Kataa Ushoga Na ‘Mapenzi Ya Jinsia Moja’

بسم الله الرحمن الرحيم

Matendo maovu yanayoitwa mapenzi ya jinsia moja ni mojawapo ya madhambi makubwa na makongwe hapa duniani. Historia inaonesha yalianza kufanyika kipindi cha Nabii Lut (As.) na Mwenyezi Mungu akaangamiza jamii iliyokuwa ikiyatenda.

Zilipita karne nyingi uchafu huo ukawa haupo au kupungua kwa kiasi kikubwa na ulikemewa vikali mpaka baada ya kuibuka mfumo wa kidemokrasia katika Ulaya magharibi ndani ya karne ya 17 na kuenea kwa fikra za uhuru binafsi ya kuwa mtu ana uhuru wa kutumia mwili wake anavyotaka yeye mwenyewe. Hapo uchafu na uovu huo ukaanza kuibuka hatua baada ya hatua.

Kidogo kidogo jamii hasa za Ulaya na Marekani zikapokea uovu huo japo awali kwa kificho na kuanza kulizoesha, kuupigia debe na kisha kuzilazimisha nchi changa kiasi cha baadhi ya nchi kuanza kuupokea na kukua kwa kasi mwanzoni mwa miaka ya 2000 na hadi sasa umeenea na kuathiri jamii zetu kwa kiasi kikubwa.

Nchi changa zinajaribu kuruhusu, kutetea na kulinda vitendo vya maovu ya ‘mapenzi ya jinsia moja’ si kwa sababu ya kukinai uhalali wake bali ni kwa kutenzwa nguvu na mataifa makubwa. Hivyo kulazimishwa na kutokana na unyonge na udhaifu wa nchi zao kifikra na kuogopa kunyimwa misaada na kutengwa kimataifa huwa hakuna budi ila kuitikia mwito huu muovu. Ambapo tumeona nchi kadhaa kama Malawi, Uganda na Tanzania zilijaribu kujitutumua dhidi ya uovu huo lakini mwisho zikabwatika chini kwa khofu ya kuambiwa hawaheshimu Haki za Binadamu na kwa masharti ya kuwa wakikataa watanyimwa misaada. Mfano mzuri kauli ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola mwezi wa Novemba 2011 jijini Perth- Australia kuzitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo ikiwemo Tanzania kutambua rasmi uhalali wa ‘ndoa za jinsia moja’

Nchi za Magharibi katika kulazimisha nchi changa zikiwemo za Afrika kulinda na kutetea ushoga na mapenzi ya jinsia moja zinaunda taasisi zisizo za kiserikali yaani NGO’s ambazo huzifadhili ili kutetea kile wachokiita “haki” za mashoga na wapenzi wa jinsia moja. Zaidi ya hapo hutumia wasanii na watu maarufu na vipindi vya runinga, redio kupigia debe jambo hilo, kufanya matendo ya kuchochea na kuzoesha umma, kama baadhi ya wasanii wakiume kuvaa nguo za kike na kinyume chake, kuvaa hereni, kusuka nywele nk. Yote haya ni kuiandaa jamii kisaikolojia kukubali ushoga na walau kuona ni jambo la kawaida linalopaswa kukubalika kijamii.

Athari za ushoga na mapenzi ya jinsia moja

Suala hili la ushoga na mapenzi ya jinsia moja ni suala ovu, chafu, baya linaloathiri afya, utu, na linalomdogosha mwanadamu kwa kumfanya kuwa uwanja wa majaribio, kwa kuwa  nchi za magharibi wanaolipigia debe leo , ndio awali walilipinga. Lakini kubwa zaidi, halikubaliki na dini zote na linashusha hadhi, murua, heshima na ustawi wa mtu katika jamii.  Katika Uislamu jambo hilo ni dhambi kubwa na laana kubwa, na lau kuna utawala wake limewekewa adhabu kali, yaani ya kuuwawa watendaji wote wawili lau watathibitika.  Pia ni suala linalopingana na maumbile ya binadamu, malengo ya kuumbwa kwake na ni kinyume na mila, desturi na ustaarabu wa kibinadamu.

Mwito

Tunatoa mwito kwa serikali ioneshe kujali raia wake kwa kuwakinga na uovu huu, kwa kuwa tuna imani kuwa ina taarifa za kutosha kuhusu vuguvugu la matendo haya ikiwemo uwepo madanguro ya mashoga sehemu mbali mbali kama vile lililopo Tandale kwa Mtogole nk.

Pili, wananchi wa jamii na imani zote waache kuunga mkono na kukataa namna zote za kuhalalisha maovu haya ikiwemo kutotoa ushirikiano kwa watu na taasisi zinazohusika na kutetea vitendo hivi. Pia viongozi wa dini na watu jumla wapaze sauti zao kuinasihi serikali na kuwanasihi watu kujiepusha navyo na kwa wanaojihusisha na vitendo hivi vichafu kuacha mara moja na kutaka toba kwa Mola wao aliyetuumba, akatupa uhai na kwake tutarejea.

Aidha, wazazi na jamii kwa ujumla iwatunze watoto na kuwalea katika mazingira thabiti ili kuwakinga na uchafu huu kwa ustawi wao na mustakbali mwema wa jamii nzima

Mwisho, jamii na wanadamu kwa jumla itanabahi hatari na kutofaa kwa mfumo muovu wa kibepari na fikra zake za ‘uhuru binafsi’ kutokana na kueneza kwake uovu na uchafu unaoathiri kizazi na kuvunja hadhi ya binadamu kinyume na alivyotukuzwa na Muumba wake.

 ‘Na wanapoondoka wanakwenda huku na huku katika ardhi ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na kizazi. Na Allah hapendi ufisadi’ (TMQ 2:205)

‘Kataa ushoga na mapenzi ya jinsia moja: Ikinge jamii na familia yako dhidi ya janga hili’

 

Risala ya Wiki No. 121

25 Jumada al-awwal 1443 Hijri /29 Disemba 2021 Miladi

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

Front Page

#WahyiChimbukoLaThaqafaYetu

#KataaUislamuMamboLeo

Maoni hayajaruhusiwa.