Kuongezeka Talaka Katika Miji ya Waislamu
Kumeripotiwa taarifa za kuongezeka sana talaka kisiwani Lamu, Kenya. Eneo linalokaliwa na takriban Waislamu wote. Pia siku za nyuma taarifa kama hizo ziliripotiwa kuhusu visiwa vya Zanzibar.
Nukta za kuzingatia katika qadhia hii:
1.Kweli jamii za Kiislamu zina misukosuko katika upande wa kijamii ikiwemo kuvunjika ndoa, lakini hili sio jamii za Kiislamu pekee, bali kila mahala, na kimsingi si kwa matakwa yetu, bali ni kutokana na athari na fikra zinazotokomana na mfumo wa kirasilmali/ kibepari. Fikra kama za uhuru na usawa baina ya wanawake na wanaume, fikra za kujiongezea (maslahi), uroho wa vitu vitu (materialism) nk. zimeathiri vibaya kila mahala. Kwa mfano kabila la wakikuyu, wanajamii wake wanalikimbia kuowa wanawake wa kabila hilo kutokana na athari za fikra za kigeni kwa wanawake wao :
https://www.cnyakundi.com/alarm-over-rate-of-kikuyu-men-ma…/
2. Hata kama katika jamii zetu tuna talaka nyingi ,hilo bado ni ushahidi kuwa jamii inathamini ndoa, na wanachukulia kuwa ndio mahusiano halali baina ya mwanamume na mwanamke.
3.Kukata shauri kuwa kila talaka ni tatizo huo ni mtazamo wa kinaswara, wanaoichukulia ndoa ati ni pingu ya maisha. Uislamu unahesabu kwamba kuna talaka nyengine ni suluhisho. Kwa mfano, jee kama mume kashindwa kumuhudumia mke wake kutokana na sababu moja au nyengine afanye nini ?
4. Uwepo wa talaka, maana yake pia Uislamu unatambua maumbile halisi ya mwanadamu, kuwa upo uwezekano wa mwanadamu kubadilika, na kamwe mwanadamu sio malaika. Na ndio pia kuna hukmu za lian, zinaa nk.
27 Oktoba 2019
Maoni hayajaruhusiwa.