelezaji kwa pande zote na kuweka hatua nyengine za haraka.” (Tovuti ya Vijana wa Yemen ikinukuu tovuti ya serikali ya Uingereza, 14/12/2018).

– Mnamo Jumanne, mabalozi walisema: Baraza la Usalama la UN inalichunguza azimio kielelezo la
Uingereza linalomtaka Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kusalimisha mapendekezo kufikia mwishoni
mwa mwezi huu juu ya namna ya kusimamia usitishaji vita mjini Hodeidah, na Uingereza imesambaza azimio hilo kielelezo ili kuunga mkono makubaliano hayo katika Baraza la Usalama. Haijulikani lini litapigiwa kura, ambapo azimio hilo lahitaji kura 9 kulipitisha na hakuna matumizi ya haki ya kura ya turufu kwa Amerika wala Ufaransa wala Uingereza wala China wala Urusi … (AlAin News, 18/12/2018)

Uingereza iliwasilisha mradi huu kama udhuru wake ili kuhusishwa katika makubaliano hayo kwa kisingizio
cha namna ya kudhibiti na kutekeleza na kujiondoa, kurefusha, ili pande zinazo zozana katika biladi ya
Yemen zisiwe na wasiwasi kuhusu idadi ya wanaofariki katika watu wake na kiwango cha uharibifu katika
majengo yake bali maslahi yao yapatikane. Hivyo basi, twaweza kusema:

Amerika na washirika wake katika eneo hilo, hususan Saudi Arabia, wako makini kuhusu kumaliza vita vya
Yemen leo na kuongoza majadiliano yanayopelekea
kupata hisa kubwa ya utawala wa Yemen kwa Mahouthi,
wafuasi wa Iran na hivyo basi wafuasi wa Amerika.
Umakinifu wa hili ulionekana kupitia kufanya majadiliano
ya Sweden. Lakini mwelekeo huu wa Amerika
haumaanishi kuwa Amerika yaweza kuupata chini ya
ushawishi wa Uingereza nchini Yemen. Uingereza
ilimtuma Waziri wake wa Kigeni kwenye majadiliano
ya Sweden mnamo 13/12/2018 ili kumsaidia mjumbe
wake wa kimataifa Griffith mbele ya Raisi wake Guterch,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa; hii ndio sababu
makubaliano hayo yalifungika kwa Hodeidah pekee, na
faili nyenginezo, hususan uwanja wa ndege wa Sanaa,
ziliakhirishwa kwa raundi za mbeleni. Vile vile misimamo
ya ujumbe wa serikali ilikuwa na shauku ya utekelezwaji
wa yale yalioafikiwa, ikiashiria kuwa ilikuwa chini ya
shinikizo la Saudi Arabia na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, na Amerika nyuma yao.

Al-Yamani alisema wakati wa mkutano wa waandishi habari uliofanywa katika tamati ya majadiliano katika
mji wa Sweden wa Rimbo kuwa serikali ya Yemen ilikamilisha makubaliano 75 pamoja na Mahouthi, lakini
hawakujifunga nayo. Aliwatuhumu Mahouthi kukataa kuondoa mzingiro wao wa mji wa Taiz … Kuhusiana na
faili ya uwanja wa ndege wa Sanaa, al-Yamani alisema kuwa serikali ilikuwa tayari kuufungua kwa safari za
ndege za kimataifa kupitia uwanja wa ndege wa Aden, lakini Mahouthi wakakataa mpango huu. Al-Yamani
alisema kuwa “mradi wa kumaliza mapinduzi haya unaanza na Hodeidah.” Alisema Umoja wa Mataifa na
jumuia ya kimataifa zinabeba masuliya ya kuwalazimisha Mahouthi kutekeleza makubaliano hayo juu ya Hodeidah na ubadilishanaji wa wafungwa … Akichangia tangazo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres la mipango ya kufanya raundi mpya, alisema: “Raundi mpya za mashauriano hazipaswi kufikiriwa isipokuwa hii ya sasa iliyo afikiwa itekelezwe.” (Russia Today, 13/12/2018). Yote haya yanafungua mlango wa kukiuka pakubwa makubaliano haya wakati wa utekelezaji wake na kuchelewesha kufanya raundi nyenginezo. Hivyo basi, inatarajiwa kuwa utekelezaji wa makubaliano ya Hodeidah utakuwa mgumu, kama ilivyo ashiriwa na ghasia zilizotokea mnamo 14 na 15 na 16/12/2018 pambizoni mwa mji wa Hodeidah, muda mfupi baada ya tangazo la makubaliano ya Sweden, ambapo Umoja wa Mataifa ulilazimika kuyahalalisha: duru ya UN ilisema: “Huku Makubaliano ya Hodeidah yakieleza kusitishwa kwa vita mara moja, ni kawaida kwa kadhia kuchukua masaa 48 au 72 kwa maagizo kutekelezwa uwanjani … Tunatarajia kuwa usitishaji vita hivyo utabikishwa kuanzia Jumanne.” (Reuters, 16/12/2018)

