Nasaha tukufu za Mtume (saw) kuhusu mwezi wa ramadhani

12

Imam Ali Ra. Amesema: Mtume SAAW alikhutubia katika ijumaa ya mwisho wa mwezi wa Shaaban, na katika khutba hiyo akaeleza haya yafuatayo:

“Enyi watu! Kwa hakika umekujilieni mwezi wa Allah kwa Baraka, Rehma na Maghfira”.

Ni mwezi  ambao mbele ya Allah ni bora zaidi kuliko miezi yote, na siku zake ni  bora zaidi kuliko siku zote, na usiku wake ni bora zaidi kuliko usiku wote, na saa zake ni bora zaidi kuliko saa zote. Ni mwezi mnaoalikwa kuwa wageni wa Allah, na mnakuwa ni watu wa kukirimiwa na Mwenyezi Mungu. (Katika mwezi huu) pumzi zenu ni sawa na kuleta tasbihi, usingizi wenu ni ibada, amali zenu ni maqbul na dua zenu ndani ya mwezi huu hujibiwa.

Basi muombeni Mwenyezi Mungu Mola wenu kwa nia safi na kwa moyo uliotoharika Akupeni tawfiq ya kufunga na kusoma kitabu chake (ndani ya mwezi huu.)

Kwa hakika mtu muovu ni yule atakaekosa maghfira katika mwezi huu mtukufu.

(Kwa mwezi huu) kumbukeni kwa njaa yenu na kiu yenu, njaa na kiu ya Siku ya Kiama. Na toeni swadaka kwa mafakiri wenu na masikini wenu, na waheshimuni wakumbwa wenu, na warehemuni wadogo wenu, na waangalieni jamaa zenu na chungeni ndimi zenu.

Yafumbeni macho yenu kwa yale yasiyoruhusiwa kutazama, na yazibeni masikio yenu kwa yasiyoruhusiwa kusikia.

Wahurumieni mayatima wa watu, ili mayatima wenu nao wahurumiwe pia.Tubuni kwa dhambi zenu. Nyanyueni mikono yenu kuomba dua wakati wa sala zenu, kwani wakati huo saa zake ni bora zaidi kuliko saa zote, ambazo Mwenyezi Mungu huwaangalia waja wake kwa Rehma. Huwajibu wanaomuomba kwa siri, na Huwaitikia wanaomnadi, na Huwajibu dua zao wanapomuomba.

Enyi watu!  Kwa hakika nafsi zenu zimewekwa rehani kwa mali zenu, basi zikomboeni kwa kuomba kwenu msamaha.

Na migongo yenu ni mizito (kwa dhambi) basi punguzeni kwa kurefusha kusujudu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ambae kudhikiriwa Utukufu wake ameapa kwa Utukufu Wake kwamba, Hatawaadhibu wanaosali na wanaosujudu, na kwamba Hatawatishia moto, siku watakayosimamishwa watu mbele ya Mola wa ulimwengu.

Enyi watu! mwenye kumfuturisha Muumini aliefunga miongoni mwenu katika mwezi huu, thawabu zake ni kama kumwacha huru mtumwa mmoja, na kusamehewa katika dhambi zake zilizopita. Pakasemwa Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Si kila mmoja wetu ana uwezo (wa kumfuturisha)? Mtume akajibu ogopeni moto hata kwa nusu ya kokwa ya tende, ogopeni moto hata kwa funda la maji.”

12 Comments
  1. Iyanna says

    We’re a group of volunteers and starting a new scheme in our community.
    Your website offered us with valuable information to work on. You have done a formidable
    job and our whole community will be grateful to you.

  2. It’s amazing to think about the potential savings and the ability to
    create complicated parts with such precision.

    It’s exciting to see how Mantle 3D can open up design possibilities that were previously too difficult to consider.

    It’s notable that Mantle’s 3D technology can deliver both high precision and cost savings,
    especially in complex projects where these factors are often at odds.

  3. read more says

    It is normally worth testing a handful of out to see which ones have the
    games you delight in the most.

    my web site; read more

  4. kobet says
  5. https://Www.redly.vip says

    We undoubtedly count on the number of operators to develop iin the near future.

    Also visit myy blog post; https://Www.redly.vip

  6. 온카 says

    Or, you can get any quantity by that calculus up to the amount supplied.

    my blog post :: http://pillersdorf.com/__media__/js/netsoltrademark.php?d=peatix.com%2Fuser%2F23083064

  7. http://O2R.Myhomesite.org/ says

    You may well want to verify your e-mail address by clicking a hyperlink sent to it.

    my web page: http://o2r.myhomesite.org/__media__/js/netsoltrademark.php?d=solink.in%2Fpqtf74

  8. more Info says

    Only UK on the web casinos licensed and regulated by The Gambling Commission are listed on this web page.

    my website https://clients1.google.co.in/url?q=https%3A%2F%2Fsolink.in%2F4tboxx

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.