Kujifanya Upo Huru, Hakukufanyi Uwe Huru

ﺑﺴﻢ ﷲ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

Habari
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Irani haitasalimu amri kwa Marekani na itaendelea na malengo yake hata kama itashambuliwa (Aljazeera).

Kauli ya Rais Rouhani haina tofauti na wengi katika watangulizi wake na yeye ni kibararka mkubwa Zaidi ya wote waliotangulia. Ambao ni vibaraka kama yeye. Anachoshindwa kuona ni kwamba dhiki na tabu zinazowasibu watu wao huishia na kwao kadhalika Mifano ya Iraq na Libya bado ni mifano ya kukumbukwa, au ndoto za rouhani zenye mwisho tofauti ambazo hufata mtindo ule ule simulizi za vibaraka hawa ni hivi kila aliyopo hujiona anaakili zaidi kuliko kibaraka mwenzake aliepita.

Iran inajionyesha kuwa inanguvu za kutosha za kupambana na Marekani, wakati ambapo imekua ikifanya kazi kwa ajili ya maslahi ya US kama inavyofanya Syria kuilinda dola ya kikatili ya Bashar Al-Assad. kwa miaka kadhaa, Iran imekua ikifanya kazi kwa ajili ya maslahi ya Marekani huku ikiendelea kukanusha. Imekua ikicheza michezo michafu huko Syria, Iraq na Yemen. Kama makubaliano kati ya Iran na utawala wa Obama ilikua ni kuisaidia Iran kutekeleza maslahi ya Marekani, sasa sera mpya za Trump ni kuonuesha tu nguvu. Saudi arabia, Uturuki, na Iran wamecheza karata nzuri kwa kuwaangamiza mapinduzi ya wasiyria na namna ambavyo Marekani anachezesha huu mchezo ni kama “kuwaimarisha vibaraka wake”. Fikra yoyote kuhusu dola ya kiislamu ni kama hukmu ya adhabu ya kifo kwa Marekani na washirika wake na ndio wanafanya kazi kwa pamoja kuhakiksha haisimami, wao wenyewe wana migogoro yao ya kugombea uongozi na uroho wa mali na hilo ndilo huwafanya watofautiane wao kwa wao na muda huu ndio wamagharibi hucheza karata ya kitisho cha vita kwa nchi za waislamu na viongozi vibaraka wanatumia karata ya “oh tunalengwa kwakua tumesimama kwenye misimamo yetu”. Ambacho hawakijui ni kwamba wanacheza na moto ambao utawapeleka katika moto wa jahannam.

Wakati Iran na Uturuki wanacheza kama waasi kwa bwana zao, Saudi Arabia imesahau zamani hata kujifanya inapingana na marekani. Huu ndo muda ambao ummah wa kiislamu watakiwa kujua kua hawa wasanii namna wanavyocheza na kuwataka waache kujifanya wanawakilisha fikra na hisia za waislamu. Waislamu wakatae kudanganywa na na hawa viongozi waongo ambao hawaoni aibu kutumia uislamu kama mbinu ya kufikia malengo yao. Uislamu sio jambo la “kuchagua” kwa hakika, ni fardhi inayotakiwa kukubaliwa kutabikishwa na kubebwa kama mfumo kamili wa maisha.

Kupinga ukafiri sio tu wakati unakwenda kinyume na maslahi yako, lakini kumlinda mtoto mmoja wa Syria asife kwa njaa na ambae nyumba yao imeharibiwa na wazazi wake wamechinjwa. Kupambana na makafiri ni kumpigania jirani yako pindi unapoona Marekani anavamia nchi ya ndugu yako. Kusimama kwa ajili ya kuikomboa Aqsa. Sisi waislamu lazima tuwe tayari kuzuia uvamizi wowote katka ardhi ya waislamu na kumrejesha kila moja ambayo tuliporwa na makafiri, lakini hili litawezekana tu endapo tutakua na ngao ya khilafah kwaajili ya kutulinda na kutuongoza. Dola ya khilafah itatokomeza uchu wa utashi wa Marekani kwa mafuta ya mashariki ya kati. Itakua na usimamizi wa kutosha kuanzia Hormuz na haitakubali meli yoyote ya kigeni maeneo hayo.
( ﻳَﻘُﻮﻟُﻮﻥَ ﺑِﺄَﻓْﻮَﺍﻫِﻬِﻢ ﻣَّﺎ ﻟَﻴْﺲَ ﻓِﻲ ﻗُﻠُﻮﺑِﻬِﻢْ ﻭَﺍﻟﻠّﻪُ ﺃَﻋْﻠَﻢُ ﺑِﻤَﺎ ﻳَﻜْﺘُﻤُﻮﻥَ )
“wanasema kwa midomo yao yasiokua katika nyoyo zao na Allah anajua vizuri wanayoyaficha” [3:167]

Imeandikwa kwenda Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Na Ikhlaq Jehan

Kwa hisani: http://www.hizb-ut-tahrir.info/…/20…/news-comment/17560.html

Maoni hayajaruhusiwa.