Hivyo basi, inatarajiwa kwa hali kwenda mbele na nyumba. Kwa upande mmoja, Amerika inataka kufunga
mandhari ya kijeshi, hususan mjini Hodeidah na bandari zake, na kisha kuendelea na suluhisho za kisiasa pamoja na kudumu kwa “sauti” ya Mahouthi yaani Hodeidah. Kwa upande wa Uingereza, kuna visingizio vya kuendelea na vita ili kufikia kwa kadri iwezekano kuwadhoofisha Mahouthi na kuwanyamazisha mjini Hodeidah kabla ya kuelekea katika suluhisho la kisiasa.

Tano: Ama kuhusu swali la mwisho (na je inatarajiwa kuwa makubaliano haya yatamaliza mgogoro wa
Yemen?) Ni kama ifuatavyo:

Makubaliano haya hayatatui mgogoro huu nchini Yemen kutokana na mgongano wa maslahi ya Amerika na
Uingereza na ala zao za kieneo walioyatia saini. Matokeo yake makubwa ni kuleta tu baadhi ya utulivu kama
mapumziko kwa mpiganaji na kisha mambo yatachemka tena, na huenda kwa njia ya warasilimali yakajumuisha maridhiano kama kanuni inayo shirikianwa na pande zote mbili kwa mujibu wa mizani ya nguvu za pande zote mbili. Na bila shaka, hili halimalizi mgogoro huo; yaani, matukio nchini Yemen yataendelea kupanda na kushuka, kupoa, na kisha kuwaka tena kwa mujibu wa mizani ya nguvu za kisiasa na kijeshi katika mzozo huo. Kitakacho umaliza ni moja ya mambo mawili kama ilivyo tajwa
katika matoleo yaliyo tangulia:

Kwanza ni kuwa Amerika au Uingereza yaweza kutatua mambo kwa manufaa yake na kutawala ushawishi nchini Yemen. Hili liko mbali na kupatikana, kama ambavyo tayari tushafafanua.

Pili liko karibu kwa idhini ya Allah kuwa Allah ataukirimu Umma huu kwa Khilafah, ili ushawishi wa makafiri na wakoloni hawa ung’olewe kutoka katika biladi hii na maovu yao yaondolewe miongoni mwa watu. Na ili ukafiri na watu wake wafedheheshwe na Uislamu na Waislamu wafate izza na waumini wafurahie ushindi wa Allah:

وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

بِنَصۡرِ ٱللَّهِۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

َِ“Na siku hiyo waumini watafurahi kwa nusra ya Allah. Humnusuru Amtakaye na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa rehma” [Ar-Rum: 4-5]

Na watu wa Yemen, watu wa Iman na hekima, ni lazima watathmini jambo hili ili washinde duniani na akhera, na Allah ndiye msaidizi wa watu wema.

13 Rabii’ al-Al-Akhar 1440 H
20/12/2018 M

Maoni hayajaruhusiwa.