Kwenda Peponi Na Motoni Kwa Pamoja

Kwa kutokuwepo dola ya kiislamu ya kiulimwengu khilafah watu wengi katika waislamu wanafanya vitendo vingi vya kuwaingiza peponi na motoni, kwa wakati mmoja.

Bila ya shaka hili ni jambo la kushangaza ukilisikia. Vyema nitakupeni ufafanuzi.

Muislamu anaswali, anafunga, anasoma Qur’an, anatoa sadaka, anatoa zaka, anatembelea mgonjwa, anakirimu wageni, anakwenda hijja,…… bila ya shaka anafanya vitendo hivi kuajili ya kwenda peponi. Lakini wakati huo huo anakula mali ya mayatima, anakula riba, anakula mirathi, anapiga kura kuchagua watu wanaotunga sheria kinyume na sheria za Allah, anawaunga mkono waovu, anawatenga wazazi wake na kubwa zaidi anafanya kitendo ambacho kinafuta mema yote ambacho bila shaka ni ushirikina.

(وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ)

“Hakika tumekufunulia na wale waliopita kabla yake ya kuwa ukishirika vitendo (vyako vyema vyote) Vitaporomoka na utakuwa ni katika waliokula hasara” [Surat Az-Zumar 65]

Kwa vitendo hivyo vyema anavyovifanya bila shaka ukimuuliza atakwambia anataka pepo. Lakini kimaumbile  anafanya vitendo vya kuingia peponi na vitendo vya kuingia motoni kwa wakati mmoja.

Lakini wapi mja huyu ataingia kiuhakika.!? Kati ya peponi na motoni. Ikiwa mtu huyu ataendelea na hali hii ataingia motoni kwa sababu peponi haingii Isipokuwa mwenye kufanya matendo kwa ikhlasi. Kwani matendo mema Kuna kuswihi ambako kunapatikana kwa kuyafanya kwa usahihi matendo hayo, na usahihi ambao unapatikana kwa kusoma, na Kuna kukubalika kwa hayo matendo mema ambako kunahitaji ikhlasi (kufanya kwa ajili ya Allah peke yake). Na wanaofanya mema kwa ikhlasi ni wachache na Allah tu ndio anawajua. Na kwenda peponi kunahitaji matendo yenye ikhlasi peke yake. Na hakuna mja anaejua kuwa vitendo vyake vimekubalika ijapokuwa waja wapo wanaoujua vitendo vyao vimesihi kwakuwa Wamevifanya kwa usahihi.

Ama kwenda motoni hakuna zaidi ya matendo Maovu. Na matendo Maovu ni muovu tu ukufanya umefanya. Na moto unakubali hata matendo yaliyochanganywa mema na maovu.

Lakini mpaka mtu aende peponi na hali ya kuwa anafanya vitendo vinavyompeleka motoni ni juu yake kuleta toba ya kikweli kweli, na kujiepusha na madhambi na kuzidisha sana kufanya matendo ya kheri. Kama alivyosema Allah peke yake.

(وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ)
“Na Simamisha swala Katika ncha mbili za mchana na sehemu Katika usiku, Hakika mema hufuta Maovu, na huo ni ukumbusho kwa wenye kukumbuka” [Surat Hud 114]

Na kwa kufanya hivyo huenda Allah akampa pepo kwa rehema zake.

Ama kuendelea na kufanya vitendo vya kumpeleka mtu motoni na peponi kwa pamoja. Hakika mafikio ya mtu kama huyo ni motoni na Mwenyezi Mungu  ni mjuzi zaidi.

Ujumbe.
Kwa vyovyote vile Muislamu hapaswi kujiaminisha na moto kwa Allah katika mazingira haya ambayo Maovu yanaamrishwa na serikali za kikafiri na mema yanapigwa vita.

Na pia hakuna kujiaminisha na mema unayofanya kuwa lazima utaenda peponi kwa kuwa hakuna anaejua kuwa mema yake yanakubalika.

Pia muislamu hapaswi kujikatia tamaa kwa matendo yake maovu anayoyafanya, Bali anapaswa akithirishe kufanya mema na kubwa zaidi kutaka msamaha zaidi kwani Allah huwa hawaadhibu wenye kufanya toba ya kweli.

(وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنْتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ)
“Na haiwezi kutokea Allah kuwaadhibu na wewe ukiwa pamoja nao, na Allah sio mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba msamaha” [Surat Al-Anfal 33]

Na Sheikh Khatibu Imran Abuu khaliil

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Maoni hayajaruhusiwa.