Yuko Wapi Mansa Kankan Musa wa Zama Hizi?
Zama Waislamu walipokuwa na hatamu na izza duniani, waliujaza ulimwengu kwa kheri na baraka. Neema zilienea katika mgongo wa ardhi kiasi kwamba watu waliishi chini ya uadilifu wa sheria tukufu za Muumba. Sheria ambazo huwasimamia wanadamu wote pasina kujali tofauti ya dini, rangi wala kabila .Kila mwanadamu aliyeishi wakati huo hata kama hakuwa Muislamu alinufaika na neema zilizokuwa zimesheheni wakati huo. Kama tujuavyo neema za Mola hukithiri zaidi pindi watu wanapokuwa wachamungu na mujtamaa unapokuwa upo karibu na Muumba wao. Amesema Allah Taala:
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنْ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
“Lau kama watu wa miji wengeamini na kumcha Mola basi tungefungua baraka nyingi kutoka mbinguni na ardhini lakini wamekadhibisha basi tukawaadhibu kwa yale waliyokuwa wakiyachuma” (TMQ 7:96).
Kwa sera nzuri za Uislamu ulitengeneza mujtamaa wa watu wenye maisha mazuri lakini kiasi kwamba wenye kipato cha juu hawakusita kuutumia utajiri wao kwa ajili ya Mola wao.
Tofauti na baadhi ya matajiri wa leo walioathirika na mitazamo hasi ya kibepari kama ile mitazamo ya kina Adam smith (no free lunch) Hakuna chakula inayowasukuma matajiri kutokua na huruma kwa masikini na mafukara na wako tayari kupata kwa njia yoyoye ile hata kama italeta maafa kwa wanadamu (end justify the means).
Jamii, viongozi na ulimwengu kwa jumla unafaa ujifunze huruma, uadilifu na uongozi thabiti wa mtawala Mansa Kankan Musa (1280 – 1337) kiongozi muadilifu na tajiri mashuhuri wa utawala wa Himaya ya Mali wa wakati huo (Afrika ya Magharibi) aliyetawala kwa miaka 25 (1312 – 1337). Inakadirika mnamo karne ya kumi na nne alikuwa tajiri mkubwa zaidi duniani kiasi cha kumiliki utajiri kwa kiwango cha leo wa Dolari za kimarekani billioni 400.
Katika safari zake kadhaa alipokuwa akienda Hijja alikuwa na msafara mrefu na akibeba pesa nyingi kwa ajili ya kuwagawia mafukara na masikini walioko njiani. Na alipokuwa akirejea kutoka Makka, alirejea na vitu mbalimbali kama nguo kwa ajili ya kuwagawia masikini njiani.
Mwanahistoria maarufu James Lewis anaelezea tukio kubwa adhimu la Hijja ya Mansa Kankan Mussa iliyofanyika mwaka 1324 akiwa ameambatana na watu elfu sitini na watumishi zaidi ya elfu 12,000 ambao kila mmoja wao alikuwa amebeba vipande vinne vya dhahabu vya kilo 1 vikiwa vimefungwa kwenye vitambaa. Msafara huo ulikuwa na zaidi ya ngamia mia moja wakiwa wamebeba kati ya pauni 50 mpaka mia 300 (puani moja ni sawa na gram 454 za dhahabu) Kankan alikuwa akigawa kila njia anayopita pesa kwa masikini mpaka alikuwa akigawa pesa ndani ya miji ya Madina na mji mtukufu wa Makka. (James Lewis )
Tukio jingine adhimu la Mansa Kankan Musa lililowashangaza wengi ni pale alipokwenda vitani maeneo ya Ethiopia akiwa mtawala wa Kiislamu aliyekuwa akisimamia wilaya maarufu Sudanic State eneo liliojumuisha pia na Afrika ya Magharibi na baadhi ya maeneo ya Chad. Katika tukio hilo la aina yake alitoka Mansa Musa na jeshi lake kwenda kukomboa mji uliokuwa umetekwa na wakristo wa Ethiopia, jeshi lake lilifanikiwa kuukomboa mji huo na kuwafurusha askari wa kikristo na kufanikiwa kuwateka Mkuu wa Jeshi la wakiristo, mke wake, watoto wake pamoja Kasisi Mkuu.
