Kupunguza Umasikini Chini ya Ubepari ni Ndoto

Mnamo tarehe 10 mwezi wa 9 mwaka 2018, waziri mkuu Iran Khan alidokeza wakati wa uzinduzi wa mradi wake wa upunguzaji wa umasikini ndani siku saba hadi kumi unaolenga kuwatoa wananchi  katika umasikini.” Mradi wa upunguzaji wa umasikini utakua ni muhimu zaidi katika siku mia moja za serikali ya PTI utakaotajwa mbele ya watu wa Pakistani katika masiku machache yajayo” Imran Khan alisema.

Upunguzaji wa makali ya umasikini hauwezekani chini ya uchumi wa kibepari. Ubepari umejengwa katika imani ya kwamba rasilimali zilizopo hazitoshi kukidhi mahitaji ya watu wote. Kutokana na msingi huu, katika jamii ni lazima kuna watu watabakia na njaa kali, ukosefu wa makazi, na uwezekano wa ukosefu huduma za kiafya, elimu na usafiri kwa ujumla. Ubepari unahifadhi hilo kama ndio njia pekee ya kupunguza tabaka kati ya mahitaji na rasilimali, kwa kuongeza uzalishaji. Hivyo ubepari unafanya kazi ya uzalishaji halafu hutumia ugawaji kama mbinu.” wanachomaanisha ni kwamba pindi ndoo ya maji ikijaa basi maji yatamwagika na kuwafikia wenye kiu. Wakati ambao uhalisia wa uchumi wa dunia unaonyesha kwamba, ndoo haijai , hata ijazwe kiasi gani. Dunia imekusanya GDP za kufikia 87.51 trilion za Kimarekani ndani ya mwaka 2018, lakin nusu ya utajiri huu unamilikiwa na matajiri kutoka Credit  Suisse  Group. Imenukuu kwamba, makampuni ya fedha yanayoongoza, matajiri wa ulimwengu 1% wanamiliki nusu ya utajiri wa ulimwengu ikitazamia ukubwa mwanya uliiopo kati ya matajiri na watu wengine. Hata wakati wa mgogoro wa kiuchumi bado matajiri wanazidi kuwa matajiri zaidi, na masikini wanazidi kuwa masikini zaidi . Hivyo katika kila nchi ambayo imaukubali ubepari, iwe ni nchi kubwa kama   US,  Britain,  France na   China,  au nyingine kama   Pakistan,  Egypt  na  India,  tunaona ongezeko kubwa la masikin. Kulingana na ripoti za hivi punde kutoka taasisi ya   Brookings  Institution,  Nigeria  imeipita  India  mwezi wa 5 2018 kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao ni masikini kupindikia. Hii inatokea wakati Nigeria  ni nchi ya sita kwa uzalishaji mafuta katika duni. Hivyo mawakala wa ubepari hudai kwamba wanajaribu kupnguza umasikini lakini ni kinyume chake.

Ahadi yoyote ya kupunguza umasikini bila kuondoa mfumo wa kiuchumi wa ubepari ni uongo . Mpaka iwe mfumo wa uchumi wa kiislamu utabikishwe. Na kuondosha  uchumi katika mikono ya wachache. Mfumo wa kiuchumi wa kiislamu unaona kwamba changamoto za kiuchumi  zinatokana na mgawanyo wake kama   Allah  (swt)  asemavyo, ﴾ مكنم ءاينغلْا نيب ةلود نوكي لَ يك ﴿

“hivyo basi mali izunguke baina yenu”

(Al-Hashar:  7). 

Uislamu haulengi kupunguza umasikini bali kuumaliza kabisa .  Mtume (saaw) asema:

مهيف حبصأ ةصرع لهأ  اميأو « » ىلاعت هللا ةمذ مهنم تئرب دقف عئاج ؤرما

“sehemu yoyote ikiwa watu wataamka asubuhi na miongoni mwao yupo mtu mwenye njaa basi watu hao wataondolewa katika ulinzi wa Allah.” (imesimuliwa na  Ahmad kutoka kwa ibn Umar,  na ni sahihi kwa mapokezi ya Ahmad  Shakir). 

Hizb  ut  Tahrir  katika kitabu chake  “muhtasari wa katiba”  imetabaniwa katika ukurasa  124,  “tatizo msingi la mdodoro wa uchumi ni ugawawaji wake  na mnufaiko kwa wananchi wote, na namna ya uyeyeushaji wa utajiri huo na kunufaisha”.”  katika ukurasa   125, imenukuliwa ,  “ni lazima kuhakikisha kwamba watu wote wanapata huduma msingi , na kuhakikisha kwamba kila mtu anatosheka na mahitaji mengine kwa kiwango cha juu kinachowezekana” Hivyo ni mfumo wa kiuchumi wa kiislamu pekee ndio waweza kuondoa umasikini  na khilafah ijayo kupitia njia ya utume itaweza hilo kwa ubora wa kiwango.

#UislamuNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.