Baadhi Ya Minasaba Ya Jumadal Al-Awwal

1.Ghazwatu Dhi- Ushairah.
Mtume SAAW aliongoza kikosi cha watu 150 au 200 ili kuandaa mazingira ya vita na kudhoofisha uchumi wa makureish, walipofika Dhi Ushairah walikuta msafara umeshapita. Bendera ya vita ilibebwa na Hamza bin Abdul Mutwalib na uongozi wa dola ulishikiliwa kwa muda na Abu Salam bin Abil Assad Al Makhzoumy
(Jumadal –ula au Jumadu –al Akhirah. Mwaka wa 2AH)

2.Ghazwatu Najd.
Mtume SAAW alifanya kampeni ya kijeshi katika mji wa Najd ili kuzima upinzani wa mabedui wa huko (Jamadul ula au Jamadul ul akhir katika mwaka wa 4AH)

3.Kutumwa Kikosi cha Zaid bin Harithah
Kikosi hiki kilitumwa na watu 170 kukabiliana na msafara wa makureish uliokuwa ukiongozwa na Abuu Al-Aws, mume wa Zainab bint Muhammad SAAW kabla ya kusilimu. Kikosi kilifanikiwa kuteka mali nyingi. (Mwaka wa 6AH)

4.Vita vya Mutah
Mtume SAAW alituma kikosi cha askari 3000 kukabiliana na jeshi la Warumi kulipiza kisasi cha mjumbe wake Harith bin Umair bin Alazd alietumwa kupeleka barua ya ulinganizi kwa Gavana wa waroma katika mji wa Busra.(Mwaka wa 8AH)

5.Kufariki dunia Bi Fatma bint Rasullulah (Mwaka wa 11 AH). Binti wa Mtume na kipenzi chake, Mtoto pekee wa Mtume SAAW aliyeishi mpaka kushuhudia kifo cha baba yake.

6. Kuibuka Vita vya Jamal (Tarehe 15 Mwaka wa 36 AH). Vita hivi vilikuwa baina ya Waislamu, wakati wa Khilafah ya Ali Ra.

Maoni hayajaruhusiwa.