21 Ramadhan

1. Siku kama hii tarehe 21 Ramadhani mwaka 40 Hijria alifariki dunia Khalifah wanne Ali bin Abi Talib kufuatia kupigwa dhoruba ya upanga, siku tatu zilizopita
(19 Ramadhan 40 Hijria) na mshenzi Abd al-Rahman bin Muljam al-Muradi wakati Imamu Ali akiswali swala ya Alfajiri.

2. Siku kama hii tarehe 21 Ramadhani mwaka 40 Hijria Al- Hassan bin Ali Abi Talib achaguliwa na Waislamu kwa kupewa baiya (kiapo cha utii) kushika nafasi ya ukhalifa kufuatia kuuwawa baba yake Khalifa wanne Sayyidna Ali Bin Abi Talib (ra). Hassan alishika nafasi hiyo kwa muda wa miezi saba, kisha kuachia ngazi, baada ya makubaliano ya sulhu baina yake na Muawiyah ambaye aliasi na kuzozana na Khilafah ya baba yake awali.
Baadhi ya Maulamaa wa Kiislamu wanamuhesabu Hassan kuwa ni miongoni mwa Khulafaa rashiduun (makhalifa waongofu)
Baada ya mkataba wa makubaliano na Bani Umayya , Hassan aliondoka Kufa (Iraq) na kurudi kuishi zake Madina, alibakia na kuishi Madina ila kwa safari za hapa na pale, mpaka mwisho wa maisha yake mwaka 50 Hijria.
Hassan alizikwa Madina katika makaburi ya Al-Baqi’, kando na kaburi la bibi yake mzaa baba Fatima bint al-Asad.

3. Siku kama hii tarehe 21 Ramadhan, 1389 Hijria (2/12/1959 – 2/12/1960) Sheikh Abdul Aziz Badry, mwanachuoni mkubwa wa Iraq na mwanachama wa Hizb ut-Tahrir aliwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani kwake (house arrest) na serikali ya Iraq kwa kipindi cha mwaka mzima. (2/12/1959 – 2/12/1960).
Baada ya kutoka kwenye kizuizi hicho, Sheikh aliendelea na msimamo wa kutetea Uislamu bila ya kutetereka, na akawekwa tena katika kizuizi kama hicho ndani ya mwaka 1961.
Mnamo mwaka 1968 Sheikh Badry alitekwa na wanausalama wa serikali ya Iraq usiku wakati akirejea nyumbani kwake na kuwekwa mahabusu ya Qasr Al-Nihay, aliteswa sana na serikali ikiwemo kukatwa ulimi na kukatwakatwa baadhi ya viungo vyake hadi kuuwawa shahid ndani ya mwaka 1969. Baada ya siku 17 watesaji walikuja kuubwaga mwili wake nje ya nyumba yake wakidai kafariki kwa maradhi ya moyo.
Aliuwawa shahid mnamo mwezi wa Rabi’ Al-Awwal 1389 A. H /1969 A akiwa na umri chini ya miaka 40. Aliswaliwa katika Msikiti wa Imamu Abu Hanifah kuswaliwa na kuzikwa.

21 Ramadhan 1441 Hijri – 14 Mei 2020 M

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.