Afisi Kuu ya Habari: Kampeni ya Kitengo cha Wanawake “KOMESHA Vitisho kwa Wanawake WachaMungu wa Kiislamu wa Kyrgyzstan!”
Mnamo 27 Juni 2020 M, Kamati ya Usalama wa Kitaifa ya Dola nchini Kyrgyzstan iliwakamata wanawake wa Kiislamu 8 wasiokuwa na tishio lolote katika mji wa Naryn kwa kushukiwa kuwemo ndani ya Hizb ut Tahrir, chama cha Kisiasa cha Kiislamu kinachofanya kazi kusimamisha serikali ya Kiislamu – Khilafah kwa njia ya Utume. Serikali ya Kyrgyzstan imekipiga marufuku chama hiki kwa madai ya kipuuzi kuwa ni shirika lenye misimamo mikali, licha ya kuwa hakijajihusisha na kitendo chochote cha ghasia, wala kusaidia kisa cha ugaidi tangu kuasisiwa kwake. Wengi wa wanawake walio kamatwa ni kina mama walio na watoto wadogo au walio na jukumu la uchunzaji wazazi wao wakongwe. Vikosi hivyo vya usalama viliwasaka wanawake hawa wa Kiislamu kwa njia ya aibu na ya kudhalilisha na kuwaweka katika baridi na njaa kwa kati ya masaa 6 hadi 12 katika kituo cha kizuizi. Wawili kati ya wanawake walio kamatwa wanaendelea kufungwa – Arunova Erkingul ambaye ni mchunzaji wa mamake ambaye alipata kiharusi na yuko katika hali mbaya, na Baktybek kyzy Mahabat ambaye ana tatizo la kiafya linalo hitaji matibabu ya mara kwa mara na ni mama wa watoto wawili walio katika chekechea. Endapo watapatikana na hatia ya mashtaka ya serikali, huenda wakakumbwa na miaka kadhaa gerezani.
Hakika ukamataji huu ni sehemu ya vita ambavyo serikali hii ya kitaifa ya kisekula ya Kyrgyzstan imevizindua dhidi ya Uislamu chini ya pazia hadaifu nayo ni kupambana na ugaidi na kutii maagizo ya mabwana zake katika serikali za Urusi na za Kimagharibi. Na katika jaribio lake la kutapatapa la kuupiga vita mwamko wa Uislamu ndani ya nchi yake na kuregesha usimamishaji wa utawala wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah, serikali ya Kyrgyzstan imekimbilia kuchafua sura ya da’wah ya Kiislamu na kuwatishia wanawake wa Kiislamu wasiokuwa na hatia na wenye kuheshimika ili kuchochea hofu kutokana na da’wah hii ya kulingania Dini ya Mwenyezi Mungu (swt).
Hakika uhalifu huu dhidi ya wanawake wachaMungu wa Kiislamu wa Kyrgyzstan HAUWEZI kupita bila uwajibikaji na kufichika kwa ulimwengu! Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir kimezindua kampeni hii muhimu kulingania kuachiliwa huru mara moja wanawake hawa wa Kiislamu wasio na hatia kutoka kwa seli za Kyrgyzstan na kukomesha mateso yanayoendelea na vitisho vya serikali ya kidhalimu ya Kyrgyzstan kwa mabinti waheshimika wa Ummah wa Kiislamu!
Mtume (saw) amesema,
الْمُسْلِمُ أَخُوْ الْمُسْلِمِ، لا يَظْلِمُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ
“Muislamu ni ndugu yake Muislamu: hamdhulumu, wala hamtelekezi.”
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Ijumaa, 02 Muharram 1442 H sawia na 21 Agosti 2020 M
Maoni hayajaruhusiwa.