Mlipuko wa Corona Ulivyofichua Uovu wa Mataifa ya Kibepari

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa miezi kadhaa sasa ulimwengu unapita katika hali ngumu ya kukumbwa na maradhi yanayoenea kwa kasi mashariki mpaka magharibi. Maradhi haya yanayojulikana kama Corona ambayo kwa mara ya kwanza yaliripotiwa nchini China katika mji wa Wuhan yameenea kwa kasi katika meneo mengi na kusababisha athari kubwa za kijamii hata kiuchimu.

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa idadi ya maambukizi imeoogezeka kwa kasi na kufikia takriban watu 105,530 huku idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo ikifikia watu 7,893 Watu waliopata nafuu ni 81,085. (WHO Update 17th March 2020.)

Kutokana na mfumo wa kirasilimali unaotawala dunia leo kupupia maslahi hata kwenye mambo nyeti yanayohusu uhai wa watu, hivi karibuni makampuni makubwa yanaotafiti tiba na kinga ya magonjwa mapya kutoka Ujerumani na Marekani yameonekana yakigombea hati miliki ya kutengeneza tiba na kinga ya virusi hivyo hadi kufikia kutaka kupelekana mahakamani kutokana na kuwa kila mmoja kutaka kupata maslahi makuu pasina kuangalia wepesi wa upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwa watu wa chini (AFP)

Aidha, kauli ya hivi karibuni ya Msemaji wa serikali ya China kuhusu njama chafu za Marekani kupandikiza virusi hivyo nchini China inadhihirishwa kwa kiwango gani mfumo huu unaotawala ulimwengu ulivyopindukia daraja la unyama kwa kuwa tayari kuuwa na kusababisha madhara kwa jamii ya kibinadamu.

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu nchini China Yang Jiechi hivi karibuni amempigia simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na kuionya Marekani kuwa hujuma wanazozifanya katika kudhoofisha China kwenye juhudi za kupambana na virusi vya Corona kamwe hazitofanikiwa (Xinhua) .
Aidha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa China bwana Geng Shuang alitoa kauli ya kulishambulia Shirika la Kijasusi la Marekani CIA kwa madai ya kuhusika kwake kusambaza virusi hivyo nchini China. Taarifa hiyo ya China ilienda mbali zaidi na kusema kuwa kuna ushahidi wenye nguvu virusi vya COVID 19 (Corona) vilitengenezwa na wanasayansi wa Marekani. Kwa mujibu wa mwanadiplomaisa huyo uchunguzi uliofanywa na wachunguzi wa mambo kutoka china (Experts) unaonyesha kuwa makala iliyochapishwa nchini Marekani katika Jarida la Journal nature medicine mwaka 2015 ilithibitisha kuwa wanasayansi wa kimarekani waliweza kupata aina mpya ya virusi vya corona ambavyo moja kwa moja vitakuwa na madhara kwa binadamu. (Medic Forum)

Hali hii inafichua uovu wa mataifa ya kimagharibi pupa yao ya kutaka maslahi makuu hata kama hali hiyo itapelekea kufa, maradhi na madhara mengine katika jamii. Amesema kweli Mola pindi aliposema

وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّهُ لاَ يُحِبُّ الْفَسَادَ).

“Na wanapotawala wanakwenda haraka katika ardhi kufanya uharibifu na kuangamiza mashamba na kizazi na Mola hapendi waharibifu” (TMQ 2:205)

Huo ndio mfumo wa kirasilimali/ubepari uliofanya manufaa kuwa ndio kipimo katika matendo na hufanya pupa na kila njia chafu kufikia manufaa ya kiuchumi pasina kuangalia heshima ya jamii sawasawa katika kufikia manufaa hayo kunaweza kusababisha vifo au mmomonyoko wa maadili kama ilivyo leo katika hoteli za kitalii kasino nk.

Katika upande wa mfumo wa Kiislamu wenye sifa ya uadilifu hulazimisha pindi mja anapotenda vitendo vyake daima kuvifungamanisha na fungamano la Mola wake na lengo la kutenda ni kupata radhi za Allah SWT.

Jambo hili ndilo lililopelekea kutokuwepo kwa tabaka baina ya watawala na watawaliwa hasa katika kunufaika na huduma za afya na kutokuwepo ugumu wa upatikanaji wa vifaa tiba kwa watu wote.

Imepokelewa kuwa kiongozi wa Kiislamu Khalifah Umar r.a aliuguwa maradhi makali, matabibu wakamtaka atumie asali kutokana na maradhi yake, na ilikuwa Baitul mali (hazina) wakati huo imejaa asali kutoka miji iliyofunguliwa. Umar RA. alikataa kutumia asali ile kama madaktari walivyomtaka kwa kuchelea kutumia mali ya Umma pasina idhini. Bali Umar ra. akawakusanya watu kisha akapanda kwenye mimbari akasema siwezi kutumia asali hii mpaka mnipe idhini ikiwa hamtotoa idhini sitotumia, watu wakalia kwa pamoja wakampa idhini ya kutumia na kunufaika na asali ya baituli mali (Tarekh Twabar).

Pia Uislamu umehimiza kusaidiana wakati wa dhiki zaidi kama wakati huu wa mlipuko wa Corona na katika haya hupata baraka na thawabu mara dufu. Kwa kuzingatia kuwa viongozi ndani ya dola yake ni masuul (wenye kuulizwa) basi huchunga sana katika usimamazi wa jamii husika.

الَّذِينَ يُنْفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنْ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ (آل عمران: 134)

“Ambao hutoa katika hali ya wasaa (nzuri) na katika hali ya dhiki na wanazuiya ghadhabu na wenye kuwasemehe watu (wenye kuwafanyia ihsani), na Mwenyezi Mungu hupenda wafanyao ihsani” (TMQ 3:134)

Na imepokelewa Amesema Ibn Jarir Twabar katika kitabu chake cha tarekh kuwa Khalifah Umar r.a pindi Waislamu walipopata ukame na ulikuwa ni wakati wa dhiki na shida na upungufu wa chakula mwaka wa ukame alikuwa hali chakula isipokuwa mkate mkavu na mafuta nacho ni chakula duni kisichokuwa na virutubisho mpaka ngozi yake ikawa nyeusi na kusinyaa, alikuwa akisema kiongozi mbaya ni yule anayeshiba na watu wake wana njaa.

Huo ndio Uislamu unaowandaa viongozi wao kuwa na khofu ya Muumba na kuwatumikia raia wao kwa kuhakikisha wanapata huduma msingi kabla ya kuangalia nafsi zao kwanza. Tofauti na mfumo unaotawala leo uliofanya watu masikini ni wenye kutaabika na kufanywa kuwa daraja la watu wa juu kupata maslahi yao kupitia watu hawa.

Ust. Issa Nassib

#UislamuNdioUfumbuziSahihi

Risala ya Wiki No. 73
28 Rajab 1441 Hijri / 23 Machi 2020 Miladi

Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania
https://hizb.or.tz/
https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.