11 Ramadhan 1441 H
بسم الله الرحمن الرحيم
Siku kama hii 11 Ramadhan, 1441 Hijri / Oktoba 7, 2001, dola ya Marekani, kiongozi wa ukafiri ulimwenguni ilivamia ardhi ya Waislamu ya Afghanistan mara baada ya shambulizi la Septemba 11 2001.
Uvamizi huo wa Marekani pia uliungwa mkono na washirika wake hususan Uingereza ambayo ilishikamana na Marekani tangu mwanzoni mwa uvamizi.
Vita hivyo vya Afghanistan ukawa mwanzo wa vita virefu mpaka leo.
Marekani ilidai kwamba malengo ya vita hivyo ni kusambaratisha kundi la Al-Qaeda na kuizulia kuwa na fursa ya kufanya harakati zake ndani ya Afghanistan kwa kuondoa utawala wa Taliban madarakani.
Raisi George W. Bush aliitaka dola ya Taliban kuwakabidhi kwa kumsalimisha Usama bin Laden na kuwafukuza Al-Qaedah. Utawala wa Taliban ulikataa kumtoa Usama bin Laden mpaka pale Marekani itakapotoa ushahidi bayana wa kuhusika kwake na tukio la Septemba 11.
Msimamo huo wa Taliban ulikataliwa na Marekani , wakiuita ni msimamo usio na maana na ni mbinu ya kucheza na muda, kisha wakaanzisha uvamizi kwa jina la ‘Operation Enduring Freedom’
11 Ramadhan 1441 Hijri – 04 Mei 2020 Miladi
Masoud Msellem
Maoni hayajaruhusiwa.