Kukhitimisha Kampeni ya Rabiul Awwal 1440H

Baada ya kuwa katika kampeni ya Rabi ul awwal, mwezi aliozaliwa Mtume wetu SAAW kwa kipindi cha mwezi mzima, leo tumekhitimisha rasmi kampeni hiyo.

Tunawashukuru Waislamu wote tulioshirikiana nao katika hali moja au nyengine katika kampeni hiyo kwa kipindi chote cha mwezi mzima.

Aidha, tunakumbushana kuwa asili suala la kuonesha Nuru ya Mtume SAAW ni jambo la wakati wote, licha ya kuwa katika mwezi wa Rabi ul Awwal huwa tunazidisha zaidi. Hivyo tuendelee kuonesha jambo hilo wakati wote, kwa jambo hilo ni sehemu ya kuulingania Uislamu.

Mwisho tunamuomba Allah Taala atupe tawfiq na malipo makubwa kwa kampeni tuliyofanya, pia kampeni hiyo iwe chanzo cha nusra kwa Umma wetu Mashariki na Magharibi.
#MuhammadNiNuruKwaUlimwengu

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

29 Rabiul Awwal 1440 AH
07 Disemba 2018 Miladia

Maoni hayajaruhusiwa.