Kunufaika na Najisi

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh…

Je inafaa kuchukua jeni ya nguruwe kwa mfano jeni ya ukuaji na kuiweka katika chakula halali mfano matango kwa ajili ya ukuaji..? 

Jawabu:

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh

Kuchukua jeni za ngurue, kuziweka kwenye mimea ili kuongeza ukuaji wake, kama vile kuzitumia katika ukuaji wa matango na vyenginevyo, hili halifai. Na ni kwasababu ya dalili zifuatazo:

-Nguruwe ni haramu na ni najisi kwa dalili zifuatazo:

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

“Hakika mumeharamishiwa nyamafu, damu, nyama ya ngurue na kilichochinjwa si kwa ajili ya Allah basi mwenye kulazimika bila kutamani wala kupita kiasi huyo hana madhani, hakika Allah ni mwingi wa kusamehe mwenye kurehemu”  TMQ Bakara:173

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ

“Mumeharamishiwa nyamafu, damu, nyama ya ngurue, na kilichochinjwa si kwa ajili ya Allah…”  TMQ Maida: 3

-Ametoa Tabarani katika Al-Kabiir kutoka kwa Abi Tha’alaba Al-Khushani, amesema: Nilimwendea Mtume (SAW) nikamwambia ewe Mjumbe wa Allah: Na mimi nipo kwenye ardhi ya ahlulkitaab na wao wanakula katika vyombo vyao nguruwe na wananywea ulevi, je nile katika vyombo hivyo na ninywe…? Kisha Mtume (SAW) akasema: “…na ukipata vyombo vyengine, usile katika vyombo vya makafiri na kama hukupata basi vikoshe hivyo (vya makafiri) kwa maji sana, kisha kulia humo”, yaani ukivihitaja na ukiwa hukupata vyengine, vikoshe vizuri, haya yanatoa dalili kuwa ulevi na ngurue ni najisi kwa kuwa vinahitaji kukoshwa ili kuvitahirisha.

Na katika riwaya ya Daruqutny anataja Mtume (SAW) kuwa kuvikosha kwa maji ndio tohara yake, nayo ni dalili ya wazi juu ya unajisi wa nguruwe na ulevi. Na hii hapa riwaya ya Daruqutny: Ametuhadithia Husain ibn Ismail, ametueleza Said ibn Yahya Al-Umawi, ametueleza Abdul-Rahim ibn Sulaiman, kutoka kwa Al-Hajaj ibn Artwa, kutoka kwa Makhuul, kutoka kwa Abi Idris, kutoka kwa Al-Hushany, amesema: Nilimwambia: Ewe Mjumbe wa Allah hakika sisi tunachanganyika na washirikina na hatuna vyungu wala vyombo vyengine visivyokuwa vyao, kasema: Akasema:

سْتَغْنُوا عَنْهَا مَا اسْتَطَعْتُمْ فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا فَارْحَضُوهَا بِالْمَاءِ فَإِنَّ الْمَاءَ طَهُورُهَا ثُمَّ اطْبُخُوا فِيهَا

“Jitengeni navyo kadri muwezavyo, kama hamkupata (vyengine), vikosheni kwa maji, kwani hakika ya maji ndio tohara yake, kisha vipikieni”. Hii ni nass ya wazi kwamba ulevi na nguruwe ni katika najisi, kwani Mtume (SAW) anasema:

فَإِنَّ الْمَاءَ طَهُورُهَا

Hakika ya maji ndio tohara yake”.

-Ametoa Bukhar kutoka kwa Jabir ibn Abdillah (RA), hakika yake amemsikia Mtume (SAW) akisema katika mwaka wa Ufunguzi wa Makkah na yeye yuko Makkah

إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الْخَمْرِ وَالْمَيْتَةِ وَالْخِنْزِيرِ وَالْأَصْنَامِ فَقِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَأَيْتَ شُحُومَ الْمَيْتَةِ فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ وَيُدْهَنُ بِهَا الْجُلُودُ وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ فَقَالَ لَا هُوَ حَرَامٌ ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ ذَلِكَ قَاتَلَ اللَّهُ الْيَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ ثُمَّ بَاعُوهُ فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ

“Hakika ya Allah na Mjumbe wameharamisha kuuza ulevi, nyamafu, nguruwe, masanamu, pakasemwa ewe Mjumbe wa Allah waonaje  shahamu  ya nyamafu kwani hupakwa kwenye Marikebu, na hupakwa kama mafuta kwenye ngozi, na watu hutumia kama nishati ya kuwashia, akasema hapana, hiyo ni haramu, kisha akasema Mjumbe wa Allah (SAW) hapo, awaangamize Allah mayahudi hakika Allah alipoharamisha shahamu yake (nyamafu) wao wakaitengeneza vizuri kisha wakaiuza wakala kipato chake (thaman).” 

-Na akatoa Muslim kutoka kwa Ibn Abass, amesema, Umar ilimfikia kuwa Samura ameuza ulevi, akasema: Allah amuangamize Samura, kwani hajui kwamba Mjumbe wa Allah (SAW) amesema:

لَعَنَ اللهُ الْيَهُودَ، حُرِّمَتْ عَلَيْهِمُ الشُّحُومُ، فَجَمَلُوهَا، فَبَاعُوهَا

Allah amewalani mayahudi wameharamishiwa shahamu  wao wakaitengeneza vizuri kisha wakaiuza”. 

-Na ametoa Abu Daud kutoka kwa Abi Zinad, kutoka kwa Al-A’araj, kutoka kwa Abi Huraira, kwamba Mjumbe wa Allah (SAW) amesema:

إنَّ اللَّهَ حَرَّمَ الْخَمْرَ وَثَمَنَهَا، وَحَرَّمَ الْمَيْتَةَ وَثَمَنَهَا، وَحَرَّمَ الْخِنْزِيرَ وَثَمَنَهُ

“Hakika Allah ameharamisha ulevi na thamani yake, na ameharamisha nyamafu na thamani yake, na ameharamisha nguruwe na thamani yake”.

Na dalili hizi zinabainisha uharamu wa kunufaika na najisi, kwahiyo, haifai kuchukua jeni kutoka nguruwe na kuiweka kwenye mimea ili kuongeza ukuaji wake, kama vile kuitumia (jeni) katika kukuza matango na vyenginevyo. Hilo halifai kwa ule uharamu wa kunufaika na najisi.

Wala hapasemwi hakika hii ni kama dawa ambayo inafaa kutumia najisi pamoja na kuwa karaha, (hapasemwi hivyo) kwa yale aliyoyapokea Bukhar  kwa njia ya Anas (RA):

أَنَّ نَاسًا مِنْ عُرَيْنَةَ اجْتَوَوْا الْمَدِينَةَ فَرَخَّصَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ أَنْ يَأْتُوا إِبِلَ الصَّدَقَةِ فَيَشْرَبُوا مِنْ أَلْبَانِهَا وَأَبْوَالِهَا..

“Hakika watu kutoka Uraina waliuchukia mji, Mjumbe wa Allah akawaruhusu wende kwa ngamia wa sadaka wanywe maziwa yake na mkojo wake…”  Hapasemwi hivyo kwasababu kukuza mimea hakuwi katika maana ya neno dawa. Kwahivyo, haifai kutumia jeni kutoka nguruwe ili kukuza mimea.

Maoni hayajaruhusiwa.