Septemba 11, 2001: Kuasisiwa Rasmi Zama Mpya za Vita Dhidi ya Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tarehe 11/09/2001 ulimwengu ulishuhudia tukio linalodaiwa kuwa ni la kigaidi. Shambulio hilo lilihusisha kuripuliwa majengo mawili (twin towers) ya kituo cha biashara (WTC) mjini New York- Marekani.
Kupitia shambulio hilo ulifunguliwa ukurasa mpya na zama mpya za vita dhidi ya Uislamu kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi. Wakazidi maadui wa Uislamu wakiongozwa na Marekani kuupaka Uislamu kwa sifa mbaya na chafu ya umwagaji damu wa watu wasio na hatia.
Mabepari wakoloni makafiri wakashtadi na vita vyao vya msalaba kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, kwa kuvamia Afghanistan mwaka 2001, na kuua malaki kwa maelfu ya Waislamu kwa muda wa miongo miwili mpaka ilivyowabainikia kuwa hawawezi kupambana na Waislamu na kupata ushindi hapo wakabadili mbinu na kuanza mazungumzo ya amani
Kisha, Marekani wakavamia Iraq mwaka 2003 na ikaendelea hali hii, amma kwa idhini ya umoja wao wa kikoloni yaani UN au hata bila ruhusa yake. Ufaransa, kwa mfano ikavamia Mali mwaka 2002 kupitia maazimio namba 2071 na 2085 ya Umoja wa Mataifa ikishinikiza makoloni yake yaani Mauritania, Niger, Burkina Faso, Chad na Mali yenyewe kumuunga mkono.
Vita hii ya kikoloni ikapelekea kuundwa kwa sheria ya ugaidi ambayo iliasisiwa na Marekani na kulazimisha mataifa yote kuiunga mkono. Wakoloni ambao ndiyo wenye maslahi na vita hivi wakalazimisha makoloni yao katika Afrika na duniani kiujumla kuchukua sheria hii na kuitumia katika nchi hizo.
Watawala katika nchi zinazokoloniwa ambao ni mbwa wa wakoloni na vibaraka haraka sana wakaichukua sheria ya ugaidi na kuipitisha katika nchi zao, wakauwa wananchi wao, wakawatesa ili kuwaridhisha mabwana zao wakoloni huku wakipewa hongo kiduchu kwa jina la misaada ya kupambana na ugaidi.
Wakati tukitafakari kuhusu dhulma ya sharia ya ugaidi na vita vyake, pia namna leo hii damu ya Muislamu ilivyo duni kiasi cha kuweza kumwagwa hovyo bila kusita tusisahau sababu kuu ya kutukumba haya yote.
Bila shaka sababu kubwa inayowapa uthubutu wakoloni makafiri ni kukosekana mlinzi wa Ummah wa Kiislamu ulimwenguni. Huyu ni kiongozi wa Kiislamu (Khalifah) anayepewa bayah yaani mamlaka ya kutawala kwa Uislamu kupitia serikali ya Kiislamu ya kilimwengu.
Sababu hiyo pekee inatosha kwa Waislamu kufanya kazi ya kurejesha tena dola ya Khilafah, ngao yao itakayolinda rasilimali zao, damu, heshima, imani na matukufu yao na pia kuwaokoa walimwengu wote kiujumla kutokana na makucha ya dhulma na ukandamizaji kwa mujibu wa sheria za uadilifu kutoka kwa Muumba wa walimwengu.
Said Bitomwa
Risala ya Wiki No. 86
26 Muharram 1442 / 14 Septemba 2020 Miladi

 

Maoni hayajaruhusiwa.