Tahamaki akaja kijana mdogo aliyepanda juu ya farasi mpaka kwa Mansa Kankan Musa, akimwita ewe.. bwana mkubwa, ewe bwana mkubwa ! Kankan akamuuliza yule kijana kwani wewe Muislamu? kijana akajibu ndio ewe bwana mkubwa, yule kijana akaendelea kusema akiwatazama kwa macho yake Mkuu wa Jeshi la kinaswara, hakika Mkuu wa Jeshi na Kasisi wamemteka mama na dada yangu. Akasema Kankan kuwaambia wanajeshi wake waiteni Mkuu wa Jeshi pamoja na Kasisi kwenye hema langu. Walipoingia akawauliza yuko wapi mama na dada wa huyu kijana? Akasema Mkuu wa Jeshi la Kinaswara baada ya kusita kusita kuwa waliondoka pamoja na msafara huko wakifanya kazi maalum. Akasema Kankan kumwambia Mkuu wa Jeshi la kinasara tuma ujumbe warudishwe wakiwa na msafara wa farasi sabini na ngamia sabini na wanajeshi elfu moja wakiwasindikiza, na utabaki wewe na kasisi mkuu hapa mkitumikia kazi za Waislamu mpaka arejee huyo mama na binti yake. Akasema tena kiongozi wa jeshi la kinaswara wakiwa wako wapo mpaka leo tutawarudisha, wakiwa kinyume na hivyo itakubidi ulipe fidia ya pesa dhahabu na mali nyingi kwa Uingereza na Ureno ili waweze kuachiwa.
Akajibu Mussa Kankan kwa hasira na ghadhabu iliyodhihiri kwenye macho yake sikia ninachosema, naapa kwa Allah ambae hakuna Mola ila Yeye, lau mkinipa Uingereza kuwa kiatu changu cha kulia na Ureno kuwa kiatu changu cha kushoto siwezi kukubali diya. (fidia ya mtu aliyeua) chini ya kichwa cha mfalme mmoja kwa ajili ya binti, na kichwa cha mfalme mwingine kwa ajili ya mama yake.
Baada ya Mussa Kankan kutuma ujumbe wa Mkuu wa Jeshi pamoja na Kasisi, akaletwa mama na binti yake kwa Rehma za Mola bado wakiwa hai.
Akasema Kankan kuwambia mateka wa kinaswara, vita baina yetu na nyinyi vitabakia na tutachelewa kutangaza ushindi mpaka mama na binti yake wafike kwenye makaazi yao. Ukatumwa msafara wenye kuwasindikiza mama na binti yake mpaka nyumbani kama alivyoagiza Kankan.
Kisha Mansa Kankan akasema kuwaambia mama na binti yake, jee mmetusamehe kwa yale yaliyotokea kwenu (kutekwa kwenu), mama akajibu ndio tumekusamehe na kwa kila fakhari ewe bwana.
Akasema Kankan Musa ninaapa kwa jina la Mola, nafsi yangu haiwezi kuridhia mwanamke wa Kiislamu alale mateka nje ya nyumba yake hata usiku mmoja. (James Lewis)
Hao ndio viongozi wa Kiislamu waliotangulia, licha ya neema nyingi walioneemeshwa na Mola wao hawakubweteka na kula neema za dunia bali walizitumia kwa kuwasaidia wanyonge na masikini kwa kuzitoa katika njia ya Mola wao katika kuhami damu na matukufu ya Uislamu. Leo tuna jukumu la kuibadilisha hali kwa kupigania kurejesha izza yetu kwa kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah itakayotoa viongozi waadilifu kwa Umma utakaoufungua mji wa Roma katika mikono ya Waislamu kama alivyobashiri Mtume SAAW.
26 Agosti 2019
Ust. Issa Nasibu
Maoni hayajaruhusiwa.